Ushauri wa bure kwa TBWAY 360 wa EATV

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
55,370
77,942
TBWAY.jpg

Umofia Kwenu wana JF,

Imeniladhimu nimuandikie waraka mfupi ndugu yetu Tonny Aka Tbway360 ili watu walio karibu nae au yeye akipitia humu JF aweze kuusoma.Nimeshawahi kukutana na Huyu jamaa mara kadhaa,mara ya kwanza nilimuona maeneo ya Mlimani city akiwa anatoka NSSF kufatilia nadhani mafao yake,nilimuona mtu wa vurugu sana kwenye gari lakini nikaona bado kijana labda bado ana ushamba wa gari.

Mara ya Pili niliona Clip mtandaoni akikimbiza gari kwa speed ya ajabu kisha akakamata Hand-Brake gari ikarotate ikarudi ilipotoka na ilikuwa eneo la wazi kabisa barabarani maeneo ya ununio,nikaona huyu jamaa kumbe ndi0 hulka yake kukimbiza magari kwa speed za hatari >160km/hr tena maeneo ya mjini.

Mara ya tatu tena nilimuona live akiwa quality plaza katoka kwenye ATM kutoa pesa,alitoka na speed kubwa sana hadi nikashangaa inakuwaje anatoka na speed kubwa namna ile wakati mbele tu kama mita 20 kuna foleni? Nikagundua jamaa bado haijui gari vizuri,yes ni dereva lakini haijui gari vizuri,mtu anayeijua gari lazima ataiheshimu.

Kilichonituma niandike huu waraka ni kwamba Jana Tbway360 alikula mzinga wa hatari na gari kubilingika mara mbili,kwa mujibu wa maelezo yake eti anasema alikuwa speed ndogo tu akapushiwa na Suzuki aliyekuwa anaendesha mfanyakazi wa tigo ikamgusa ubavuni na kupelekea gari kubilingika mara mbili.Tbway anatufanya sisi watoto wadogo,gari kwenye speed ndogo uguswe tena na suzuki swift ubilingike mara mbili?

Dogo Tbway360 hiyo umegewa kama funzo,hiyo ni rasharasha tu,punguza sifa barabarani,kwa mtu anayefahamu gari hawezi kufanya ujinga wa kukimbiza gari kwa mispeed ya hovyo hovyo tu,next time hutopata hata muda wa kwenda TIGO HQ kuwatukana SGA....Haya sasa kama ulikuwa na bima kubwa fuatilia michoro ya ajali uende bima kama ulikuwa na 3rd party ugulia maumivu ya Legacy.

Ndinga Baada ya Kula Mzinga.
TBWAYAFTER.jpg

Gari yake kabla ya ajali.
TBWAYABEFORE.jpg

VIDEO CLIP TBWAY360 ALIPOVAMIA TIGO HQ NA KUANZA KUWATUKANA SGA SECURITIES KWA TUHUMA ZA KUMFICHA MFANYAKAZI WA TIGO ALIYEIGONGA GARI YAKE.
 
Attachments

  • TBWAY_TIGO.mp4
    7 MB · Views: 194
Legacy yenyewe ipo riced sana.
Hawa vijana wanao endesha vi artezza na Subaru wana vurugu flani hivi zisizo na maana.
Ile sauti inayotoka kwenye muffler inawazuzua kweli,unakuta gari mlio mkubwa ipo hapo hapo.
Wakija kumiliki gari zenye engine za maana tutawazika mapema.
Badilikeni matozi wote..
Artezza Subaru ni 15M, kiwanja upana futi tatu, urefu futi saba, kina futi sita ni bureeee!
 
Pole yake sana

Ila jamaa simkubali wala nini,ana sifa sana,hata anavyotangaza kipindi chake sifa nyingi na dharau flani hasa akikutana na msanii chipukizi tena wa mkoani hahaha atapigwa madongo na vimaswali vya kejeli mpaka aone moto
 
Legacy yenyewe ipo riced sana.
Hawa vijana wanao endesha vi artezza na Subaru wana vurugu flani hivi zisizo na maana.
Ile sauti inayotoka kwenye muffler inawazuzua kweli,unakuta gari mlio mkubwa ipo hapo hapo.
Wakija kumiliki gari zenye engine za maana tutawazika mapema.
Badilikeni matozi wote..
Artezza Subaru ni 15M, kiwanja upana futi tatu, urefu futi saba, kina futi sita ni bureeee!
Akiona hii hatorudia tena
 
Back
Top Bottom