USHUHUDA: Kuku wa kienyeji (Pure) - Biashara kichaa isiyo na tija

Ginner

JF-Expert Member
May 8, 2011
1,513
2,001
Kumekuwa na upotoshaji kwa baadhi wa watu wanaojiita wataalamu wa ujasiriamali, hasa wanaofanya shughuli za ufugaji kwa maandiko ya whatsapp bila kuwa na hata kuku mmoja bandani.

Nimesukumwa kuandika bandiko hili hapa kutokana na jumbe mbali mbali za uufugaji wa kimtandao unaoshawishi vijana kuwa watatajirika mapema kwa shughuli za ufugaji kwa kuanza na kuku wa kienyeji kumi na moja na kuweza kupata Zaidi ya kuku miatatu ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa uzalishaji. Hoja yao inaweza kuwa sahihi, ila ningependa kusisitiza mafanikio katika ufugaji hayapo katika idadi ya kuku unayomiki, bali ni namna ulivyoweza kumanage biashara ya ufugaji.

Hoja yangu leo hapa ni kwamba, Biashara ya kuku wa kienyeji hailipi na nikupoteza muda wako. Na nitatetea hoja yangu kwa mifano hai na uzoefu wangu katika ufugaji.

Biashara ya Mayai. (idadi isiyo na tija kibiashara)

Kwa asili ya kuku wa kienyeji,huwa wanatabia ya utagaji wa mayai 7-10 na mara nyingi ni siku kwa siku 10 mfululizo, utamiaji -siku 21, na uleaji wa vifaranga - siku 50-60. Hii inampelekea kwa kuku mmoja kuweza kutaga wastani wa mayai 35-50 kwa mwaka kwani anapoteza muda mwingi kwa shughuli za utamiaji na malezi ya vifaranga badala ya kutaga. Idadi hii ya mayai haina tija kibiashara kwani kuku mmoja anaweza kukuzalishia tray 1 mpka mbili kasoro pekee kwa mwaka ambayo kwa bei ya soko si Zaidi ya shilingi za kitanzania 20,000 tu kwa mwaka.

Changamoto kwenye soko la mayai ya kienyeji. (Uhifadhi wa mayai)

Mayai ya kienyeji ni kati ya bidhaa ngumu Zaidi kuhifadhika. Ikumbukwe kuwa tofauti na mayai ya kisasa, mayai ya kienyeji huwa yamerutubishwa na majogoo. Hivyo kuharibika ndani ya muda ya week moja au pungufu kama hayatatuzwa katika mazingira salama kwaajili ya utunzaji. Kipindi cha joto kali, mayai haya huanza kujitenenezea kifaranga au mishipa ya damu ambayo baada ya muda mfupi hugeuka viza na kutofaa kwa matumizi tena.

Kwa uzoefu wangu binafsi, nilianza kusambaza mayai ya kienyeji kwenye supermarkets miaka mitatu iliyopita. Nilipata changamoto kubwa sana ya kubadilisha mayai mara kwa mara kwani mteja akichukua yai viza ni kumpoteza kabisa. Hii ni changamoto ya kwanza ambayo mpaka sasa bado inasumbua wafugaji wengi.

Bei juu kwa mayai ya kienyeji

Gharama za mayai husika, bei ya mayai ya kienyeji iko juu ukilinganisha na gharama za mayai ya kuku wa kisasa. Soko kubwa la mayai ni pamoja na vibanda vya chips, migahawa na hoteli. hawa wanauhitaji mkubwa sana wa mayai na soko liko juu muda wote wa mwaka.

Soko la mayai ya kienyeji lipo Zaidi kwenye households(soko la familia) hasa kwa vigezo vya kuzingatia afya zaidi. Soko hili la familia sio kubwa, ni soko dogo na mara nyingi hutumia tray moja kwa kipindi cha wiki mbili au Zaidi. Kwa mzalishaji mkubwa wa mayai ya kienyeji ni lazma awe na soko la familia pana Zaidi kuweza kupata faida ndogo, nasema faida ndogo maana ili kuzalisha mayai tray kumi (mayai 300) kwa siku, utahitaji Zaidi ya matetea 700 mpaka 1000 ya kienyeji pure. idadi ambayo ni kubwa kuliko idadi ya mayai yanayopatikana.

