Nimekuwa na mpenzi wangu(mchumba) kwa takribani mwaka sasa, mara nyingi tumekuwa tukikwazana lakini tunasuluhisha na kusonga mbele.Ugomvi mkubwa hasa naweza sema ilikuwa pale alipoambiwa tu kwamba nilijaribu kumtongoza rafiki ake na alilazimisha tuachane lakini mimi ilinibidi kumueleza kweli yote na kumsihi asiyasikilize ya watu tena na alionekana kurudi nyuma na akakubali tuendelee.
Sasa ndugu zangu, kwa muda kama wa wiki mbili ulopita kutokana na vile alivyokuwa akiona namkosea mambo mengine madogomadogo nahisi alihisi huenda simpendi na ni kwa sababu ya Ex girlfriend wangu (japo si kweli na sina mawasiliano naye) nahisi alifikiria hivo kwa sababu siku fulani tulipogombana nilimtaja huyo Ex kwa kumwambia hiyo tabia alonionesha my Ex hakuwa nayo(nadhani hapa nilikosea).Kutokana na hilo alianza kufuatilia namba za huyo Ex na akafanikiwa kuzipata na huyo Ex (ambaye kimsingi nilimuacha mimi)alimueleza mambo mengi kunikandia na mbaya zaidi alimweleza kuwa nilimtongoza tena nilipokwenda likizo nyumbani(Jambo nililonianya nishangae), baada ya hapo aliniita vizuri tu kama kuna amani na nilipofika alinambia alichoambiwa kwa uchungu.Nilionesha kuchoka kujitetea kwa jambo moja kwani angeniona muongo lakini ilinibidi nifanye hivyo ila hakuonesha kunielewa kwani hata kwenye simu aliniblock kabisa nisimpigie kwani alinambia hataki mapenzi tena ameumia sana ,ilibidi niwatumie ndugu zangu hapo alionesha kuelewa na siku hiyohiyo alinipigia simu yeye kuniuliza nipo wapi na ninafanya nini, nilimjibu na baada ya hapo aliniaga kwa kusema "usiku mwema" cha ajabu ile asubuhi tu nilipompigia alikuwa akinijatia simu naalizidi kukumbushia ya nyuma yote(kwa meseji alidai mapenzi hataki tena).Ilinibidi nimtafute ana kwa ana kidogo akaonesha kurudi nyuma tena na akaniomba tusubiri mitihani iishe tutazungumza, tuliendelea kuwasiliana hata kiss nilipomuomba alinipa lakini hakutaka nimuite mpenzi akidai bado moyo wake haujarejea ktk mapenzi.Wakati huo wa mitihani tulishirikiana na niliendelea kumsaidia nikisubiri mitihani iishe tuzungumze kama alivyosema yeye.
Wakuu, tupo wote chuo na tunakaa hostel japo kwa sasa tumefunga na tulipofunga tu aliniaga anatoka kidogo kwenda kwa birthday ya rafiki ake nimsubiri hostel atarudi tuzungumze cha ajabu wakuu muda aloniahidi kurudi ulipita sana na nilipompigia simu alikata na alinitumia meseji kwamba msimamo wake ni uleule kama inawezekana nimtafute tu mwingine lakini yeye ahitaji tena kusikia mapenzi na tayari amekwisha ondoka yupo nyumbani(maanake hostel harudi) na kuanzia hapo niligundua kaniblock tena calls, whatsapp na jana kaniblock hata fb, nimekuwa nikimtumia meseji hajibu tena mpaka leo.
Wakuu naombeni ushauri wenu nifanye nini kiukweli nampenda..? Wote naihitaji ushauri wenu kutokana na experiences zenu ktk hili utanifaa sana.