Florian musumi
Member
- Sep 14, 2011
- 8
- 45
USHAURI KWA VYAMA VYA UPINZANI KUELEKEA 2020 NAFASI YA UBUNGE NA URAIS!!
Road To 2020.
Florian Musumi.
Mwanza.
1. Mgombea Urais.
Kwa hali inavyoendelea Sasa Karata pekee kwa vyama vya upinzani ni Tundu Antipas lissu, wanaharakati na wanachama wa vyama vya upinzani Walio wengi wamekuwa wakimtaja sana katika kinyang'anyiro hicho.
Ushauri wangu kwa viongozi Wa Vyama hivi Vya upinzani, ni Kweli lissu ni Jibu sahihi kwa Nafasi ya urais 2020 Ila sio wakati sahihi, Kwa Nafasi ya urais 2020 Lissu hawezi kushinda kwa sababu Mbalimbali
1.Moja wapo ni Kukubalika Kwa Rais Magufuli hasa wananchi wanyonge kabisa.kwa Maendeleo aliyoyafanya Hasa katika kuwekeza Katika kundi hilo Ambalo linawapiga kura wengi Na watanzania Wengi kuliko wengine.
2. Kumbuka Rais Magufuli Anaingia kwenye uchaguzi huo Bado akiwa Amri jeshi Mkuu, Hivyo kwa lugha rahisi hakuna Ambae atakubali kuachia Madaraka wakati anauwezo wa kushinda, Anauwezo wa kufanya kampeni Muda wowote wakati wowote na Atakuwa amejiandaa vya kutosha.kuna Ambao wanaenda Mbali zaidi wanafananisha Mfumo wa serikali Wa Tanzania na Nchi zingine Ambazo wapinzani walimshinda Rais aliyekuwepo Madarakani. Kumbuka Mfumo wa serikali kulingana Na Katiba Yetu ni Tofauti na Nchi hizo. (System ya Tanzania Ni tofaut na Nchi zingine)
3. Umoja wa CCM kwa sasa umeimarika kuliko mwaka 2015 Kulingana Na viongozi wa Chama walipo kwasasa Katibu Mkuu Dr bashiru ally, Mh polepole Chini ya Mwenyekiti Imara Mh. John Pombe Magufuli Na umeongeza wanachama wengi na wadau wengi Kutoka upinzani.Hivyo hii inasababisha Kampeni za Ccm kuwa nyepesi zaidi upande wa Urais 2020.Pamoja na hilo Mh Rais Amekuwa akiwatumia wapinzani wake wa 2015 katika shughuli Na Nasafi Mbalimbali Hii imedhoofisha upinzani kwa asilimia kubwa.
Kwasababu Hizo ili kuweza kuwa na Tundu lissu katika Bunge la 2020-2025, Mshauri Tundu lissu agombee ubunge na Sio urais.
Nini kitatokea Lissu akigombea urais?
Ni kweli kwa kampeni za 2020 zitaweza kufanana kidogo na Kampeni za mwaka 2010, Ambazo Dr Slaa aliweza kutafuta Urais kutoka kwa Dr kikwete.Jambo ambalo lilishindikana Na kwa hali ya kawaida kama 2010 Likishindikana chini ya Rais Jakaya kikwete, Kwa 2020 Ni ngumu sana Chini ya Uongozi wa Jemedari John pombe Magufuli.
Lissu Baada ya kushindwa Uchaguzi 2020 atakuwa Amekosa Sifa ya kuingia Bungeni! Atabaki na Ndoto hizo hizo za Kuusaka urais 2025, lakini Kwa historia ya Upinzani Lissu hataweza tena kupewa Nafasi ya mara ya pili 2025, kumbuka Mbowe -2005, SLAA-2010, LOWASSA-2015. kwasababu hii Safari ya Tundu lissu Kuachana na Siasa Kama ilivyokuwa Dr slaa itakuwa Imeivaa.
2. Upande Wa ubunge.
Kwa uchaguzi ujao wa Mwaka 2020, Vyama vya upinzani vinatakiwa kuwekeza kwa Wabunge wapya Kabisa Ambao Ndio itakuwa Safari yao ya Kwanza Kwenda Bungeni.
Ila Wapinzani Wakiamua kuwekeza Tena kwenye Majimbo yafuatayo Inaweza kumaliza Uchaguzi Imekosa Majimbo Yote hata yale Ambayo hayakuwa TARGET YA CCM.
1. Mbeya mjini
2. Arusha Mjini.
3. Majimbo yote Ya Dar.
4. Jimbo la Tarime Vijijini.
5. Bunda Mjini.
6. Iringa Mjini.
(Walejee CCM Kama wanahitaji kuwa wabunge 2020-2025)
Upinzani Kwa Vyovyote vile Chama Tawala Tayari Kinauwezo wa Kushinda Majimbo hayo bila Wasiwasi,
Lakini upinzani Pia watahitaji kushinda Majimbo hayo kwa lazima Kwasababu Wabunge wa Majimbo hayo Ni viongozi waandamizi wa Chama na Ni Icon Ya upinzani Kwa sasa.
Kitakachotokea Upinzani Wakilazimisha kushinda Majimbo hayo itajikuta imepoteza Majimbo Mengi Ambayo ilikuwa na Uwezo wa Kushinda ambayo sio Target Yao.
Kwanini Sijamtaja Mbowe,Zitto,Mbatia? Hawa ukumbuke Ni viongozi wa Vyama vya Upinzani NChini hivyo kwa Huruma na Mfumo wa vyama Vingi Bado wanaweza kuwa na Nafasi ya kuendelea Kuwa wabunge 2020, Ila wafuasi wao ambao Ndio Mwiba zaidi Hawataweza kuungana na Viongozi wao Bungeni 2020.
Mwisho.
Kwasasa Upinzani Unahitaji kuibua wabunge Wapya vijana tofauti na waliozoeleka, Ambao watakuja na Hoja Mpya tofauti.
2020 Wapinzani wekeni Nguvu kwenye Ubunge na udiwani Ila kwenye Urais Mtapoteza Muda na Fedha nyingi wakati asilimia za kushinda 0.
NB. Chama cha mapinduzi kwa uchaguzi wa 2020, wanauwezo na Uhakika wa kushinda Viti vyote vya ubunge Kulingana na Maendeleo na Hatua alizofanya Mh Rais na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi.
Mh. John Pombe Magufuli.
Road To 2020.
Florian Musumi