KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,773
- 4,937
Kwako Rais wa JMT,
Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan,
Awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mungu kwa kutujalia kufika muda na wakati tukiwa tu wazima wa afya na kuendelea kulijalia Taifa letu amani, umoja na mshikamano.
Pia, nakupongeza kwa kuteuliwa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, nampongeza pia Dkt. Hussein Mwinyi kuaminiwa tena na kuteuliwa kugombea Zanzibar, nampongeza Dkt. Emmanuel kwa kuteuliwa kuwa mgombea mwenza wa CCM na pia nampongeza MZEE WASSIRA kuchaguliwa kuwa makamu Mwenyekiti CCM Bara.
Mhe. Rais, pamoja na mambo mengi napenda kutoa ushauri wa kuanzishwa ofisi ya mshauri Mkuu wa Taifa ambaye atawajibika kwa Baraza la Mawaziri au kwako mhe.rais.
Ofisi hii ndio itakayowajibika kutoa ushauri wa kitaalamu kwa taasisi, idara, wizara na mamlaka zote na zaidi itasaidia ku-organize kazi na majukumu ya washauri mbalimbali waliopo nchi.
Kwa mtazamo wangu, pakiwa na hii ofisi itasaidia kupatikana kwa ushauri mzuri zaidi kwa sababu utakuwa unaratibiwa kitaasisi na zaidi kwa sababu itakuwa inawajibika kwako au kwa Baraza la Mawaziri basi ushauri wao utakuwa unaheshimika.
Pia, itasaidia kuondoa migogoro mbalimbali kwa kuwa kila taasisi itakuwa inafahamu wapi pa kuanzia kutafuta ushauri migogoro inapotaka kuibuka.
Pia , itasaidia kuchochea mabadiliko ya Kasi kwa sababu itatoa ushauri kwa haraka kwa mambo mbalimbali kwa kuwa itakuwa imejikita kufanya hivyo.
Pia, itakusaidia kupata ushauri wa mambo mengi kwa wakati mmoja kutoka kwa mshauri Mkuu wa Taifa kuliko sasa inakubidi kukutana na washauri mbalimbali ukitaka taarifa mbalimbali.
Naomba kuwasilisha.
Ahsante