Urusi yaanza kufufua ndege zake za abiria, kukabiliana na vikwazo vya nje

Joseph_Mungure

Senior Member
Mar 6, 2021
110
167
Kwa miaka mingi usafiri wa anga wa kiraia wa Urusi umekuwa ukitegemea ndege na baadhi ya vipuli muhimu kutoka nje ya nchi kama Boeing na Airbus.

Anga ya kirusi ilijaa ndege za kigeni, zikiondoa ndege za ndani, hivyo kuzuia miradi ya ndege kama vile Tu-204/214 kuendelezwa.

Katika kipindi hiki cha vikwazo vigumu zaidi, Urusi imerudi nyuma na kuanza kufufua kile ilichokiacha ikiwemo ndege ya abiria aina ya Tupolev Tu-214.

Hii inakuwa ndege ya kwanza ya abiria inayozalishwa nchini URUSI kwa asilimia 100% pasipo kuagiza malighafi, vipuli na sehemu muhimu katika utengenezaji.

Tu-214 imepaa rasmi kwa majaribio siku ya alhamisi 21 Novemba 2024 ambapo kampuni inayoshiriki kufufua ndege hizo kwasasa ya United Air Corporation imesema, T-214 itatumika kama mbadala wa Boeing 757 iliyobereshwa.

Ndege hiyo tayari imekamilisha safari yake ya kwanza ya saa 1 dakika 10 baada ya kubadilishwa vifaa kadhaa vilivyoagizwa kutoka nje na kutumia vifaa vya kirusi.

Tu-214 ni ndege ya injini mbili bodi nyembamba inayotokana na kizazi cha Tu-204, yenye uwezo wa kubeba abiria 210 na umbali wa kilomita 6,500.

Awali Tupolev Tu-214 ilitengenezwa kwaajili ya shirika la Aeroflot kama mbadala wa Tupolev Tu-154 trijet ya masafa ya kati katika miaka ya 1990.
Baadae ikafanyiwa maboresho makubwa na kuwa Tu-204SM ambayo ilifanya safari yake ya kwanza mnamo 29 Desemba 2010 kabla ya mradi kusimishwa hadi hivi leo tena.

"Alpha Mike Tango"

Soma zaidi;
 
Back
Top Bottom