Usajili wa Engineers, Kwenye Bodi ya Wakandarasi (ERB) Hatua zake inakuwaje kusajiliwa?

Evans-Arsenal

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
868
1,385
Naomba kufahamu jinsi mtu aliyemaliza Chuo anavyoweza kujiunga au kusajiliwa na Bodi ya wakandarasi hapa Tanzania (ERB)
 
Naomba kufahamu jinsi mtu aliyemaliza Chuo anavyoweza kujiunga au kusajiliwa na Bodi ya wakandarasi hapa Tanzania (ERB)
Umechanganya sana habari. ERB ni Bodi ya Usajili wa Wahandisi(Binadamu,Watu ambao ni Professionals)!
Usajili upo wa aina nyingi kidogo lakini zinazotuhusu wazawa ni Tatu kama siyo nne/tano:-

1. Consulting Engineers and Consulting Firms
2. Professional Engineers
3. Graduate Engineers(fresh from School au yeyoye atakayezembea kujisajili ERB hata kama ana miaka 40 kwenye tasnia ya Uhandisi bado atakua ni Graduate Engineer)
4. Professional au Graduate Technician Engineer
5. Technician Registration.
Unaweza kupata maelezo ya kina kwenye tovuti yao, wewe google ERB utapa yote hayo,japo nimeeleza kidogo baaddhi inaweza isiwe kiusahihi sana.

Swali lako limejikanganya kidogo. Umezungumzia Graduate Engineer kujisajili Bodi ya Wakandarasi. Hapo umekosea,kwa sababu CRB-Contractors Registration Board(Bodi ya Uasjili wa Makandarasi) haisajili watu,bali husajili Kampuni za Kandarasi za Ujenzi,Umeme,Mawasiliano na Specialist,kwa ufupi ili kusajili kuwa Mkandarasi lazima ufuate michakato yote ikiwemo Incorporation,MoU,Brela,Wataalam ikiwemo wewe Mhandisi na wataalam wengine,Vifaa,Mtaji nk.
Kwa kifupi

ERB-Wataalam
CRB-Kampuni za Kandarasi hasa za Miundombinu kama Ujenzi nk
 
Asante mkuu nmekuelewa sana ntafanya hvyo.
 
Kama umelenga ERB na hukuwahi kujisajili Tafuta fomu za Registration especially GE(Graduate Engineer).Nyaraka ambazo utaambatisha ni Cheti cha kidato cha 4&6,kuzaliwa,Cheti cha Chuo&Transcript yako.Aidha,usisahau kudumbukiza Ada yako ya maombi ya usajili.Baada ya kuwasilisha Maombi yako itakupasa kusubiri Board Meeting kujadiliwa kwa maombi,kama utakidhi vigezo Majina yatatangazwa na kuendelea na hatua ya kuanza kulipa Annual fees na kwa GE mpaka upate Professional Experience(almost above 3yrs not less)
 
Asante mkuu.
Nmeshaiona fomu yao, na graduate engineer lazma awe na experience ya 3yrs kwenye field yako oky, mara ya kwanza nkajua kunakuwaga na mitihani ya kufanya ndo uwe registered na ERB..
 
Aisee mimi sio Engineer wala sijasomea Civil Engineering lakini huyu jamaa kilaza kweli, yaani unashindwa kujua hata kujua vitu muhimu kama hivo vinavohusu taaluma yako?
 
Dogo ngoja nikusaidie. Mana mi pia ni professional engineer. Kuna njia mbili.
1. Kupitia SEAP
2. Kupitia uandikaji wa technical professional report sharti likiwa uwe umeshafanya kazi za engineering zaidi ya miaka mitatu
 
Dogo ngoja nikusaidie. Mana mi pia ni professional engineer. Kuna njia mbili.
1. Kupitia SEAP
2. Kupitia uandikaji wa technical professional report sharti likiwa uwe umeshafanya kazi za engineering zaidi ya miaka mitatu
Naomba uelezee hiyo njia ya kwanza SEAP mkuu.
 
nini tofauti ya mhandisi na mkandarasi?
Mhandisi ni Mtu ambaye ni Mtaalamu.
Mkandarasi ni Mtu ambaye ana kampuni inayoshika Kandarasi(Tender/Zabuni)! Kwa kuwa imezoeleka kuwa ni General Term kuashiria mtu aliye na Kampuni ya Ujenzi lakini kiukweli hata Kampuni ya Usafi ni Mkandarasi wa Usafi.
Sasa kwa ujumla wake Mkandarasi huwa pia ni KAMPUNI ambayo ina watu wa kuiendesha kwenye Zabuni inazoomba. Mkandarasi hivyo anaweza kuwa ni Mtu mwenye Kampuni,lakini pia kwa lugha ya kawaida iliyozoeleka mitaani ni Kampuni pia ya kazi za Ujenzi wa Miundombinu kama barabara,Majengo,Minara,mabomba ya maji,umeme,gesi nk. Wakati mwingine Mzabuni wa Supplies pia ni Mkandarasi. Msafirishaji wa Mizigo mikubwa nae hushinda Kandarasi/zabuni.

Kiswahili kimekosa maneno mahsusi kutenganisha Mtu na Kampuni.
Mkandarasi anaweza kuwa ni Mtaalam katika kazi za Kampuni au anaweza kuwa yeye ana mtaji tu na kuajiri wataalam.
 
Je nikitaka kusajili kampuni ya ukandarasi wa ujenzi wa majengo natakiwa niwe na vitu gani? Au kuna masharti gani ya kusajili kampuni ya ukandarasi ya daraja la saba?
 
Pale Katika requirements za kuwa graduate engineer ,Kuna requirement ya kusubmit certified copies of certificates and original against the copies.Swali langu ni vyeti gani vinavyohitajika ku be verified na ni Kwa njia gani(mamlaka inayohusika na Iko kitendo Cha verification).
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…