Usajili wa line na vibao vya makazi havina tija kwa Wananchi

commonmwananchi

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,377
1,954
Wezi wa mitandao wameishinda serikali! Vibao vya makazi vimeimarisha nini tangu kuwekwa kwa gharama ya zaidi ya B360?

Tunashuhudia kila mwaka nchini, Serikali kupitia TCRA, tukielekezwa na kulazimishwa kusajili line za simu kwa watumiaji wapya, lakini pia kuhakiki kwa wale ambao walikwisha sajili awali.

TCRA inatufanyia au kuwasababishia usumbufu baadhi ya wananchi wa Tanzania hii hususani wale wa vijijini.

Kwani hulazimika kutumia gharama za ziada ili kukamilisha zoezi hilo, ikiwemo usafiri ili kufikia ofisi au matawi ya mawakala wa mitandao ya simu nchini.

Hii inakuwa ni kutuongezea gharama na makali ya maisha juu ya yale ya msingi tunayopitia kwa sasa, ikiwemo mifumko ya bei na Tozo.

Pia ni wazi kwamba zoezi hili halina tija kwa wananchi bali kwa Serikali, hususani wakati wa uchaguzi pekee. Nasema hivyo kwa sababu kama ni kudhibiti wizi wa mitandaoni, zoezi hilo limeshindikana. Wananchi wameendelea kuendelea kuibiwa mamilioni kila uchao.

Pia tumeendelea kuona watu wakighushi na kutumia majina ya viongozi wa kitaifa kwenye mitandao ya kijamii na kukusanya pesa kwa uhuru bila vyombo husika kuwadhibiti.

TCRA, Police Cyber Crime wote wapo ila hakuna chochote.

Upande wa vibao vya makazi, mradi uliopigiwa chapuo na serikali nchi nzima, huku ukitumia mabilioni ya shilingi za Kitanzania za walipa kodi na wakatwa Tozo wa nchi hii, lakini niambieni ni vibao vingapi ambavyo bado vimesimama na vinasomeka?

Pia niambieni kama nitaweza kwenda toka sehemu moja ya nchi hadi kwingine bila kumuuliza mtu?

Je, hizo bilioni 360 zingeingizwa kwenye sekta ya afya nchini, ni ipi ingekuwa tija zaidi?
 
Back
Top Bottom