Ushuhuda mwanaume mwenzenu: Nilioa Single Mother yalioyonikuta ni haya. Nilichukua uamuzi huu...

Record Man

JF-Expert Member
May 25, 2023
471
844
Habari jf mimi nina umri wa miaka 40 sasa, ni member wa jf mda tuu ila nimekuja na id hii mpya kuleta kisa changu kilichonikuta na uhamuzi niliochukua. Mimi ni mmoja wa wapondaji sana wa single mother humu jf coz yalinikuta mwenzenu. Nitajitahidi kuelezea kwa ufupi.

Mwaka 2009 nilikutana na binti mmoja jina lake linaanzia na M.
Aisee nilipenda sana yule dada tena haswa haswa nilifanikiwa kuingia kwenye mahusiano na yeye na alikuwa ananieleza vingi sana kuhusu familia yake hata mimi nilimueleza pia kwa uwazi. Ila hakuniambia kuwa alikuwa na mtoto hakaja kuniambia baada ya mwaka mmoja na nusu tupo deep relationship nilishituka ila baadae nikaona mtoto sio shida, nilimuuliza ilikuwaje ukapata mtoto alinieleza tuu kuwa alikuwa kwenye mahusiano na jamaa mwishowe katika kufanya sexy " akajikuta tuu mimba hiyo , ila hakupanga kuwa na mtoto ilitokea tuu" tena alienda mbali na kuniambia walijaribu kutoa ili mda ulikuwa ushapita wakaambiwa ukiitoa sasa utapata madhara so akaamua kuacha tu ili azae.

Hakaniakikishia kuwa jamaa aliyezaa nae walishaachana ila wapo tuu kuhudumia mtoto na mawasiliano kuhusu mtoto. Nikimwangalia binti ni mtu aliyenushauli vitu vingi nikaona isiwe shida ngoja niuoe tuu.

Nilienda kuwaambia home kuwa nimepata mtu ila baadae nikawaambia kuwa anamtoto tayari, Mama kwanza kashituka.., Baba akaniambia kuwa "kuoa mwanamke mwenye mtoto sio shida na sio vibaya ila ni muhimu kujua huyo mwanaume aliyezaa nae ni mtu wa aina gani, tabia yake ipoje hata na familia yake ni muhimu kujua ni watu wa aina gani" je ufanya hilo kijana wangu. Mimi nikasema tuu binti kashanipa information zake zote nimelizaka nazo, mzee akasema sawa ila tuu kuwa "mkini".

Mama yeye ndo akasema yani umekosa kuwaona mabinti wote hawa mpaka ukaona huyo. Mama akaniambia kuwa "mwanangu sikiliza sisi wanawake ukiona tumezaa na mtu huwa tumempenda hatuzai na mwanaume ambaye hatumpendi". Mama yangu mimi ni mswahili alienda mbali na kuniambia "mwanaume akimkuna vizuri mwanamke huwa tunajisahua kuwa na mimba tunaweza kupata".

Ila baadae nikaona tu maneno haya ni mtu mzuri, mimi nikaoa bhana
Baada ya ndoa akaniambia tumchukue mtoto mimi nikasema fresh tuu. Dogo tukawa tunakaanae home na hata shule mimi dogo nikawa nampeleka mimi na gari na mke wangu kumpeleka kazini.

Matatizo yakaanza baada ya mke wangu kupata ujauzito. Simu zilikuwa nyingi za Dada wa jamaa aliyezaa na mke wangu walikuwa wanapiga simu sana wanataka kuongea na shangazi yao kuna kipindi simu zilizidi mpaka nikaona kero ila nikafumbia macho.

Siku moja mke wangu akasema kuwa anataka kwenda Beach ununio nikasema sawa akamuchukua dogo wakaenda kule Beach ununio mimi nilikaa home nikaona aaa iweje waende pekeao ngoja na mimi niende nilipofika kule kwenye bar moja hivi nilimkuta mke wangu, dogo na jamaa aliyezaa nae na Dada wa jamaa wapo wamekaa na wana pata vinywaji na chakula, sikutaka niende nikakaa pembeni nikawa nawaangalia walikuwa ni watu wa furaha utafikili ni familia moja.

