ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 21,507
- 51,160
Wakuu nilikuwa na msichana fulani niliyeishi naye miaka takribani mitatu ila bahati mbaya hatukupata baraka za kuwa na watoto na kibaya zaidi tukaja kuachana kwa mambo fulani fulani ambayo sioni haja ya kuanza kuwachosha kuyaelezea.
Ila sasa mama yake alikuwa ni mtu mwema kwangu kiasi kwamba nikawa namsaidia pesa ndogo ndogo kwa kuwa hali yake sio nzuri sana ya kiuchumi, kama ni ugomvi tunao mimi na mwanaye tu na toka niachane na mtoto wake sijawahi kuongea naye tena na ni takriban miezi sita sasa imepita na nimepata mchumba fulani ambaye bado tunapangana pangana.
Sasa nimeotea hela kwenye mitikasi yangu ninawiwa kumtumia pesa mama mkwe ila naona kama inaweza ukawa mwanzo wa kuanza kurudisha rudisha mahusiano tena mambo yakawa mengi tena maana wananijua in and out.
Mimi nina tabia ya upole na huruma natamani tu nimsadie ila nataka isiwe sababu kwamba bado nawawaza waza isitoshe ni watu fulani wa mambo za Kiswahili swahili nadhani mshaelewa yaani, mambo ya kiwitch witch wanaziamini.
Mnasemaje nimsalimie na ku boost kidogo ka 30000 au nile buyu tu.