Ushauri kwa wahitimu wa vyuo vikuu

pwilo

JF-Expert Member
May 27, 2015
10,812
13,737
Habari za weekend wadau,

Leo naomba nitoe ushauri kwa wahitimu wa vyuo mbali mbali ambao wamemaliza na wanaotarajia kumaliza astashahada, stashahada, na shahada kuhusiana na mfumo wa ajira portal.

1.Kama umemaliza bachelor na ulikuwa umeanza kusoma certificate na diploma na ukahitimu ukapewa vyeti basi usiweke cheti chako cha bachelor kwenye mfumo, maana ni ngumu kuondoa taarifa ukishaweka.

2.Ni rahisi kupata kazi kwa sasa kwa wenye certificate na diploma kuliko bachelor degree utakuja kujuta.

3.Ukifanikiwa kuajiriwa basi unaweza kuwasilisha cheti chako cha bachelor baada ya kuthibitishwa wengi wamefanya hvyo.

4.Wengi wanateseka na ku upgrade taarifa kule ajira portal kwasababu wameweka taarifa za bachelor hivyo ni ngumu kuzitoa ikitokea nafasi za chini yake.

5.Usichague sehemu au mkoa wa kufanya kazi kwasababu ukipata kazi unaweza kuhama lakini pia vijana mtambue zama zimebadilika sana mjaribu kuangalia alternative.

Alamsik.
 
Pamoja sana mkuu
 
Kwahyo mkuu, hizi taarifa ninazosikia kuwa kama mtu umeajiriwa na diploma inatakiwa ukae kazini miaka mitatu then u-upgrade cheti ya degree ni kweli...?
 
Sio kweli mkuu mwaka baada ya kuthibitishwa unapanda.
 
Kuna watu watumia certificate mpaka leo japo wana masters na wamesomeshwa na shirika.
kuthibitishwa na utumishi sio leo.
Hao mara nyingi wanakuwa wamesoma kitu tofauti na walicho ajiriwa kwa mfano mwalimu anaenda kusoma finance au law au procurement anatakiwa afanyiwe recategorization kitu ambacho sio rahisi lakini mwalimu wa certificate akaenda kusoma diploma ya ualimu bachelor ya uwalimu na masters ya ualimu ila ukienda tofauti ni tatizo.
 
Ni kitu hicho hicho, utumishi hauwajui vizuri
 
Back
Top Bottom