Mjukuu wa kigogo
JF-Expert Member
- Sep 19, 2023
- 440
- 1,081
Buunda inamajuungu Sanaa muraKwanza shikamoo mheshimiwa diwani.Kwanza kabisa pongezi sana kuwa kiongozi mchapakazi sana ni kiongozi wa kata ngumu zaidi kisiasa wilayani Bunda,NYASURA.Kata hii pia inatajwa kuwa ni kati ya kata Tano ngumu zaidi mkoani Mara.Kiuhalisia kuwa mshindi katika uchaguzi ndani ya Chama au ule unaohusisha wagombea wa vyama mbalimbali katika kata ya Nyasura ni kielelezo tosha kabisa unakubalika zaidi kwa wananchi bila kujali itikadi ya vyama vyao. Nikiwa ni mwanachama pia wa Chama cha Mapinduzi napenda nikupe huu ujumbe
1.PONGEZI
Binafsi nikiri wazi wewe ni mchapakazi sana ukiwa umeshiriki kwenye shughuli nyingi sana katani hususani ujenzi wa shule,barabara,vituo vya afya nk.Jambo jema umekuwa ukishiriki bila kutafuta kiki.Ninaposema bila kutafuta kiki ni Kwa kuwa matukio mengi umekuwa ukiyafanya vipindi vyote hasa zile nyakati ambazo siyo za uchaguzi.Kwangu mimi naamini bado unastahili kuendelea na nafasi ya udiwani kwa miaka zaidi!
Pongezi nyingine ni kutowagawa wananchi wako wa kwa itikadi za kisiasa hata kwenye mikutano ya hadhara na kuwapa FURSA ya kukuchallenge wapinzani wako.Hii ndio maana halisi ya siasa!
2.CHANGAMOTO
Hapo Nyasura shughulika sana na mpasuko wa wakazi wa Eneo liitwalo Zanzibar na hasa baada ya kura za maoni zilizompa nafasi nyabaturi Ndege kuwa mgombea na hatimaye kushinda uenyekiti.Eneo Moja wameanza kuonyesha uasi wa kujitenga na kuanza kuunda ngome (strong hold) ya upinzani.Tuzibe ufa mapema tusije kujenga ukuta!
Kuwa makini na hizi Team za wagombea ubunge,utakapounga mkono upande ambao ni mbovu hilo ndilo litakuwa anguko lako la kisiasa na heshima yako itakufa rasmi!Baki neutral mkuu utapotea otherwise karata zako uzichange vizuri zaidi Eneo hili.
Kwenye vikao vya maendeleo katani Kuna baadhi ya watu wenye ushawishi wamekuwa wakikwamisha kupitishwa kwa agenda Kwa interest zao binafsi na hasa kutafuta umaarufu .Kundi hili linaongozwa na mwenyekiti mmoja wa bodi ya shule Moja ya msingi(Jina kapuni).Hawa watu wanafahamika,Watafuteni faragha mzungumze nao ili kuepusha mikwaruzano isiyo na maana Kwa siku za mbeleni!
Wakati ni ukuta......
Masahihihisho
Jina ni Magigi Samuel Kiboko