Ushindani wa soka uliopo nchini uchochee kuinua ubora wa soka Tanzania

Tlaatlaah

JF-Expert Member
May 18, 2023
20,005
22,008
Mathalani,

Ushindani wa jadi baina ya simba na Yanga uchochee kuibua vipaji vya soka na kuinua ubora na viwango vya soka la Tanzania, kitaifa na kimataifa 🐒

Viongozi wa serikali na wasio wa serikali, wahamasishe na kusimamia ushindani huu, uwe mkubwa zaid na uwe wa amani na utulivu ili kusudi kuibua vipaji zaid na kupandisha ubora wa soka letu.

Tujizuia na Tujiepushe na utani wenye sura za vitisho na ishara za kudumaza na kudidimiza ushindani wa soka humu nchini ni vizuri kuchunga ndimi zetu hasa kwa wenye mamlaka.

Ulimi ni moto, unaweza kutenganisha na kuunganisha, kuchonganisha na kusuluhisha, unafurahisha na kuhuzunisha, ulimi unagombanisha na kupatanisha n.k🐒

God bless Simba, God bless Yanga and happy Easter in advance 🐒
 
Hongera sana Mkuu kwa hoja nzuri michango ya maana Kama hii ni nadra sana Hapa jukwaani.

Pamejawa na ujinga mwingi na upumbavu wa kutosha.

Michezo hasa mpira wa Miguu ni Mchakato kidogo.

1. Nadhani wangeanza kwanza kusomesha waalimu wa michezo na Watu wasome Coaching.

2. Selikali ingeboresha michezo ya UMITASHUMITA NA UMISETA.

3. Yangetwengwa maeneo ya michezo au viwanja vya Michezo zaidi ya 20 kila wilaya.

4. Vijengwe viwanda kwajili ya Mipira, koni, Jersey jezi, viatu nk.

5. Kuwepo na Academy za kisasa kabisa za Mpira. Hasa kwa vijana wenye vipaji.

SEMA SISI WATANZANIA WENGI NI VICHAA MAWAZO KAMA HAYA NI MWIKO SELIKALINI.
 
Hii ni wiki muhimu sana katika historia ya mpira wa Tanzania.
  1. Kwa mara ya kwanza, Tanzania imecheza mechi na timu ya Ulaya (mechi dhidi ya Bulgaria kwenye FIFA Series)
  2. Kwa mara ya kwanza, timu mbili tofauti za Tanzania zinacheza mechi za robo fainali ya CAFCL katika msimu mmoja
  3. Kwa mara ya kwanza, kwa top 3 teams za Africa zinacheza katika ardhi ya Tanzania ndani ya wiki moja
 
Hii namba 3 naomba unitajie hizo timu mkuu
 
Back
Top Bottom