Jioni home nikamuuliza mke kuhusu hilo akasema tu tulikutana mtoto pia ni muhimu kuwa karibu na wazazi wake. Nikaona isiwe jambo. Ila nikamwambia kwanzia leo kitu chochote kuhusu mtoto na mzazi mwenzio uniambie kama mnataka kukutana na kumpeleka mtoto nishirikishe mimi. Akasema sawa.

Baada ya kujifungua tukapata watoto mapacha wakiume tupo tukakubaliana jina moja nitoe mimi na lingine yeye. Mimi nimetaja langu ila yeye alilotaja ni jina la mzazi mwenzie, mimi nikashituka kwa nini unataka hilo jina. Na jina la jamaa ni la kabila lao nikamuambia hilo jina ni la kabila mimi sio kabila hilo basi akajishitukia yakaisha.

Siki moja nilikwenda kumcheki kwa mama yale coz alikuwa anapata uzazi kwao ile nimefika nikamkuta na jamaa anaondoka pale kwao amempelekea zawadi mama mkewe wangu vitu vingi kama Vitenge na mambo mengine tukapisha tuu tukasalimiaana.

Aaa nikashituka madogo si wangu nini. Japo baadae hakafanana na mimi na kwa mbali kama wanafanana na mzee wangu.

Baada ya mke kurudi home nilitafuta mfanyakazi awe anasaidia kazi home. Siku moja nilichelewa kurudi pale home nikarudi night nikamkuta mdada wa kazi anaangaika na kuosha vyombo vilikuwa vingi sana.

Nikamuuliza kurikoni mbona vyombo ni vingi hivyo akaniambia kuwa walikuja Wageni hapa home, nikamuuliza akina nani akaniambia ni wadada wawili, kumbe walikuwa ni Dada za jamaa walikuja home.

Mimi nikamuuliza wifi inakuwaje leo mbona hukunimbia kuhusu hilo akasema tu walinishitua kuja walikuja kumsalima mtoto wa kaka yao. Mimi eeee.

Kuna muda mfanyakazi alaipata shida akarudi kwa na mimi nilisafili kwenda mkaoni, ile nimerudi jioni tunakula msasi mezani dogo akalopoka mama Baba atakuja kulala lini kama alivyokuja juzi. Daaa ile kitu ilinikata maini kuendelea kula nilichukia hatari , hasira nilizopata sijawahi kuzipata siku ile , ila nilijikaza kiume.

Baada ya kuingia chumbani nikamuona sura initia hurumu ya mke wangu nikamuuliza ilikuwaje akaanza kujitetea kuwa dogo anzingua tu alikuja kumuona mtoto tu ila alichelewa kuondoka tu, hakukuwa kuna kibaya chochote. Daa nikawa nimeshaelewa nishagongewa hapa tayari. Muda huo watoto wangu wana 7 mouth. Nikamwambia mimi sio mjinga kuniambia hakukuwa na chochote.

Kuna siku jamaa alipiga simu na kutaka kuongea na mwanae alimpigia mke wangu mimi niko nje nasikiliza Baba anamwambia mwanaume kuwa unakula vizuri huko, anakupiga, anakusumbua, zawadi anakupa, na akamwambia uwe unamwambia mama awe anakuleta kwa Babu na Bibi na kwa Baba.

Tangu siku hio dogo akawa anang'ania karibu kila siku kuwa anataka kuongea na Baba yake, asubuhi na hata jioni anataka kuongea na Baba yake.

Kipindi kile jamaa alikiwa hajaoa bado. Sasa hizi simu za dogo kutaka kuongea na Baba yake ikawa ni kero kwangu, nikamwambia mke wangu ni vyema mtoto ukamwambia sio iwe kila siku tuu, akanijubu yule ni Baba yake anahaki ya kuongea nae mda wowote. Nikamwambia unaonaje mtoto ukampeleka huko. Kasema basi nimukuelewa nitamfundisha mtoto. Sasa baada ya mapacha wangu kuwa na umri wa miaka kama 1 na nusu.

Siku moja nimekaa na friends jioni kama saa 11 jioni Naperuzi facebook nikakuta picha imetumwa kama 3 minutes ago kwenye account ya dada wa jamaa yule aliyezaa nae ni picha nyingi tu ya mzazi mwenzie na mke wangu wapo kwenye sherehe ya birthday ya dogo mimi nilikuwa sijui tena yupo mpaka mama mkwe wanasherekea na kulishana kike kabisa na kukumbatiana, aisee niliruka kama ukichaa hivi nirurudi home akiri kama ipo kama nusu.

