Kuna tatizo sugu la ardhi limekuwa likiendelea nchi kwa miaka mingi. Halmashauri nyingi hazitaki kupima mashamba vijijini kwa makusudi mpaka wanapopata mradi. Mradi ukitokea wenye mashamba wanapewa fidia kidogo, mashamba yakishapimwa wanamilikishwa wafanyakazi wa ardhi halafu wanayauza kwa faida kubwa. Ukikisia kuna mradi wowote wa kupima viwanja vilivyokuwa mali ya vijiji ujue nusu ya viwanja hivyo watapewa watu wa ardhi. Ni lazima tuhakikishe kuwa watu wa vijijini pia wanapewa hati kuu siyo kupewa hati za kimila halafu baada ya muda wanapoteza haki zao za kumiliki ardhi hasa wale wenye ardhi kubwa.