Baada ya LOWASSA kuhamia CCM, Chadema wametengeneza agenda ya kutaka kuendeleza porojo zao dhidi yake. Eti amerudi CCM ili Mali zake na familia yake iwe salama. Agenda ya Ufisadi hawawezi kuinua kinywa kumtuhumu kwa vile wanajua watachekwa sana. Nimemsikia Halima Mdee akisema Lowassa amewasaliti watu waliompa heshima baada ya alichokiita kudhalilishwa na CCM baada ya kukatwa kuke Dodoma. Hakika wakati mengine nafikiri kuwa Mwanasiasa ni punguani(hazimtoshi vizuri) siyo wote lakini mnisamehe. Hivi akina nani walimdhalilisha Lowassa? Chadema waliopita ndani na nje ya Tanzania wakitangaza LOWASSA ni Fisadi lakini akahamia kwao au CCM waliomkata kuepuka kushindwa uchaguzi kwa sababu ya ufisadi wake uliohubiriwa na CHADEMA?
Nimeona hata Magazeti ya leo yanasema sasa ni LOWASSA na Chadema, wakati maskini wa Mungu Mzee wa watu hatasema chochote.
Chadema wanataka kutuambiaje kuhusu hizi Mali za LOWASSA wanazosema, ni haramu au halali? Kama ni halali Serikali izitakie nini? Si walitakiwa wajitokeze kwenye vyombo vya habari wamtete Mjumbe wao wa Kamati Kuu na aliyekuwa mgombea wao wa urais huku wakiwaonesha Watanzania uhalalli wa mali zake huku wakiitaka Serikali imuache? Kama siyo halali, Vipi walikaa naye muda wote bila kumkataa kwa sababu hiyo?
Sikio la kufa halisikii dawa, sijui ni uchanga/ulimbukeni au kujitoa ufahamu. CHADEMA wanarudia kosa lile lile la kupoteza muda wakihangaika na Lowassa. Hii ya safari hii ni mbaya zaidi. Lowassa kivyovyote vile hawezi kuwa mgombea wa CCM, 2020, 2025 n.k. Kimsingi LOWASSA siyo kwamba hawezi tena biashara ya jumla (Augustino Mrema) bali hata ya rejareja hawezi kufanya, alichofanya LOWASSA ni kutafuta heshima ya kustaafu akiwa Chama cha Ukombozi, Chama Tawala, Chama cha Baba wa Taifa.
Banaye, CHADEMA Mnatia kinyaa, nini mnataka kuwaonesha Watanzania? Kwamba siasa za maji taka mmezaliwa nazo , mnaziishi na kuzienzi? Au kwamba Lowassa ameondoka ghafla kama ambavgo MAKALA ya Hemedi Ali ilivyokuwa inasema? Kama ndivyo ugulieni kimyakimya, labda mtaonekana mmekomaa kisiasa kuliko kubwabwaja.
C.C Tundu Lissu, Halima Mdee, Peter Msigwa, Godbless Lema. Kuweni Kisiasa, Taifa linawategemea.
Jumamosi njema.
Saa nne usiku ni JS Soura vs Simba SS. Nimeshatinga uzi wangu wa Tanzania , Tanzania kwanza, Simba na yanga , Makamba na Matonya baadaye.
Merci Beaucoup
Au Revoir.