Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,329
- 118,597
Wanabodi,
Hakuna ubishi kuwa Chama cha Demokrasia na Maendeleo, Chadema kiko kwenye mgogoro mkubwa!. Ushindi wa Zitto kwenye pingamizi, ni nusu shari tuu, shari kamili ni ushindi wake kwenye kesi ya msingi ambao utatengua maamuzi yote ya CC ya Chadema yaliyomvua nyadhifa zake kinyume cha sheria, taratibu na kanuni kwa mujbu wa katiba ya Chadema!, aminini msiamini, Chadema itaaibika, itafedheheshwa, itafedheheka na itatahayari! huku ikiendelea kupoteza credibility yake ambayo tayari imeishaanza kupotea!, hivyo naishauri Chadema, yote yaliyotokea mpaka hapa, hiyo ni nusu shari tuu, ni a "Heri Nusu Shari, kuliko Shari Kamili!", wenye busara wa Chadema kama mpo, nawashauri muepushe shari kamili!.
Kunapotokea mgogoro unaotokana na makosa ya wazi ya kiutendaji kutaka kukomoana kwa kutunishiana misuli, kwa kawaida kuna mwashishaji na mmaliziaji yaani "Anza wewe, mimi namaliza!", ipo namna kwa Chadema kujiponya na dhahama hii ilioianzisha, kabla mmaliziaji hajaimaliza!, dawa ni kujishusha tuu kwa kukubali yaishe bila kutafuta mshindi na mshindwa, wakaitana, mkosaji akaomba msamaha, mkosewaji akaifuta kesi, na kukubali ama kuendelea kama zamani, au kuachsana kwa usalama na sio kufukuzana, kutimuana na kutunishiana misuli!.
Wana Chadema wengi kwanza hata hawaelewi katiba yao inasema nini!, sikuile nimeuliza humu kuhusu kile kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya katiba ya Chadema kiliondokaje, Katibu Mkuu Mzima wa Chadema alikuja humu, akatamka wazi kuwa kipengele hicho hakikuwahi kuwepo!, ndipo JJ. Mnyika akaokoa jahazi kwa kueleza kilicho tokea!. Hivyo watu humu wanapiga kelele nyingi, huku hawaelewe maudhui ya kesi ya msingi, Zitto ameomba muhtasari wa kikao kilichomvua uongozi ili aweze kukata rufaa!, kikao hicho kilichomvua uongozi kilifanya madudu ya ajabu!, halafu watu wanakuja humu kusifia ujinga!, Chadema hapo ilipo, ni kama mtu anaoga mtoni, kisha mwendawazi kaja na kukimbia na nguo zako!, mwenye busara, atachutama tuu na kuendelea kujisetiri mpaka msaada uje, lakini inachofanya sasa Chadema, ni kutoka ndani ya maji hivyo hivyo kama ilivyozaliwa, na kuanza kumkimbiza mwendawazimu anayekimbia na nguo zake!.
Kwenye baadhi ya migogoro, kuna mkosaji na mkosewaji. Kwenye hili la Zitto, Chadema ndie mkosaji, ndie aliyelianzisha, anachofanya Zitto ni kumalizia tuu!. Dawa ya tatizo kwanza ni kulitambua kosa ni lipi, ukiisha litambua kosa, unakubali makosa, unajishusha na kujinyenyekeza, unatubu kosa, unaomba msamaha, mnasameheana, mnashikana mikono, mnakumbatiana, mnayasahau yaliyopita sii ndwele, mnaganga yajayo ikiwemo Zitto kufuta kesi!.
Mimi Pasco wa JF, siku zote nimekuwa nikilia na matatizo ya Chadema kufanya maamuzi ya papara, kibabe, jazba ambayo ni kinyume cha katiba yake kwa kuwaadhibu wanachama wake kwa kuwafutia uanachama!. walianza na Kafulila, hadi akaitwa sisimizi!, mimi nililalamika humu!. Sakata la Kafulila na wenzake CHADEMA -
Chadema walipojidai hawamtambui JK na kuisusia ile hotuba yake, niliwalalamikia humu kuwa ile ilikuwa ni zuga tuu!. Zitto alisimama kwenye ukweli na sio kujiunga na hiyo zuga! na hapa ndipo dhana ya usaliti ilipoanza kukolezwaChadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.
