Ushauri kwa Anayejua Solar za Fenix

Jumanne Mwita

JF-Expert Member
Nov 18, 2014
516
1,348
Habari? Naomba kuuliza kwa ambae alishawahi kutumia Solar kampuni ya Fenix, solar zao zikoje na ziko vizuri kuliko Sundar ambao wameliteka soko la nishati ya jua?

Kama ulisha wahi kuitumia naomba unisaidie hapa kujibu au maoni maana nimepata mtu anauza hiyo solar ya Fenix kwa upande wangu sijawahi itumia. Uzoefu wangu ni kampuni ya Sundar ndio naitumia mpaka sasa.

Naomba ushauri ikiwa anayeiuza solar hii anauza kitonga sasa nisije jichanganya kumbe ni kanyaboya nashikishwa kwa wale wataalamu wa haya mambo naomba kupata ushauri.

Pia nina swali jingine, ninaweza kuziunga solar hizi mbili yaani Fenix na Sundar zote ni 100W hakuna shida yeyote kuchanganya kampuni?
 
Back
Top Bottom