Biashara ya Nyama

Na declare interest, mimi pia ni msambazaji wa nyama ya kuku wa kienyeji, hivyo naongea kwa uzoefu, na niko tayari kukosolewa. Pamoja na kufugwa katika misingi ya kijani (organic rearing), iyo pekee haitoshi kumpa thamani inayostahili huyu kuku sokoni.

Thamani ya kuku sokoni ni uzito alio nao, organic component ni jambo la ziada lililo muhimu pia. tunavyo jadili bei ya soko ya kuku huyu ni lazma tumliganishe na gharama za bidhaa pinzani zilizoko sokoni. Haitawezekana kumuuza kuku mwenye kilo moja au pungufu kwa bei ambayo tunashawishiana humu ya 15,000-20,000 wakati bidhaa pinzani (nyama nyeupe) kama samaki sato toka mwanza wanauzwakwa 7,500 kwa kilo, au kitimoto, nyama ya ngombe ambazo nazo kilo ni 7,500-8,000.

Hivyo basi, hoja yangu hapa ni uzito wa kuku husika. Ukiachana na jamii chache za kuku wa kienyeji (kuchi etc) wenye uzito mzuri, majority ya kuku pure wa asili/kienyeji kwa majogoo huwa na pungufu ya kilo moja na nusu. Kumbuka uzito wa kuku hawa sio kwasababu ya malisho duni, laah hasha, bali ni kutokana na vinasaba (genes) vyao kuwafanya kuwa na maumbo madogo madogo. kwa kuku wa aina hii, sitegemei mfugaji kama atafanikiwa kuwapeleka sokoni na kuweza kupata bei nzuri toka kwa mlaji wa mwisho.

Nini kifanyike?

Ili ufugaji uwe wenye tija kibiashara ufanyike, ni lazma wafugaji tuamke na kuachana na ufugaji wa kuku hawa asilia kwani hawana tija. Nikisema hivi simaanishi watu waache kufuga, hapana, ila wafuge aina /breeds za kuku zenye tija kibiashara. Kuku pekee unaoweza kuwafuga kwa mbinu za kienyeji na bado wakakuletea mfugaji faida nzuri kibiashara, ni kuku aina ya chotara (cross breeds). Hii ni aina ya kuku wenye sifa zote za ukienyeji kwa misingi ya mbinu zao za kuwafuga pamoja na namna walivyo nauwezo wa kuhimili mazingira hasa ya vijijini.

Kuna aina mbalimbali ya kuku hawa ikiwamo Black/ white australorps, kroiller, Rhodes island red, red hamshire, Sussex etc. Hawa ni kuku ambao wanaserve purpose zote za mayai na za nyama. Mfano kuku aina ya black/white australorps wao wanauwezo wa kutaga mpaka mayai 250 kwa mwaka, tofauti na wa kienyeji, mayai ya kuku hawa huwa makubwa na yenye kasha jeupe na kiini cha njano kama utawafuga kwenye mazingira na mbinu asilia (za kienyeji).

Ukilinganisha uwezo wa utagaji wa kuku hawa utagundua utagaji wao ni Zaidi ya asilimia 500% ukilinganisha na ule wa kienyeji pure. Idadi hii ya mayai toka kwa kuku mmoja kwa mwaka, anaweza kumwezesha mfugaji kuzalisha mayai kwa wingi na kushusha Zaidi bei ya mazao yake (mayai) kuwa chini kuweza kuliteka soko kwa urahisi Zaidi. Kumbuka, bei ya juu ya mayai ya kienyeji ni kwaajili ya kulipia gharama kubwa za utunzaji wa kuku huyu ilihali utagaji wake ni hafifu.

Pili, kuku hawa wana nyama nyingi Zaidi kuliko hawa wa kienyeji kwa majogoo hufikia mpaka uzito wa kilo 3-3.5. huku matetea hufikia kilo 2-2.5 na huwa na nyama nzuri, iliyokomaa vyema na yenye ladha. kwa uzito huu kwa majogoo, kuku hawa uuzwa kwa bei ya 20,000 - 25,000 wakiwa hai. bei ambayoni kwa mujibu wa bei ya soko kwa makadirio ya shilingi 8,000 kwa kilo kwa nyama nyeupe.