Kama kwenye Chadema bado kuna wenye busara wachache, nawashauri watafute legal ipinion kwa wanasheria nguli zaidi ya hao inaowategemea, wawaambia position yao kwenye shauri la msingi!, dawa ni kumuangukia tuu Zitto, kumuomba msamaha kwa yote, kumuomba afute kesi, na amini nawaambieni Zitto, baadada ya kuujua ukweli wa mambo kuhusu Chadema, atajiondokea zake, kistaarabu na kwa heshima!.
Alipojiunga kuna mambo hakuyajua kuhusu Chadema!, kuna baadhi ya viongozi wake alidhania ni watu wenzake!, kumbe "machoni tuu ni kama watu!. Alipojiunga alidhania Chadema ni chama cha wote!, kumbe Chadema ni chma cha watu, kina wenyewe!, hivyo kesi ataifuta, atawaachia wenyewe chama chao na ama aamue kuendelea na siasa ila kama anajipenda maisha yake!, aachane kabisa na siasa! wenye uelewa wataelewa ni kwa nini!.
Moja ya makosa makubwa kabisa ya Chadema, ni not doing the right thing at the right time and doing it right!. Niliwaeleza hapa!, Kwenye hili sakata la Zitto, Chadema did the wrong thing!, at the wrong time, and did it wrongly!.But it still has the chance to do the right thing kurekebisha makosa, tena at the right time, before its too late, and it got to do it right!.Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
Naongea kama nani au nashauri kama nani?!. Mimi sio mwanachama wa chama chochote, ila ni mlipa kodi wa JMT. Chadema is a public party paid by taxpayers money, hivyo Chadema kinaendeshwa kwa kodi yangu!. The public has the right to know its public and private conduct, and when it does wrong!, ni haki yangu kukiambia, kukikosoa na kukishauri.
Why kila siku Chadema tuu, kwani vyama vingine havipo?!. Jibu ni "mti wenye matunda!".
Mpira uko uwanjani, its up to Chadema kuamua kusuka au kunyoa!.
The choice is yours!.
Pasco.

Walipowatimua wale madiwani wa Arusha, mimi nililalamika humu ....Uamuzi wa CHADEMA dhidi ya madiwani: "A Big Mistake!"Kama ni kufukuzani, fine, lakini kutumia taratibu, sheria na kanuni walizo jipangia , sababu zisiwe chuki binafsi, makundi, au kutofautiana kambi,hali ilivyo CCM kwa sasa ingetakiwa iwe ndio oportunity kwa Chadema ku-seize, lakini nanyi ndio mnaanza...
Walipowatimua kina Shonza na genge lake, nililalamika sana humu kuhusu ukiukwaji wa katiba sgeria na kanuni kwa kuendesha kangaroo court na nilililalamika humu...Wito: CHADEMA Watendeeni Haki Wanachama Wenu Ili ...Kitendo cha Kamati Kuu ya Chadema kuwavua uanachama madiwani wake wa Arusha, is "A Big Mistake"!, and there is a price to pay, so Chadema must pay the price which is very high!.
1. Ile sheria ya kulazimisha wawakilishi wa wananchi, lazima wadhaminiwe na vyama, its a bad law, na inakwenda kinyume cha Katiba ya JMT inayotoa uhuru kwa kila raia kushiriki katika uongozi wa serikali tangu ya mitaa hadi serikali kuu, hadi mahakama kuu ilishatoa rulling hicho kipengele kuwa ni 'unconstitutional' na kiwe struck out from the books of law!. Naamini Chadema hilo wanalifahamu, hivyo kitendo cha kutumia kipengele hicho hicho ambacho ni bad law, to its advantage, is "A Big Mistake!".
2. Ukishachaguliwa, Diwani au Mbunge, hata kama ulidhaminiwa na chama, wewe, unakuwa umechaguliwa na wananchi, na unakuwa ni mtumishi wa watu na kule kwenye ngazi za maamuzi, Baraza la Madiwani na Bungeni, unawakilisha maslahi ya wananchi waliokutuma, na sio maslahi ya chama kilichokudhamini, japo katika uwakilishi wako, pia maslahi ya chama yatazingatiwa. Kitendo cha chama kuwafukuza wawakilishi halali wa wananchi kwa maslahi ya chama, is "A Big Mistake!".
3. Sisi ambao hatuna vyama, lakini tuna shauku ya kuona Tanzania inaongozwa na chama mbadala, tumekuwa na imani kubwa sana na Chadema kama ndicho chama pekee mbadala ambacho kimethibitisha kikiaminiwa, kinaweza kuleta mabadiliko ya kweli. Hivyo tunategemea Chadema kitafanya maamuzi yanayofuata misingi ya haki. Kitendo cha kuwavua uanachama madiwani wake hawa, waliochaguliwa na wananchi, (sio chama) bila kuwasikiliza, ni kuwa "condem Unheard", which is against principles of Natural Justice, and this is a "A Big Mistake!".
Tangu jana baada ya uamuzi wa BAVICHA kuwavua uanachama wake baadhi ya wanachama wake hivyo kuwafanya wanachama hao kupoteza uanachama wao wa CHADEMA, naomba kutoa wito kwa Uongozi wa CHADEMA, kuwatendea haki wanachama wake, ili kujenga imani kuwa CHADEMA itawatendea haki Watanzania come 2015 just in case!.
Ushauri huu lengo lake ni kutuaminisha sisi Watanzania wengine tusio wanachama wa CHADEMA, kuwa Chadema ni chama cha haki na kinafanya maamuzi yake kwa kufuata misingi ya haki hivyo kutupa matumaini kuwa CHADEMA inaweza kuaminika na kukabidhiwa nchi mwaka 2015!, vinginevyo kwa mambo haya kama yalivyo sasa, na kama CHADEMA haitabadilika, then kwa 2015 CHADEMA itakuwa bado haijakomaa kiasi cha kutosha kuaminika na kukabidhiwa nchi!.
Chadema walipojidai hawamtambui JK na kuisusia ile hotuba yake, niliwalalamikia humu kuwa ile ilikuwa ni zuga tuu!. Zitto alisimama kwenye ukweli na sio kujiunga na hiyo zuga! na hapa ndipo dhana ya usaliti ilipoanza kukolezwaChadema Yakubali Yaishe! Yamtambua Rais!, Yampongeza Rais!.
Na sio mara ya kwanza kwa Chadema kufanya makosa ya kimsingi kabisa ya kisheria, taratibu na kanuni!, Waliposusia mchakato wa katiba na kutoka nje, niliwaeleza humu kuwa Lissu amewapoteza!, hakuupinga muswada ule kwa mujibu wa kanuni, bali yeye ndie alitoa go ahead ukapita kisha wakajifanya kususa, nililisemea sana hili hapa!.Katiba: CHADEMA mlikosea! Kubalini yaishe, Tusonge mbele!Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe amekubali yaishe, wanamtambua JK kama Rais, Wanampongeza! Mbowe ameomba reconciliation for the sake of Umoja wa Kitaifa.
Mbowe amewashukuru wapiga kura kwa kura walizoipigia Chadema!.
Hiki Mbowe alichokifanya Bungeni, ndicho Dr. Slaa alichotakiwa kukifanya ile siku ya kutangazwa matokeo!
Nilisema that was a golden missed opportunity. Sasa Mbowe amerekebisha makosa ya Dr. Slaa. Chadema sasa inarudi juu!
Chadema sasa tusonge mbele, hata mimi nikirudi uraiani, naweza kufikiria kujiunga Chadema, kuimarisha nguvu!
Asante sana Mhe. Freeman Mbowe!.
Kanuni ya Kuu ya Kwanza kwa mwanahabari yoyote ni to tell nothing but the truth. Naomba kuitumia kanuni hii kuwaambia Chadema, they were wrong!, walikosea!, kwanza wakiri makosa, pili wakubali yaishe na mwisho wasonge mbele, 2015 sio mbali kihivyo!.
Sasa na hili la Zitto, kufuatia Chadema kuzoea vile vya kunyonga kwa kangaruu court zake, kwa Zitto, wamekutana na vya kuchinja!. Wao walidhani Zitto ni jina tuu, wakijiaminisha sio mzito!, wala hana uzito wowote, wakatunisha msuli wakidhani ni chepesi, kumbe kiukweli, Zitto ni Zitto kweli, sio jina tuu, bali ni Mzitto haswa!, sio mtu wa kukisukumizia kule kama kila ki "sisimizi!", hapa sasa Chadema imekutana na kisiki!, tena kisiki chenyewe cha mpingo!, kutoka kulee mwisho wa reli!. Kilichoshafanyika ni kwa Chadema kujikwaa tuu katika kisiki hiki, na kujikwaa sio kuanguka!, busara ni kwa Chadema kuangalia imejikwaa wapi, ili mbele ya safari isije kujikwaa tena, na hatimaye hata ikaja kuanguka!.Mchelea mwana kulia, hulia yeye, japo binafsi sio mshabiki wa chama chochote cha siasa bali ni mkereketwa wa demokrasia ya kweli ndani ya bunge, hivyo wapenzi wote wa dhati wa demokrasia, lazima waikubali Chadema kama ndicho chama pekee cha upinzani Tanzania bara kilichoonyesha nuru ya matumaini ya uwezekano wa kupatikana kwa demokrasia ya kweli ndani ya bunge na labda hata ukombozi wa pili wa Mtanzania baada ya uhuru na miaka 50 ya utumwa wa chama kimoja CCM kuhodhi madaraka yote ya dola.
