Kwa heshima na taadhima naomba ushauri kwenu wadau.Mimi ni mwananchi katika nchi moja ya SADEC.Kwa hali ilivyo hivi sasa nchini kwangu,mwananchi yoyote anayeweza kusema siasa za taifa lake hazimhusu,huyo hajielewi kabisa.
Hapa nchini kwetu,Siasa ndizo zinazotupangia karibia kila kitu kuanzia hata kiwango cha MB za intaneti tunazozitumia hapa jamii forum.Kwa wafanyakazi, kikokotoo na kodi kwa wafanyabiashara vyote hupangwa na wanasiasa.
Kwa muda mrefu mimi nimekuwa mwanachama wa chama kilichopo madarakani kutokana na sera bora hasa za ujamaa na kujitegemea na nadharia kuwa rushwa ni adui wa haki.
Lakini nikifuatilia kwa makini sasa hivi,nahisi kabisa misingi tuliyoachiwa na waasisi wetu imeanza kutelekezwa kutokana na siasa za uchawa na vyeo vya ujanja ujanja.
Watu wanaohoji na kuuliza maswali magumu kuhusu mustakabali wa nchi yetu wanaonekana wapinzani au wanaotumika.Baadhi ya Machawa na wenye IQ ndogo wanaonekana ndiyo mashujaa wanaokabidhiwa majukumu nyeti ya kuwasemea vyema wafanya uamuzi na wenye kuamua hatma ya taifa letu.
Niliwahi kufikiria kuwa mwanaharakati wa kutetea haki lakin naogopa kutokana na tetesi za kupotea kwa baadhi ya vijana wenzangu niliokuwa naona harakati zao za kusema maovu yanayoendelea.Kama ni kweli,nimevunjika moyo kweli kweli.Wengine ni wazee, huku katika nchi mwanachama wa SADC inasemekana(sina uhakika) wanasota korokoroni sababu tu walionekana wajuaji na wanaongea sana.
Asikwambie mtu hakuna anayependa kufa mapema bila kutimiza purpose au jukumu la kuletwa kwake duniani.
Mbaya kabisa unaweza kujitoa mhanga kuzungumza sana kuhusu mabaya yanayoendelea,ukapotezwa na wananchi wakakusahau baada ya siku mbili.Nikifikiria pia kujiunga na chama kikuu cha upinzani katika hii nchi,sioni kabisa dhamira njema ya baadhi ya viongozi wao kutokana hata na rafu wanazozifanya katika uchaguzi wao wa mwaka huu.Imagine tuhuma kibao za rushwa katika uchaguzi wao.Tuhuma tu zilitosha kabisa kumlazimu Kaisari amuache mke wake aliyekuwa anatuhumiwa kuchepuka.Japo ushahidi ulionyesha hakuwa na hatia.Wanaotuhumiwa wote kulamba asali,walitakiwa kujitafakari moral authority zao.Lakin ndo kabisa bado wanatupigia kelele tu.
Je nijiunge na chama kipi sasa ndugu zangu?Nijiunge na chama chenye sera ya ubwabwa?Au nijiunge na vyama vingine vinavyosemekana ni mapandikizi ya kukisaidia chama tawala ili kitawale milele?Au nibakie chama tawala?Lakini hiki chama tawala nacho kisipopata upinzani na changamoto bungeni,watawala si ndiyo watajisahau na kujiona Miungu watu sababu hakuna mtu wa kuwa challenge?Niendelee kubaki chama tawala ili maumivu yabaki ndani kwa ndani kwa yanaoendelea?
Au niisaliti dhamira yangu njema ya kuwa mzalendo kwa taifa langu na kuungana na machawa wanaosifia sifia tu kila kitu wakitegemea uteuzi na vyeo?
Au niendelee kubishana tu vijiweni kuhusu timu za MWAKALOBO ambazo nazo hata mpira hazijui na zinategemea zaidi uchawi?Au na mimi nijiunge na wachawi?Lakin naogopa sababu juzi nimeambiwa wachawi wote wameshakufa.
Nani sasa atabakia mzalendo wa kutetea nchi ikiwa vijana wote tumekuwa wa hovyo tunaoshabikia connection,shisha,uchawa na trend za BARTZAR wa nchi yetu jirani ya Equitorial?Au nihamie Burundi ndugu zangu?Au nihamie kwa Mi SHANGAZI?
Nipo njia panda na pengine ushauri wenu unaweza kunisaidia Ili nibakie mzalendo kwa taifa langu