Ushauri wangu maridhawa kwa vijana wenye ndoto ya kufanya kazi za majeshi kupitia JKT

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
10,723
13,662
Kichwa Cha habari kipo wazi sana Kama kinavyojieleza NALIA NGWENA nimeamua kutoa ushauri/ronja kwa vijana wenye ndoto yakufanya kazi za majeshi kupitia JKT/Nini Cha kufanya ukiwa mtaani kipindi unafukuzia nafasi za jkt.

Fanya hivi/chunga hivi /usifanye haya unapokua mtaani na una ndoto za majeshi I'll isilete usumbufu katika usajili.

Mosi, usichore tatoo katika mwili wako, Kuna kasumba vijana wengi wanapata nafasi ya kujiunga na jeshi lakini kwenye usahili anangushwa na tatoo alizozichora mwilini mwake.

Usithubutu kuchora tatoo ya Aina yoyote katika mwili wako.

Pili, usishiriki Mapenzi ya jinsia moja(mtoto wa kiume Linda Malinda Kama Mali) kazi za majeshi mtoto wa kiume lazima ugangamale Sasa ukiwa mtepeto (huna Malinda ) huwezi kufanya kazi za majeshi

Kuna upimaji maalumu utabainika tu Kama hiyo ni michezo yako.

Tatu,Linda damu yako ya mwili isipatwe na maambukizi ya virusi Kama virusi vya ukimwi,
Damu ni silaha kubwa sana kwa kijana mwenye ndoto na kazi za majeshi, jeshi linataka watu fiti tofauti na hapo ni unfit.

Nne, uaijiingize kwenye matumizi ya madawa ya kulevya
Kijana pigania ndoto zako ufike unapopataka achana na madawa ya kulevya ni adui mkubwa wa ndoto.

Tano, fanya mazoezi ya nyumbani/pasha mwili wako ili utakapofika huko mwili usishangae kabisa uendeleze pale ulipo ishia.

Sita, epuka michezo ya ajabu itakayo kusababishia ajali ya kushonwa maana mwili ukishonwa tayari ni unfit ndoto za kujiunga na jeshi zitapotea.

Ya mwisho andaa documents zako Kama vile vyeti vya kuzaliwa kitambulisho Cha nida/namba ya nida mapema weka kabatini ukisikia milio ni kuamka nakutembea faster.

Kijana mpambanaji, I wish you all the best and high spirits of hard fighting.

Jeshi siyo mwili mkubwa Bali jeshi ni kufungua moyo.

NB: NIMETOA USHAURI TU KWA VIJANA USIJE PM KUNIOMBA CONNECTION.



Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Safi sana, ushauri mzuri sana Mashallah.

Kuna mtu humu amekuja kulalamika kwamba Jeshi limemwambia unfit so ana moja kati ya hayo ulioelezea.

Ila mambo yenyewe yote ni mabaya mabaya tu
 
Of course ushauri ni mzuri sana, kwenye ishu ya matizi ni kweli kabisa muhimu sema RTS hata uende vipi kuna vitu havizoeleki japo utakuwa tofauti kabisa na yule asiyekuwa na mazoezi kwa muda. Kikubwa ni kufungua moyo.
 
Sawa, ila sishauri mtu kupoteza muda huko JKT

Labda darasa la 7 na form 4 failure kwakua bado hawana majukumu

Sasa hivi uzuri watu wa degree wanachukuliwa moja kwa moja hawana haja ya kupita JKT, SAFI SANA
Mzee kila hatua Ina changamoto zake, unaweza usiende huko ukidhani kuwa utapoteza muda ukaingia kitaa ukakaa benchi mpaka basi
Kila mtu ana bahati zake.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom