FRANC THE GREAT
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 5,500
- 8,061
Duru zinaarifu kuwa Rais Donald Trump anapanga kurejesha kampeni zake za uchaguzi kwa kufanya mkutano wake wa kwanza panapo Juni 19 mjini Tulsa, Oklahoma.
Juni 19 ni siku inayofahamika kitaifa kama Juneteenth ambayo ni kumbukizi ya siku ya kukomeshwa kwa utumwa nchini Marekani.
Trump alitoa tangazo hilo katika kikao chake na viongozi Wamarekani weusi Jumatano alasiri katika ikulu ya White House katika mazungumzo ya pande zote na viongozi hao.
Mkutano wake huu unaopangwa kufanyika ni wa kwanza tangu ule wa mapema mwezi Machi kabla ya kuenea kwa virusi vya corona kulikopelekea zuio la mikusanyiko mikubwa.
Mji wa Tulsa jimboni Oklahoma unakumbukwa katika historia kutokana na mauaji ya kibaguzi ya mwaka 1921, ambapo kundi la watu weupe lilivamia na kuharibu makazi na vituo vya biashara vya watu weusi na kuua mamia ya wakazi weusi katika eneo hilo.
Vyanzo mbalimbali vya habari vimearifu kuwa baada ya mkutano wa Oklahoma, Trump anapanga kuzihamishia kampeni zake katika majimbo mengine ya Florida, Texas, Arizona pamoja na North Carolina hapo baadaye.
Rais Donald Trump akizungumza jambo katika kikao chake na viongozi Wamarekani weusi Jumatano ikulu ya White House Washington, DC. [PICHA: AP]