Mapungufu

Pamoja na ubora wa kuku hawa katika ufugaji wa kibiashara, kuku hawa pia wanachangamoto mbali mbali ikiwemo kutokuwa na uwezo wa kutamia. Pamoja na hii kuwa changamoto pia ni fursa kwani kwa yeye kutotamia kunamwongezea nafasi ya yeye kuendelea kutaga mara nyingi Zaidi bila kupumzika. Hivyo changamoto hii ni faida kwa mfugaji anaelenga kufuga kwa tija. Kwa vile mayai haya huwa yamerutubishwa na majogoo, nirahisi kwa mfugaji kuongeza idadi ya kuku kwa kupitia kutotolesha kwa mshine za kuangulia vifaranga au kumpa kuku mwingine ayatamie kwa niaba.


Neno la kufungia:


“ I think I touched a raw nerve when I said farming is NOT cool! I believe farming takes a lot of HARD work and dedication. Lets not lie to the youth that they'll become instant millionaires when they get into farming. It becomes "cool" once you master the trade......” caleb

Ufugaji unalipa ukiweza kuibudu biashara ya ufugaji,


Kwa ushauri Zaidi kuhusu shughuli za ufugaji, tuwasiliane kwa namba 0755815174. pia pata fursa kusoma ya Makala mbali na utaalamu kutoka kwenye mtandao wetu www.instagram.com/becky_chicks or www.facebook.com/becky_chicks

Nimejaribu kuattach picha za baadhi ya kuku bora wanaofaakufugwa kienyeji na wakaleta tija kibiashara hapa chini. Neno langu si sharia, nakaribisha Michango





 
Safi umenena vyema ila mie ninao matetea wakienyeji niliowanunua mkoani nianzishe mradi mkubwa na mwanzoni walitaga mayai 15 kwa msimu ila nilipofahamu njia yakuchanganya msosi wao walitaga non stop hadi nibadilishe ndo waweze kuatamia ila lazima uhakikishe hawaumwi na kuhusu majoo nilipataga mbegu ya jogoo chotara na niliwafuga kwa miez 9 wafikisha uzito wa kg 2.5 japo sikumaintain chakula....i think with a formular n well care its not wasteful
 
Mkuu inaonekana upo kwenye hii industry kwa muda wa kutosha, je unazungumziaje kuhusu soko la hizo bidhaa?
 
Nakupa hongera kwa somo hili zuri
Naomba unipe ufafanuzi wa wapi ivo vifaranga vya hao kuku (cross breed) vinapo patikana especially kwa Dar na je Bei yake ikoje kwa kifaranga..
 
Kaka unapatikana wapi?? Na je naweza kupata hao kuku kutoka kwako?? Make soon natak nianze kufuga nshaanza kuandaa banda... npo ubungo river side
 
Mkuu kwanza nikupingeze kwa makala yako nzuri.

Ila mimi niko katika kufanya utafiti na hawa kuku wa kienyeji na nimechagua kuku 7Majike na jogoo mmoja. Nimefanikiwa kwa mwezi wa nne sasa kupata mayai 5 kila siku yakishuka ni 4 kuku hupunzika kidogo na kuendelea siwalazishii naweka mayai kwenye mashine.

Tunachotakiwa ni kubuni mbinu za kuwafuka kuku wa kienyeji kwa maslahi na sio kuwaacha.

Pia ninao wengine nafuga ila nitatoa taarifa kamili baada ya utafiti kufika kikomo.
 
Ndugu ungesema umefanya utafiti kwa wafugaji kadhaa na kuona wote hao wanalalamika hailipi hapo makala yako ingepata sapoti.

La na yenyewe itabaki kuwa sawa na zile za wale wanaosema inalipa kwani nao waliweka data jinsi inavyolipa kama wewe ulivyoweka data.

Ila mwisho wa siku unapata unachokitegemea,what you think and believe is what you get.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…