Tumeona serekali yetu ikitekeleza miradi mipya ya kimikakati mikubwa kama ujenzi wa reli ya kisasa mabasi ya mwendo kasi na bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere hii yote ikiwa ni mipango na mikakati ya kufikisha huduma bora kwa jamii.
Tumeona treni ya SGR imekamilika na kuanza kazi imefurahiwa na wananchi wengi sababu ya ubora uharaka na bei kuwa rafiki.
Wasiwasi wangu ni muendelezo wake je? itadumu katika ubora huu kwa muda gani na je? utakuwa mradi endelevu au utakufa au kupoteza ubora kama ilivyo kwa mradi wa mabasi yaendayo kasi katika jiji la dar es salaam.
Inapaswa taifa liukubali ukweli wa kwamba serekali sio mtoa huduma wala mfanya biashara bora. Kauli hii inathibitishwa na hali halisi iliyopo katika shirika letu la ndege na mradi wetu wa mabasi yaendayo kasi.
Hivyo serekali inaweza kubaki kuwa mtengeneza njia kwa kujenga miundo mbinu kama reli barabara na kuyapa fursa mashirika au kampuni binafsi za ndani au nje ya nchi kuendesha miradi husika na kuendelea kuilinda na kuitunza.
Kwa miradi kama mradi wa mabasi yaendayo kasi serekali inaweza kuyapa makampuni ya usafirishaji ya wazawa na ikaendeshwa vizuri na serekali ikapata gawio zuri kwani tumeona makampuni mengi yenye uzoefu wa zaidi ya miaka ishirini na zaidi katika biashara hiyo.
Katika shirika la ndege serekali inaweza kuacha shirika liwe kama kampuni binafsi na kuipa fursa ya kuuza hisa huku yenyewe ikiwa na hisa zake hii itasaidia pia kukinga shirika na migogoro inayoihusu serekali na watu au mashirika binafsi inayoweza kupelekea ndege zetu kushikiliwa mara kwa mara kama tulivyoona kipindi cha nyuma na kusababisha hasara kwa shirika kwa kufuta safari zake.
Katika uendeshaji wa reli pia serekali inaweza kuwaachia watu binafsi au kampuni kufanya biashara hii na serekali ikaendekea kujenga miundo mbinu huku ikipata gawio lake.
Katika biashara zote hizi serekali inapaswa kuhakikisha wazawa au mashirika na kampuni za kizawa zinapewa kipaumbele ili faida zinazopatikana katika biashara hizi zibaki katika nchi yetu na taifa kuendelea kunufaika.