Salaam!!.
Jamani weekend ndio inaisha, hivyo kesho ni siku yakutoana akili na Maboss, kheri yako wewe kama ni Boss mana utapona lakini pia jitahidi usiwatoe wenzio akili.
Leo nilikuwa safarini siku nzima kutokea kusini mwa Tanzania kurudi Jiji la.....!! Dar es salaam na katika safari hii simu Yangu nilikuwa out of charge hivyo nikawa sio mtu wakupitapita mitandaoni haswa mtandao pendwa wa Jamii forums.
Kiukweli kabisa nimekuwa addicted na huu mtandao jamani hata kama huwa sileti thread za Mara kwa Mara lakini nilazima niingie kusoma kilichoandikwa na thinkers wengine.
Saahizi ndio nimepata nafasi yakuingia Jf sasa, basi wakati nasubiri ifunguke nikama Mtu kwenye alosto na sigara yani na ndio ameona mtu anaiwasha hivii.
Kama kuna aina ya vitu vinavyolevya basi naomba na Jf ijumuishwe kwakweli.
Ahsanteni!!.