Kuelekea 2025 LGE2024 Usawa wa Viongozi wanawake na wanaume bado ni kitendawili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Thabit Madai

Member
Oct 8, 2024
52
137
IMG-20241023-WA0135.jpg


NA AMRAT KOMBO, ZANZIBAR

Usawa wenye hadhi sawa unamaanisha kwamba watu wote katika jamii wanapaswa kuwa na fursa sawa za kushiriki katika ngazi ya maamuzi na uongozi. Hali hii inategemea muktadha wa kisiasa,kiuchumi na kijamii .

Ingawa kuna ongezeko la uwakilishi wa wanawake katika Bunge na Serikali, takwimu zinaonesha kuwa idadi yao ni ndogo ikilinganishwa na wanaume. Kulingana na Ripoti ya Umoja wa Mataifa UN ya mwaka 2022 inaonesha wanawake uwakilishi ni asilimia 26.1 ya viti vya Bunge duniani kote.

Na kwa upande wa wanaume walikuwa na uwakilishi wa asilimia 73 ya viti hivyo. Hii inaonesha kwamba wanaume bado wanashikilia sehemu kubwa zaidi ya viti vya maamuzi katika serikali za nchi mbalimbali.

Chama cha ACT -WAZALENDO wametoa Baraza la wasemaji wa kisekta lenye muundo wa Wizara za 16 ili kufuatilia utendaji wa serikali kisera, kisheria na kiutendaji ,lakini kinachosikitisha katika Baraza hili usawa wa kijinsia ulikuwa ni mdogo .

Ukiangalia wasemaji waliteuliwa wa sekta hiyo wanaume ni 15 mwanamke ni mmoja hii inaonesha kuwa usawa wenye hadhi sawa bado ni changamoto.

Naibu Katibu wa Chama cha ACT WAZALENDO Zanzibar,Omar Ali Shehe Amekiri kuwepo kwa changamoto ya uhaba wa wasemaji wanawake kulinganisha na wanaume ila amesisitiza kwamba kutokana na mikakati ilowekwa itasaidia kutatua changamoto hiyo kwa kuwapa uelewa na ujasiri wasemaji wasaidizi wananwake.

“ Ni kweli kwa upande wa wasemaji rasmi wanawake ni kidogo kuliko wanaume, na tumeweka hivi kutokana na mikakati tuliyoiweka katika kuwajengea uwezo,ili kuweza kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya jamii zao.”Amesema Omar

huku akiongeza kuwa “Wengine tumewachaguwa kuwa wasemaji wasaidizi kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo ujasiri ili kuimarika na kuweza kuja kuwa wasemaji rasmi”.Ameongezea Omar wakati wa mahojiano.

Mwenyekiti wa uchaguzi wa Chama Cha ADA -TADEA Juma Ali Khatib amesema katika chama chao wanafuata usawa wa kijinsia japo kuwa asilimia ya ushiriki wa viongozi wanawake ni ndogo

.“Usawa wa kijinsia katika nafasi ya uongozi katika chama chetu upo kwani makamu mwenyekiti wa chama chetu ni mwanamke japo kuwa kwenye asilimia ya viongozi wanawake ni 30 na wanaume 70 na hii inatokana na muamko mdogo wa kujitokeza kugombea kwa upande wao.” Amesema Juma.

Takwimu zinaonesha kuwa wakuu wa mikoa mwanamke ni mmoja sawa na asilimia 20,wakuu wa wilaya wanne sawa na asilimia 36 na masheha wanawake 79 sawa na asilimia 20, wanaume 309 sawa na asilimia 80 kwa masheha wote wa Unguja na Pemba ambao ni 388.

Mwakilishi wa Jimbo la Dimani Mwanaasha Khamis Juma ambaye amewania kupata nafasi hiyo amesema usawa wa kijinsia bado ni kipengele kikubwa japo kuwa dhamira ni kufikia asilimia 50 kwa 50 wanawake na wanaume.

