isajorsergio
Platinum Member
- Apr 22, 2018
- 4,143
- 6,537
Usafiri wa anga nchini Tanzania ni usafiri ghali na wa gharama ya juu hadi kufikirisha ukilinganisha na mataifa mengine yakihusisha na safari kutoka bara moja hadi bara jingine.
Usafiri wa anga chini ya Air Tanzania kwa kiasi kikubwa ukisaidiana na Precision Air unaonekana kama umewalenga wanasiasa na wafanyabishara wakubwa.
Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Caracas, Venezuela hadi Madrid, Uhispania ni takriban $290 sawa na TZS 864,311 - hiyo ni nchi hadi nchi kwenye mabara mawili tofauti.
Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Bukoba, Tanzania hadi Dar es Salaam, Tanzania ni takriban TZS 631,000 sawa na €212 - hiyo ni mji hadi mji ndani ya nchi.
Safari ya ndege ya moja kwa moja kutoka Fort Lauderdale, USA hadi Cartagena au Barranquilla, Colombia ni takriban $69 sawa na TZS 189,000 - hiyo ni nchi hadi nchi.
Safari ya ndege ya unganisho kutoka Mbeya, Tanzania hadi Mwanza, Tanzania ni takriban 1,100,000 sawa na $403 - hiyo ni jiji hadi jiji ndani ya nchi.
Hii ni mifano midogo sana maana kuna safari za kutoka Seoul, Korea Kusini hadi Barcelona kwa TZS 1,023,000.
Swali langu ni kwanini ATCL na washirika wake ndani ya nchi wana gharama kubwa katika usafirishaji! Je wanatumia teknolojia na mifumo tofauti na ghali ukilinganisha na mataifa mengine?
Ni sababu zipi za msingi zinazofanya flights za ndani ya nchi kuwa ghali maradufu kiuhalisia na hata ukilinganisha na mataifa mengine?
Ni maelekezo kutoka juu kuendelea kuwafinya watanzania wazidi kuishi kijamaa?
JamiiForums naomba msaada wa kuwatafuta ATCL, Mamlaka ya Anga na Wizara ya Uchukuzi watupatie ufafanuzi na statistics zinazohalalisha gharama za usafiri wa anga.