Bingwa wa mabingwa wa mbio fupi Mjamaica Usain Bolt atatakiwa kukabidhi moja ya medali zake za dhahabu alizopata Beijing Summer olympic 2008 katika mbio za kupokezana vijiti 4×100 baada ya vipimo vya mkimbiaji mwenzake Nesta Carter kuonesha mwili wake ukiwa na dawa za kupasha/kuongeza nguvu zilizozuiliwa katika mbio.
Kutokana na matokeo hayo sasa Trinidad &Tobacco ndio wamepewa nafasi ya kwanza wakifuatiwa na Japan na Brazil