“Katika mwaka 2020 wanaume walijitokeza kugombea nafasi ya uwakilishi 190 na walioshinda 42, ukilinganisha na wanawake waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ilikuwa 61 na waliobahatika kushinda ni 8, kupitia idadi hii bado tunasafari ndefu ya kufikia asilimia 50.

Mwanaasha ameeleza sababu ya kutofikia asilimia kubwa ni bado baadhi ya vyama vya siasa wana mtazamo hasi kwa wanawake, hivyo amewashauri vyama hivyo kutoa nafasi kwa wanawake hao ,

“Mfumo wa kisiasa unakosa uelewa kuhusu umuhimu wa ushiriki wa wanawake, hupelekea wanawake kupata vikwazo vya upendeleo wa kijinsia. Ambavyo huchangia nafasi za wanawake kushika nafasi za maamuzi kuwa chache” Amesema Mwanaasha

Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar ,Thabit Idarous amesema wanawake wamepewa fursa mbalimbali za uchaguzi tofauti na historia ya nyuma kwani walikuwa wananyimwa haki hiyo.

“ Kutoka mwaka 2015 hadi 2020 wamejitokeza wanawake takriban 80 kugombea nafasi mbalimbali ikiwemo uwakilishi,ikilinganishwa na wanaume zaidi ya 400 waliojitokeza kugombea nafasi hiyo." Amesema Thabit

Akizungumzia juu ya kuwepo kwa sera maalum ya jinsia kwenye vyama vya siasa Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa

“Changamoto kubwa ipo katika vyama vya siasa ,hivyo vitakapofanya marekebisho ya sera maalumu ambayo itatoa ushawishi wa kuongeza idadi ya viongozi wanawake kwenye majimbo, itasaidia kuwa na muaroubaini wa tatizo hilo.” Ameongeze Thabit

Takwimu za uchaguzi wa mwaka 2020 kwa upande wa Zanzibar wabunge walioteuliwa na vyama kugombea nafasi hiyo wanaume 257 walioshinda 46 ambapo wanawake walikuwa 81 na walioshinda wanne hali hii inaonesha wazi kuwa bado usawa wa kijinsia ni suala lisio na usawa kwenye uteuzi hata ndani ya vyama.

Mkurugenzi wa Chama cha Wanasheria Wanawake Zanzibar – ZAFELA Jamila Mohammed, amesema bado tatizo la usawa wa kijinsia katika jamii hawajalipa kipaumbele kwasababu mbalimbali ikiwemo kuwepo kwa mfume dume pamoja na kutokuwepo kwa sheria madhubuti ambayo itasaidia kuongeza idadi ya viongozi wanawake.

“Sisi tunajitahidi kutoa elimu kwa kushirikiana na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA – ZANZIBAR kwa viongozi wa vyama vya siasa ili kutoa fursa sawa za uongozi kati ya mwanamke na mwanaume lakini hadi sasa bado muamko ni mdogo”. Amesema Jamila

Baada kupata maoni hayo muandishi hakuishia hapo alikwenda kukutana na wananchi mbali mbali nakutoa maoni yao juu ya suala hili la usawa wa jinsia katika uongozi.

“Kuna jitihada mbalimbali zinazofanywa ili kuhamasisha ushiriki wa usawa kati ya wanaume na wanawake unakuwepo , lakini bado kuna kazi kubwa inahitajika ili kubadilisha mawazo potofu kwa jamii kuhusu mwanamke.” Amesema Khamis

“Katika vyama vya siasa uteuzi wa wagombea mara nyingi unategemea vigezo vya kifedha na ushawishi badala ya uwezo wa kisiasa au ujuzi,wanawake mara nyingi wanakosa fursa hiyo kutokana na ukosefu wa rasilimali na mtandao mzuri wa kisiasa .“ Amesema Amina


IMG-20241023-WA0136.jpg
 
Back
Top Bottom