Tanzania Mpya
JF-Expert Member
- Apr 11, 2012
- 252
- 145
Safi sana na wamtafute Kiongozi wa Daladala kama Mwaibula sijui Mwaisabula???? as waliofuatia hawajafit viatu vyake kwa kweli!Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Paul Makonda, naomba uliangalie suala la usafiri ktk jiji lako la Dar es Salaam. Kwa sasa hali ilivyo ni vigumu sana kwa magrupu maalumu kupata usafiri (daladala) nyakati za asubuhi na jioni. Jamii ya wasafiri au watumiaji wa usafiri huu jijini Dar kwa kweli hawajawathamini Wazee, Akina mama, Wajawazito, watoto, na walemavu ktk kupata usafiri hasa kwa nyakati hizo.
Magrupu haya yanaweza kukaa kituoni kwa muda wa masaa hata matatu bila kupata usafiri, wakati vijana wenye nguvu na wasiojali wanakuja kituoni na kutumia nguvu na kuondoka mara moja.
Naomba ktk uongozi wako mh, ufikirie utaratibu wa kupanda magari haya kwa foleni. Yaani, aliyetangulia kufika kituoni apate usafiri mapema na sio kutegemea nguvu. Utaratibu huu utawasaidia hao niliowataja hapo juu kutohangaika na usafiri wa kwenda hospitalini, makazini, mashuleni, na majumbani na pia.
Utaratibu huu unawezekana, ni kujipanga tu na kufanya maamuzi. Tuikatae aibu hii ya kutothamini wazee, walemavu, wajawazito na watoto katika jamii yetu. Wakati umefika sasa tutende haki.
Nakutakia kazi njema Mkuu.
any way kila wazo ni wazo ngoja tulipokee ila italazimu kila kituo paajiriwe mtu kama bank wa kusimamia hizo foleni kuzuia wachepukaji duh sidhani lakini
Wazo zuri tuone aibu Kwenye hili Ni kweli wanateseka mno hili kundi tajwa lakini utaratibu huu unaweza kufanya kazi labda Kwenye vituo vya mwendo kasi pekee ila huku mbagala zakhem kwetu mydear itabaki kuwa ndoto tu , natamani Yale mabus ya wanafunzi yangenunuliwa kipindi cha awamu hizi huenda yangedumu hata miezi mitatu maana yale yalifanya kazi siku tatu yakatoweka kabisaaa ahahahahhahahahaha.
Ni wazo zuri na huo ndio utaratibu wa watu walostarabika. Ishu hapo ni namna gani ya kutekeleza huo mkakati.
Ni kweli kabisa mkuu,PENYE NIA PANA NJIA.
Sasa si ndo maana ilibuniwa mabasi yaendayo kasi?
ili kutatua mambo kama haya
Mleta uzi "BIG UP" hakuna lishindikalo chini ya jua.
Sasa si ndo maana ilibuniwa mabasi yaendayo kasi?
ili kutatua mambo kama haya
SidhaniSizani
Mleta mada hili ni suala la "Discipline" and "Attitude" na ni vizuri kama litazingatiwa au litafundishwa toka mwanzo hasa kwa watoto wetu,
Mtu mzima kumbadili tabia ghafla sio kazi rahisi kama tunavyofikiria,
Nchi kama Japan na Singapore mbona haya mambo yamewezekana? tena wala huoni msimamizi wa kuwasimamia watu eti ili waingie kwa nidhamu na utaratibu...Hakuna kisichowezekana ni suala la kujiongoza tu.