Mimi ni msichana mwenye umri wa miaka 28. Nilikua kwenye mahusiano na kaka mmoja kwa kipindi cha miaka minne, kwa kipindi hicho nilimpeleka kumtambulisha kwa wazazi, hakunitambulisha kwa ndugu zake akidai kwamba siku chache kabla ya kuleta mahari angenipeleka kwao.
Kuanzia mwezi wa kumi mwaka jana alianza kubadilika, kupunguza mawasiliano, majibu ya mkato na mambo mengine kibao. Sikujali saana nikijua labda ana mambo yake binfsi.
Wiki chache kabla ya tarehe ya kuleta mahari nilifatwa na wanawake wawili wakidai ni wake zake, mmoja kazaa nae watoto wawili, na mwingine kazaa nae mtoto mmoja, nilipomuuliza alidai ni kweli amezaa nao lakini hana mpango wa kuwaoa. Nikiangalia umri wa mtoto wa mwisho ni kama miaka miwili hivi ina maana alikuwa na mahusiano nae kipindi akiwa na mimi.
Kinachoniuma zaidi kuna baadhi ya vitu vyangu nilimpa afanyie kazi ikiwemo laptop, printer, na kuna hela aliniazima kama 550,000/= Kuanzia mwezi huu mwanzoni niliamua kuanza mazoezi ya kumpotezea, bila kumwambia lolote ili hasira zipungue halafu nije nifate vitu vyangu nikiwa sina hasira.
Naomba mnisaidie wapendwa jinsi ya kufanya ili siku nikienda kufata vitu vyangu nimuone wa kawaida, roho inaniuma mno kwa sababu nimepoteza muda wangu, aibu nyumbani, halafu nashindwa kabisa kumsahau, najisikia kufa kufa, nashinda nalia, nina hasira kwa kila mtu mpaka wenzangu ofisini wananishangaa.
Nitaitoaje hii hali nisaidieni mliopitia hali hii please!