Ushauri kati ya DOM na DAR

baby nillaah

Senior Member
Apr 7, 2017
110
64
Habari za wakati huu wanajamvi ,naomba mnipe USHAURI je mi wapi patanifaa kwenda kuzichanga changa kutokana fursa zilizopo eneo husika kati ya Dom au dar ni wapi Kuna unafuu wa gharama za maisha...... ahsante nawasilisha
 
Dar es salaam kuna unafuu kuliko Dom hilo liko wazi,Dom utakuta nyumba ya kawaida kabisa ambayo Dar ungeipata kwa 30 hadi 40 utashangaa kule 50 hadi 60 na hata chakula Dom ni ghali mno kuliko Dar..Pia Dom usafiri ni changamoto sana unaweza ukawekwa stend saa limoja na nusu unasubiri gari tu na wenyewe wanaona kawaida eti..
 
Ahsante... Kuna mtu pia ananambia Dom vyumba ghari sanaa..
 
Ujasiriamali mdogo mdogo mradi tu
Maisha yaende.
Dar mkuu.

Kila biashara huku inalipa. Kikubwa umakini na juhudi.

Ingawa kama una mwenyeji ingekua poa zaidi maana unahitaji mwezi mmoja wa kujua eneo zuri la biashara yako, na mahala utakapokua unatoa mzigo na mahali utakapo kaa (kodi chumba).

Kama mwenyeji poa zaidi. Atleast unaweza jua jinsi utakapoanzia.

Maeneo kama Sinza unaweza pata hadi chumba kwa 50-70 kwa mwezi ingawa kuna michango kama Maji, umeme na usafi inaweza fika 20 kwa mwezi, hafu biashara zako ukawa unafanya Mawailiano, hadi Mwenge. Hapo ata dala dala haupandi unatembea tu.

Kama bishara zako haziitaji fremu unaibuka Kariakoo ingawa uko itabidi ukakae nje ya mji kidogo kule nyumba hazigusiki.

Karibu sana mzee baba waambie wakazi wa Ipogoro Kihesa Ilula Kidamali Kalenga hadi TRM wakuombee.
 
Ahsante sanaaa....Nmepata na muongozo Incase nakuja huko mjini basi najua how to start
 
Habari za wakati huu wanajamvi ,naomba mnipe USHAURI je mi wapi patanifaa kwenda kuzichanga changa kutokana fursa zilizopo eneo husika kati ya Dom au dar ni wapi Kuna unafuu wa gharama za maisha...... ahsante nawasilisha
Dar upatikanaji wa Hela ni rahisi na hata Vyakula vya Bei nafuu vipo ila Dodoma ni pazuri ukiwa na Kazi kwani upatikanaji wa Vyakula ni mkubwa zaidi.

Dar es Salaam ukiwa huna Hela hutokosa kwa Kula au Mtu wa hata Kukutoa na Buku ila kwa Dodoma utalala Njaa kwani Watu hawana Hela.

Dodoma ni Mkoa wa Kusainiwa tu Cheques ( Cheki ) za Hela ila Dar es Salaam huku ndiko ambapo zinatumika vizuri.

Mwisho ni kwamba 95% ya Wafanyakazi na Watu wote wenye Hela walioko Dodoma kila Ijumaa wanakuja kula Raha Dar es Salaam na Jumapili wanalianzisha kurejea Dodoma.

Ushauri wangu tafuta Fursa hapa Dar tu
 
Back
Top Bottom