Ushauri kwa wadogo zangu, kaka na dada zangu wanaotaka kukata tamaa kisa wamefeli Kidato cha Nne

Mar 28, 2014
38
27
Habari wakuu wangu wadogo marahaba wakubwa shikamooni.

Kwanza natanguliza shukurani zangu dhati kwa wote mliopitia hapa na kusoma uzi huu.

Leo napenda nitoe ushauri kwa wadogo zangu kaka zangu dada zangu mliomaliza Form four na matokeo kuja tofauti yaaani kufeli kupata four au zero kabisa. msikate Tamaa bado una nafasi ya Kuwa unavyotaka Kuwa, Kufeli shule sio mwisho wa kila kitu.

Unaweza ukawa ulipitia changamoto nyingi mfano zikiwemo ada, mamb ya kifamilia, Ubovu wa watoa taaluma, ukosefu wa hela za masomo ya ziada, umbali msongo wa mawazo makundi, magonywa nk

Hata me nilifeli form four nilipata zero tena zero plus (nimenogesha yaan zero ya mwisho namaanisha) lakini sasa Mungu kanitambulisha chuo kuwa Mwanafunzi bora kati ya wanafunzi Bora class Imagine how mambo yanavyobadilika from zero to best student.

Nakumbuka nilichekwa sana afu dogo alipata one ya 11 Akimaliza Azania Sec School kaka nimepata zero iliuma sana nilikosa pa kukimbilia nikawa mfano mbay mtaani ila sikukata tamaa hata walionicheka kipindi kile mitaa ishawameza. Wale wenzangu waliosikiliza maneno ya Mtaa Mitaa inawacheka wao sahivi.

Nilirudia na kurudia mpaka nilipopata credit za kusoma chuo.

Kikubwa Usikate TAMAA sahiv utasemwa utadharauliwa utaonekana hauna kitu kichwani debe tupu utachekwa utatukanwa Wazazi walezi ndugu jamaa watakuumiza na kila namna ya maneno ya kuvunja Moyo, INAMA, LIA, INUKA KISHA futa MACHOZI, plan zako usimwambie Mtu isipokuwa Mtangulize Mungu.

ANZA upya Bado nafasi unayo kile unachokiamini Iwe kurudia shule au kusimamia Kipaji ulichonacho fanya kwa Nguvu Utawashangaza siku Moja, Hakikisha Mungu Juhudi Nidhamu wanakuwa rafiki zako wa kila siku usiwaache🙏

NB: nashindwa attach chet sababu kina majina yangu kamili

Nawasilisha✍️
 
Matokeo yametoka, waliofeli wakiwa na matarijio ya kuendelea juu kimasomo ndio huumia zaidi kuliko wale ambao matokeo yoyote kwao wanaona kawaida tu, kuna ambao hawana namna tena kurudia mtihani ili wapate cheti cha kuomba kozi za vyuo, hawa ndio wa kutiwa moyo wasimamie vipaji vyao ndio vitakuwa mkombozi wao.
 
Matokeo yametoka, waliofeli wakiwa na matarijio ya kuendelea juu kimasomo ndio huumia zaidi kuliko wale ambao matokeo yoyote kwao wanaona kawaida tu, kuna ambao hawana namna tena kurudia mtihani ili wapate cheti cha kuomba kozi za vyuo, hawa ndio wa kutiwa moyo wasimamie vipaji vyao ndio vitakuwa mkombozi wao.
Umenena vyema kiongozi
 
Back
Top Bottom