Wengi wa wapenzi wa demokrasia wanaishabikia mno Chadema wakichelea kuiambia ukweli kuwa watalia, mimi nachelea mashabiki na wapenzi wao kulia mwaka 2015, hivyo nawaambia ukweli ili hata kama mtalia, lakini itakumbukwa mliambiwa!.
Yaliyopita si ndwele, tugange yaliyopo (Tume ya kukusanya maoni) na yajayo (Katiba Mpya).
Namalizia kwa kusisitiza, kufanya kosa si kosa, kosa ni kurudia kosa!. Chadema kwenye uundwaji tume mmefanya kosa!. Sheria imetungwa na sasa sio kosa tena, kosa ni kurudia kosa kama hamtoa maoni yenu kwenye tume!. Two wrongs don't make right, better late than never!.
2015 sio mbali kihivyo!.
Kama kwenye Chadema bado kuna wenye busara wachache, nawashauri watafute legal ipinion kwa wanasheria nguli zaidi ya hao inaowategemea, wawaambia position yao kwenye shauri la msingi!, dawa ni kumuangukia tuu Zitto, kumuomba msamaha kwa yote, kumuomba afute kesi, na amini nawaambieni Zitto, baadada ya kuujua ukweli wa mambo kuhusu Chadema, atajiondokea zake, kistaarabu na kwa heshima!.
Alipojiunga kuna mambo hakuyajua kuhusu Chadema!, kuna baadhi ya viongozi wake alidhania ni watu wenzake!, kumbe "machoni tuu ni kama watu!. Alipojiunga alidhania Chadema ni chama cha wote!, kumbe Chadema ni chma cha watu, kina wenyewe!, hivyo kesi ataifuta, atawaachia wenyewe chama chao na ama aamue kuendelea na siasa ila kama anajipenda maisha yake!, aachane kabisa na siasa! wenye uelewa wataelewa ni kwa nini!.
Moja ya makosa makubwa kabisa ya Chadema, ni not doing the right thing at the right time and doing it right!. Niliwaeleza hapa!, Kwenye hili sakata la Zitto, Chadema did the wrong thing!, at the wrong time, and did it wrongly!.But it still has the chance to do the right thing kurekebisha makosa, tena at the right time, before its too late, and it got to do it right!.Kuelekea 2015: Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!
Wanabodi, Preamble: "Kwa opinion yangu, Uchaguzi wa 2015, Chadema Kuchukua Nchi Kwa Kishindo!... Only If...!"!Trend za Upepo wa Kisiasa kuelekea 2015, zinavuma kwa Kasi ya Ajabu kuelekea Direction ya Mabadiliko (The Wind of Change, is Sweeping Across Tanzania) na kila dalili inaonyesha na kuelekeza Chadema is gaining momentum and there is nothing to stop it kuchukua nchi mwaka 2015 iwapo...
Chadema is doing the right thing!. Doing the right thing alone, doesn't guarantee sweet clear victory for Chadema, it got to do things right!. Hii inamaanisha ili Chadema ishinde kwa kishindo kinachotakiwa, lazima ikubali kubadilika and start doing things right besides doing the right thing!.
- Hivyo ndugu zangu viongozi wa Chadema najua 2015 mmedhamiria kwa dhati kuchukua nchi kwa ushindi wa kishindo!, lakini ili lengo hili litimie, ni lazima kwanza mkubali kusikiliza, pili mkubali kuzifanyia kazi hizi hoja na tatu mkubali kubadilika!.
- Imethibitika pasi shaka kuwa uchaguzi wa 2015, Ikulu ni ya Chadema, hivyo sasa kuelekea 2015, kila dalili zinaelekeza Chadema kuchukua nchi, ila kwa maoni ya wengi serious waliochangia thread hii (ukiondoa wale wa ushabiki), wengi wamekubali Chadema iko on the right track, ila ili kutimiza lengo hilo la kubisha hodi ikulu, na kukubaliwa kuwa mpangaji rasmi wa jengo lile, lazima Chadema ikubali kubadilika, apart from doing the right thing kama inavyofanya sasa, it got to do things right!.