Wakarudi na dogo home na mapacha nikamuuliza ilikuwa ukaenda bila taarifa yangu wakati tulikubaliana unishirikishe na mimi nivyo vitu, akanijibu haya mambo hayakuusu coz wewe uhusiki maana kule wewe hawakujui ila wanakuona tu, aisee yale maneno nilikasirika sana nikajikuta nimempiga cofi moja matata. Akakasirika na kuondoka pale. Mimi si nikamuacha tuu coz nilikuwa na hasira. Home siku ile nilala pekeangu coz aliondoka na mdogo. Asubui nikajua kuwa atakuwa kaenda kwao. Nikamua kwenda kwao.

Nimefika kwao nikamkuta mdogo wake akaniambia kuwa Dada hajaja hapa home. Daaa niliondoka nikarudi home akili ikasema inawezekana kaenda kwa jamaa yake. Baada kama ya 1 hour akarudi na hasira sana. Nikamuangalia tu.

Baada ya siku kama 2 hivi akaniaga kuwa anaenda town nikasema sawa jioni akarudi na mizigo mingi sana ya dogo. Nikaangalia tu, baada kama muda tu dada wa jamaa akapiga simu kutaka kuongea na dogo, dogo akasema leo tumeenda na baba na mama Beach tumekula vyakula vingi na kuninulia vitu kibao.

Nikaacha tu ila nikaanza kumkumbuka maza, kumbuka hayo yote yanatokea sijawahi kuwaeleza home. Nilimuambia mke wangu kuwa unajua wewe ni mke wa mtu akaema ninajua sana, ila ninahitaji mtoto wangu have karibu na Baba yake wewe sio Baba yake. Na usinifundishe.

Nikamwambia basi mpeleke mtoto kwa Baba yake au kwa Babu zake kesho asubui akaamuka na hasira hata mtoto shule hakumpeleka akaenda kwao akamwambia kuwa mume wangu hamataki mtoto na kumpeleka mtoto kwa wazazi wa jamaa kule na kuwaleza, siku ile hakurudi home , kwanza alichelewa hakulala kwao hata kwa wazazi wa jamaa yake , najua alilala kwa jamaa.

Niligombana nae sana mpaka Mama yake yani mama mkwe wangu akaniambia kuwa" Mwanaume acha wivu kwani ulipo muona mtoto wangu alipata mtoto kwa njia gani, hujui kuna mwanaume ndo alimpatia baraka ya mtoto, acha wivu wa kijinga , yule ni kama mume mwezio muheshimu".

Baba wa binti akamwambia binti yake kuwa wewe umeolewa heshimu ndoa yako sawa. Alivyorudi home akaongeza simu kuwasiliana na Dada ya jamaa wanaongea kuhusu mtoto na kufungua biashara zao na mambo mengine tena wanaongea mimi nasikia kabisa nilivumilia kama 5 months naangalia tu na kuvumilia.

Nikiaangalia page za facebook za Dada wa jamaa wao wanopost tu picha za Mkewangu na mtoto wa kaka hayo na kuandika maneno kuwa " Hata kama ni mume mpya acha wivu umekuta watu wanamahusiano yao".

Kuna siku nyingine dogo alikuwa anapata kipaimara sherehe ilifanyika kwao jamaa sasa sikupewa tahari nilikuja kuona mke wangu kawepa mapicha picha whatApp status.

Tuligombana sana coz zile picha zilikuwa na maudhui mambayo ukiangalia ni kama mke na mume. Daaa nikikumbuka kapata hasira sana. Kuna siku ilikuwa ni siku ya father day kama alichukua pesa yangu niliyompa ya kufanyia watoto shopping anaenda kununua zawadi za mzazi mwezie na ile pesa ilikuwa ni kama 340k.

Nilikuja kujua baada ya kuona status ya mzazi wenzie kupitia simu ha mke wangu na watoto hakuna chochote walichofanyiwa. Nikamuuliza akaniambia ukitaka pesa yako nitakurudishia.

Nisiwachoshe ila nilifanyiwa vitibwi vingi sana tena sana na baby dady, mtoto mwenyewe , baby mama, dada za jamaa, na mzazi wa kike wa mke wangu.

