USA yasema haijaidhinisha Safari ya Anasa ya Rais Rutto nchini Marekani!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
94,010
164,260
Serikali ya Marekani yasema haijaidhinisha safari ya Anasa ya Rais Rutto nchini humo

Msemaji wa Marekani mh Andrew amesema " kwa kweli Marekani haijalipia ndege ya kukodi ya Rutto kwenda Marekani "

Source Mwananchi

My take; Kumbe Ziara za Marais wetu huwa zinagharamiwa na nchi Wenyeji Chadema mpunguze uzushi 😂😂

==

Nairobi. Serikali ya Marekani imefafanua kuwa haijaidhinisha malipo ya ndege binafsi ya Rais wa Kenya, William Ruto kwenda Marekani.

Rais Ruto ameanza ziara ya kiserikali ya siku nne nchini Marekani. Aliondoka nchini Kenya Jumapili, Mei 19, 2024.

Katika mujibu wa taarifa ya leo Jumanne, Mei 21, 2024, Msemaji wa Ubalozi wa Marekani jijini Nairobi, Andrew Veveiros amesema: “Kwa kweli, Marekani haikulipia ndege ya Rais Ruto kwenda Marekani.”

Jibu hilo linafuatia habari ya kipekee iliyochapishwa na The Standard na KTN News leo, ikieleza ni kiasi kitakachowagharimu walipakodi kwa ziara ya Ruto Marekani.

Awali, gazeti la The Standard liliripoti kwamba walipa kodi watalipa gharama kubwa kwa safari ya Ruto. Ikulu imekodi ndege ya biashara ya Boeing 737-700 inayoendeshwa na kampuni ya Royal Jet ya Dubai.

Ndege hiyo ya kifahari yenye makao yake makuu Abu Dhabi, Falme za Kiarabu, inahudumia soko la anasa kati ya UAE, Ulaya na Marekani. Gharama ya kukodi ndege hii ni kubwa takriban Dola za Marekani 18,000 (Sh46.7 milioni) kwa saa.

Safari ya ndege ya kwenda njia moja kutoka Nairobi hadi Atlanta, kama ilivyonukuliwa na Royal Jet, ni sawa na dola 748,600 (Sh1.94 bilioni) kwa safari ya saa 18. Ikizingatiwa safari ya Rais Ruto kwenda na kurudi Washington (safari ya karibu ya saa mbili), gharama ya jumla inaweza kuzidi Sh4 bilioni.

Saa moja ndani ya BBJ iliyoundwa na Edese Doret inaanzia dola 12,000 (Sh31.14 milioni), hadi kufikia dola 18,000 (takriban Sh46.7 milioni).

Kumsafirisha Rais na wasaidizi wake kutoka Nairobi hadi Atlanta, Marekani kunaweza kugharimu kati ya Sh572.28 milioni (makadirio ya chini) na Sh852.5 milioni (makadirio ya juu). Gharama zinazofanana zinatumika kwa safari ya kurudi.

Ingawa kuna machaguo mengine ya kibiashara, kama vile Shirika la Ndege la Kenya (KQ), uzoefu wa Ruto kwenye BBJ bado haulinganishwi.

Wakuu wa nchi za kigeni mara nyingi hukodisha ndege za mashirika ya nchi zao wakati wa ziara za serikali pale ndege zao za rais zinapokosa uwezo unaofaa. Katika kesi hii, safari ya Ruto ni mfano wa utajiri kwa gharama ya ajabu.

Kwa hiyo, wakati safari ya siku nne ya Rais Ruto nchini Marekani inapoendelea, mlipakodi atatakiwa kulipia safari ya rais ambayo inavunja kanuni za kibiashara, safari ambayo imejaa anasa na utata.

Ruto amesafiri kwa mtindo unaoashiria ziara ya kwanza ya Rais wa Afrika nchini Marekani katika kipindi cha miaka 15.
 
