Ushauri: Yupi ananifaa kati ya hawa wanawake watatu ukizingatia bado sijatoboa?

Brown Mduma

Senior Member
Sep 29, 2020
180
284
Iko hivi, mimi nina wanawake watatu ambao nilikuwa nadate nao. Katika hao watu watatu mmoja yuko vizuri kiuchum, yaani anajiweza na ni mtu ambae ametokea kwenye familia ya kishua lakini ni mtu ambae ana matumizi ya pesa na anapenda sana vitu vya gharama, hata nyumba anayoishi kodi yake ni kubwa kuliko yangu.

Tatizo linakuja ambapo anataka tuishi pamoja lakini anataka tuhamie kwenye apartment kalii ambayo ni chumba master, sebule, na jiko ndani, ambapo sehemu niliyopo mimi apartment kama hiyo kodi zake zinaanzia 150-200K, hiyo sehemu anasema kodi anayolipa yeye kwa sasa ni 80K.

Anaishi chumba kimoja Master lakini mimi naishi chumba na sebule nalipa 70 sehemu nzuri tu ila choo cha nje, wapangaji wa 3 tuishie hapo.

Tuje kwenye hawa wengine wawili waliobaki ndio wale ambao hawana kila kitu, sema hawana matumizi makubwa ya pesa yaani hata ukiishi nae kila siku ukiacha 3000 kwa meza kila tu kikiwepo ndani, wala hutasikia malalamiko yoyote tena utarudi umepikiwa vizuri pamoja na kufuliwa.

Huyu wakishua ambae anamiliki boda 2 kwa wiki anakula 140K nae anapika pia na kufua anafua na ananipenda tatizo lipo tu kwenye maisha aliyoyazoea, yaan ni mtu ambae hajazoea shida kwenye maisha yake.

Kitu ambacho kinanipa wasiwasi mimi ni kwamba; tangu nimeanza kudate nae matumizi yangu yameongezeka tofauti na nilivyokuwa na wale wangine ambao wananitegemea mimi kwa kila kitu, na sio kwamba yeye hatumii pesa zake kwangu anatumia sana tu hata juzi hapa alinunulia pamba na manukato ambapo vimemkost sio chini ya 100K.

Tuje kwa majirani zangu sasa ambao wanampenda sana mmoja kati ya hawa ambao wananitegemea mimi, yaani hadi wananiambia huyu anakufaa tulia nae. Tatizo ni kwamba huyu wakishua nae kafa kaoza, yaani hata nikimwambia nina shida ya 100K niazime nitakurudisha anafanya kweli lakini binafsi siko deep sana kwake kama yeye alivyo deep kwangu.

Sasa kwenu wazoefu yupi ananifaa hapo ukilinganisha mimi bado ni mpambanaji na bado sijatoboa.
 
You are not mature enough kuoa..
Unajua kabisa humpendi ila unataka awe anakusaidia huku unataka pia kumpangia matumizi...

Oa wa size yako...anaekupa amani...
Kuoa sababu mtu anakusaidia ..siku ukiweza jisaidia mwenyewe utamchukia
Sio Wote wameoa wanawake wanaowapenda shehe Sometimes mtu anaangalia future ya huko mbeleni
 
Oa mwanamke anae ku push beyond your margin sasa mkuu unaogopa manzi sababu anamatumizi makubwa huyo ana ku push akili iweze kuchakata zaidi hao wengine mtaishia kuishi maisha ya ufukara.
 
Oa mmojawapo ya wale 2, wanaendana na kipato chako, lkn ukimuoa wakishua gharama zake ndani ya familia wewe ndie utawajibika kuzitafuta, kama utashindwa utakosa heshima na sauti ya kumkemea au kumkataza jambo ambalo utalipenda maana anakuzidi noti.
 
Mwanamke anaekupenda kwa dhati, anakuheshimu, ana utii kwako na awe na maono ya mbeleni.

Hata wewe ni yupi kati ya hao unampenda na kumjali hata kama hana kitu?
 
Back
Top Bottom