David Harvey
JF-Expert Member
- Jul 17, 2014
- 2,827
- 5,786
Wasaalam?
Ipo hivi juzi asubuhi Jumapili niliingia nyumbani nilikuwa SA kwa mambo ya kikazi, kufika nyumbani nilimkuta binti yangu wa kwanza pamoja na dada wa kazi kumuuliza mama yako yuko wapi? Akasema ameenda kanisani, nikamuuliza mbona hajaenda na watoto(watoto ni mapacha wana miezi 4) wakashindwa kunipa jibu nikapiga kimya nikaenda kupumzika kutokana na uchovu.
Imefika saa 7 mchana nikashtushwa na kelele za watoto walikuwa wanalia mno nahisi walikuwa wanataka kunyonya kuangalia makopo ya maziwa yameisha nikatoa pesa wakaenda kununua lakini nilipiga marufuku matumizi ya maziwa ya kopo.
Nimebuy time mpaka saa 10 jioni kimya mtu hajarudi nikipiga simu inaita tu haipokelewi, nikashikwa na gadhabu sana nikachukua watoto nikawatupia kwenye gari safari mpaka kanisani kwa wife.
Nimefika kanisani nimemkuta wife yupo madhabauni anaombea watu nikachukua watoto nikawaweka pale pale madhabauni nikamwambia awanyonyeshe watoto wana njaa, akagoma akasema nimemfanyia vitendo vya aibu!!
Ghafla mchungaji mkuu akaja akauliza kuna nini? Mimi nikamwambia mchungaji hayakuhusu nataka watoto wanyonye niondoke nao nyie endeleeni na ibada zenu,mchungaji akadakia akasema ibada ya leo inahitaji utulivu ndio maana tulitangaza watoto wote wabaki majumbani.
Nikamvuta kinguvu wife nikaondoka nae nikamwambia Leo ndio mwanzo na mwisho kusali katika makanisa ya kiroho kama hauwezi kusali roman Catholic pumzika nyumbani tu.
Nimepigiwa simu sasa hivi natakiwa kituo cha polisi kwa kosa la kufanya fujo kanisani na kufanya shambulio la kimwili dhidi ya wife, niende au nisiende? Kwa sababu kesho asubuhi inabidi niende Bujumbura kikazi.
Asante
MREJESHO: no 1
Nimeripoti police nimewekwa selo kwa dakika 30 mama mkwe amekuja ameniwekea dhamana nimetoka.
Cha ajabu muda huu nimerudi nyumbani nimemkuta dada wa kazi tu.. kuuliza naambiwa ameenda kanisani yeye na watoto wote .
Kusikia kwa kenge mpaka damu zimtoke ngoja niende kwanza Bujumbura.
Asante
MREJESHO no 2
Leo tar 5 nimerudi kutoka Burundi muda huu nimeingia nyumbani nimewakuta na waumini wenzake wanafanya fellowship,sitaki kuanzisha vurugu nasubiri kesho nirudi polisi kwanza kuripoti.
Asante.
MREJESHO no 3
Polisi wamesema tuyamalize kifamilia.
Tumekaa kikao cha familia binafsi nimempiga marufuku kwenda tena katika ilo kanisa na hakuna kufanya tena fellowship nyumbani kwangu ni kheri arudi Roman Catholic, kama hataka basi afanye ulokole wake ndani yangu akiwa na watoto wake lakini sio kwenda tena katika makanisa ya kiroho.
Pia wazazi wake wamempiga marufuku kwenda ktk makanisa ya kiroho.
NB:Tumegundua kanisa halijasajiliwa mimi na rafiki yangu tunalivalia njuga ilo kanisa mpaka lifungwe kwa gharama yoyote.
Mwisho