Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika kupitia FOCAC umekuwa na mwelekeo endelevu

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,094
1,094
1724307967044.png

Katika miaka mingi iliyopita, Afrika ambayo mara nyingi ilionekana kama bara lisilo na tumaini, ilishindwa kabisa kuvutia washirika wake wa jadi ikiwemo Marekani na nchi za Ulaya. Kupitia changamoto hii, China iliibuka na kuishika mkono Afrika ambapo baadaye ikawa mshirika wake mkubwa wa kutegemewa.

Wahenga wanasema “Bora mtu akupe mshipi wa kuvulia kuliko kukupa samaki”. Ili kulikwamua bara hili, China ilifikiria njia nyingi ambapo miongoni mwao ni kuanzisha Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC) mwaka 2000. Ushirikiano huu wa FOCAC uliashiria mwanzo wa enzi mpya. Kuanzia hapo China iliimarisha jukumu lake kama mshirika anayependelewa zaidi na nchi za Afrika, na kuendeleza ushirikiano wake wa kiuchumi na kibiashara na kuwa wa kina kabisa.

Tangu Mkutano wa FOCAC wa mwaka 2021, Ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika umeendelea kuimarika na kufikia kiwango cha juu zaidi ukitoa manufaa yanayoonekana kwa watu wa China na Afrika.

Akielezea maendeleo na mafanikio ambayo yamepatikana chini ya mipango tisa ya ushirikiano iliyotangazwa na China wakati wa Mkutano wa 8 wa Mawaziri wa FOCAC uliofanyika miaka mitatu iliyopita nchini Senegal, Naibu Waziri wa Biashara Tang Wenhong alisema, mipango hii tisa ambayo ni pamoja na matibabu na afya, kupunguza umaskini na maendeleo ya kilimo, kukuza biashara na uwekezaji, uvumbuzi wa kidijitali, maendeleo ya kijani na kujenga uwezo n.k, imeleta maendeleo ya kasi ukiwa na mafanikio ya kushangaza na ushawishi mkubwa.

Tangu mwanzoni mwa karne ya ishirini na moja, kupitia ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara, China na Afrika zimehimiza maendeleo ya pamoja ya kiuchumi na kijamii ya pande zote mbili, na kuunganisha msingi muhimu wa Jumuiya ya China na Afrika yenye Mustakabali wa Pamoja.

Kwa sasa China imesalia kuwa mshirika mkubwa zaidi wa kibiashara wa Afrika kwa miaka 15 mfululizo, ambapo mwaka 2023, biashara kati ya China na Afrika ilifikia dola za kimarekani bilioni 282.1, ikiwa karibu asilimia 11 ikilinganishwa na mwaka 2021, hii inaonesha kwamba biashara kati ya China na Afrika iko imara zaidi.

Mbali na biashara, uwekezaji kati ya China na Afrika nao pia umekua kwa kasi zaidi. Takwimu zinaonesha kuwa hadi mwishoni mwa 2023, uwekezaji wa moja kwa moja wa China barani Afrika ulizidi dola bilioni 40, na kuifanya kuwa moja ya vyanzo vikuu vya uwekezaji wa kigeni barani Afrika.

Katika miaka mitatu iliyopita, makampuni ya China yametoa nafasi nyingi zaidi za ajira zipatazo milioni 1.1 kwa wenyeji wa nchi za Afrika. Wakati huohuo maeneo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara ambayo makampuni ya China yamewekeza na kujenga barani Afrika, katika sekta kama vile kilimo, usindikaji na viwanda, yamevutia makampuni zaidi ya 1,000 na kusaidia kuongeza mapato ya kodi ya Afrika na mapato ya fedha za kigeni kutokana na mauzo ya nje.

Ukiwa mkutano mwingie wa kilele wa FOCAC unafanyika hapa Beijing kuanzia tarehe 4 hadi 6 Septemba, kazi zinazohusiana na misaada ya China na ushirikiano wa maendeleo chini ya mipango tisa iliyopitishwa miaka mitatu iliyopita kwenye mkutano wa Senegal, zimekamilika na matokeo yake yameonekana.

Akitolea mfano naibu mkuu wa Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo ya Kimataifa la China, Liu Junfeng, amesema miradi 25 ya matibabu na afya imetekelezwa, ambayo ni pamoja na makao makuu ya Vituo vya Afrika vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa pamoja na mradi wa hospitali ya Bobo-Dioulasso iliyopo nchini Burkina Faso ambayo yote ilifadhiliwa na China.

FOCAC pia imegusa maisha ya watu wa kawaida hasa wanyonge, kwa kuweka miradi 47 ya kupunguza umaskini na maendeleo ya kilimo ambayo imetekelezwa katika nchi za Afrika kama vile Malawi, Burundi na Cote d'Ivoire. Katika kipindi hicho, China pia ilituma zaidi ya wataalam 500 wa kilimo barani Afrika, na kutoa msaada wa dharura wa chakula wenye thamani ya takriban dola za Kimarekani milioni 100 kwa zaidi ya nchi 30, ikiwa ni pamoja na Djibouti, Gambia na Mali.

Katika mkutano wa kilele wa FOCAC 2024, uliopangwa kufanyika Beijing kuanzia Septemba 4 hadi 6, China na Afrika zitaendelea kuimarisha urafiki wao na kujadili mipango ya ushirikiano, na kutarajiwa kuwa mkutano huu utakuwa njia ya kufungua mlango zaidi kwa Afrika na kuimarisha ushirikiano katika viwanda na minyororo ya usambazaji, ili kuendeleza ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya China na Afrika na uhusiano wa maendeleo ya kunufaishana pamoja.
 
Back
Top Bottom