"Nilikuwa naambiwa tuu acha wivu huyu ni mume mwenzio"

Kuna kipindi niligombana nae sana akaondoka home kama 3 mouth na kwenda kukaa kwa jamaa, watoto wangu akawapeleka kwa mama yake.

Kwa kuwa jamaa yake alikuwa hajaoa kipindi naangaika mimi na hizo drama. Baadae alipata kuhamishiwa mwanza kikazi na kuamua kuoa na kumchukua mtoto wake na kwenda nae mwanza.

Huku mimi mke wangu sina hamu nae tena coz ya drama nyingi nikaanzisha mahusiano na Mdada mmoja hivi kwa ajili ya kujiliwaza na alinisaidia sana huyo dada.

Baada ya jamaa kwenda mwanza mke wangu ndo akaanza kujirudi wakati mimi simuitaji kabisa.
Akalalamika tuu aa shetani alinipitia nilijisahau naomba tuendelee nikamwambia mimi na wewe basi sikuhitaji tena wewe tuu chukua vyako ondoka kwangu, nilimtoa mwa nguvu home. Alienda kuwaeleza kwao.

Baba yake aliniita ili tumize ishu, ila msimamo wangu ulikuwa ni uleule sikutaka kubadilika hata tone. Mama yake akawa anomba pia na radhi kwa yale yaliotokea ila mimi wala.

Nikaondoka pale na kwenda home kuwaelezea wazazi waliniangalia tuu japo wao ni wazee sana, Baba akanimbia tuu pole. Mama akanyamaza kimya.

Nilimueleza dada yangu akaniambia tu " mdogo wangu kwani wewe ulifikili mtoto alipataje kuna mwanaume kama wewe alimlalia juu akapatikana mtoto, hukufikilia hilo".

Nimetoka hapo Mama akanitumka sms kuwa nilikuambia hapa home na baba yeko ulikuwa mbishi.

Wazazi wa binti walinita tena pamoja na viongozi wa dini ili kusuruhisha ila mimi msimamo ni ule ule , nikawaonyesha sms ya mama aliyonitumia nikawaambia haya yote waliyonitokea sikuwaambia home coz niliona aibu kwa vile walinishauri sana ishu ya kuoa mwanamke mwenye mtoto. Ila mimi nilitumia nguvu tuu.

Baba yake binti akasema tu okay sawa kama umeamua hivyo sawa coz ni chaguzi zako, basi mimi nikaondoka zangu.

Ila tu msahama na vilio vilikuwa vingi sana , na kuomba turudiane tulee watoto wetu mimi nikamwambi basi ni mwisho.

Nilioa tena na baada ya kuoa nikamwambi mimi ni mume wa mtu na huyu ni mke wangu tena nilimuota dukani kwangu pasipo kujua nikamtambulisha nikamwambi ukitaka kujua hali ya watoto wetu basi uongea na mke wangu sio mimi labda kuwe na ishu ya muhimu.

YAPO MENGI YALITOKEA SIJAELEZA MPAKA KUCHUKUA UHAMUZI HUO. NITAELEZA KATIKATI YA UZI.

SORRY KWA UREFU WA ISSUE YANGU.
 
Pole sana kaka japo uzi ni mrefu.
Ila ukiona watu wamezaa kabisa kabla ya ndoa hao walikuwa deep relationship yani deep ile deep mpaka wakafika hio stage sasa kuambiwa ilikuwa
mbaya hatukupanga kuzaa ni uhongo mtupu ,
Fikilia mtoto wao akija kuwa mkubwa watamwambia kuwa hatukukupanga uje duniani.
Hizo ni mbinu za single mother na single dady wanazitumia ili kuweza kianzisha mahusiano mapya.
 
Yaani wee mama yako mzazi ambaye ni mwanamke amukupa ushairi wee ukajidai unajuwa wanawake kuliko mwanmke mwenyewe. Aisee wee kweli ulilrogwa.

Kwanza mwaka na nusu demu ndio anakuja kusema ukweli hiyo ilikuwa disqualification ya fasta kabisa.

Waheshimu wanawake kama mama zako na dada zako lakini kma mke wachukulis kama chombo cha starehe tuu
 
Copy and paste
 
Uhamuzi......


kwa huu uandishi alikuwa sahihi tu kukupiga matukio
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…