Serikali ya Marekani yasema haijaidhinisha safari ya Anasa ya Rais Rutto nchini humo

Msemaji wa Marekani mh Andrew amesema " kwa kweli Marekani haijalipia ndege ya kukodi ya Rutto kwenda Marekani "

Source Mwananchi

My take; Kumbe Ziara za Marais wetu huwa zinagharamiwa na nchi Wenyeji Chadema mpunguze uzushi 😂😂
Huyu Ruto si aliwadanganya Wakenya na kujiita hustle?
 
Biden karibu kipindi chake cha miaka 4 kinaisha hajawahi kufika Africa pamoja na kuongoza taifa tajiri duniani, wa kwetu sasa utadhani wajuu wanaenda kutambika kwa babu kila mwezi, ni aibu yake kwenda kudhurura Marekani huku wananchi wake wamejaa shida.
 
Rais na mkewe wamekodi ndege hadi Wamarekani wenyewe wameogopa 😂😂
 
MEMA YA NCHI IKO DUNIAN HAYO MENGINE POROJO TU HATA NYIE MNGESHIKA MPINI MAREKAN MNGEINGIA KILA WEEKENSMD KAEN KIMYA
 
Just asking kwani Kenya hawana Katiba Mpya?
Katiba Mpya si ndio suluhisho la matatizo ya Nchi za Kiafrika according to our petty politicians?
Au bado haijaanza kufanya kazi Kenya?
 
Serikali ya Marekani yasema haijaidhinisha safari ya Anasa ya Rais Rutto nchini humo

Msemaji wa Marekani mh Andrew amesema " kwa kweli Marekani haijalipia ndege ya kukodi ya Rutto kwenda Marekani "

Source Mwananchi

My take; Kumbe Ziara za Marais wetu huwa zinagharamiwa na nchi Wenyeji Chadema mpunguze uzushi 😂😂
Acha porojo. Marekani wamejibu kelele zilizoenea Kenya kuhusu gharama za hiyo safari na tetesi za serikali ya US kugharamia ukodishaji wa ndege hiyo.

US hakuna mchezo na matumizi ya kijinga ya pesa za walipa kodi. MaRais wenu wanazifuja tu na hamna ubavu wa kuwahoji. Hakuna cha kulipiwa.
 
Umeongea kile kile cha gazetini 😀
 
Just asking kwani Kenya hawana Katiba Mpya?
Katiba Mpya si ndio suluhisho la matatizo ya Nchi za Kiafrika according to our petty politicians?
Au bado haijaanza kufanya kazi Kenya?
Unajua katiba inavyofanya kazi?

Ulimsikiliza juzi Prof Mukandala alivyozungumza kuhusu umuhimu wa katiba makini kuhusiana na tukio la kuzama kwa meli ya MV Bukoba mwaka 1996?

Unaelewa katiba ya Marekani ilivyofanya kazi kipindi Donald Trump akiwa Rais na baada ya kumaliza muhula wake wa kwanza wa miaka minne?

Sasa fuatilia yanayoendelea Kenya kuhusu habari hii ya Ruto kukodi ndege ya anasa ujue kama katiba ina umuhimu au la.
 
Hiyo katiba ya Kenya imesaidiaje kuzuia Ruto asifuje fedha za Nchi ya Kenya?
Amechukuliwa hatua gani kwa mujibu wa hiyo Katiba Mpya?
Kelele za media na wapinzani zilikuwepo tokea enzi za Moi.Kilichobadilika nini?
 
Ngoja tuone
 
Serikali ya Marekani yasema haijaidhinisha safari ya Anasa ya Rais Rutto nchini humo

Msemaji wa Marekani mh Andrew amesema " kwa kweli Marekani haijalipia ndege ya kukodi ya Rutto kwenda Marekani "

Source Mwananchi

My take; Kumbe Ziara za Marais wetu huwa zinagharamiwa na nchi Wenyeji Chadema mpunguze uzushi 😂😂
Jpm alikuwa kiongozi mzuri Sana SEMA alizidisha kidoogo ukauzu
 
Back
Top Bottom