Urusi kuiuzia Iran ndege hatari za S-35!!

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,883
20,423
Kuwasili nchini Iran kwa ndege za kivita aina ya Sukhoi 35, mapema mwaka ujao

[https://media]

Mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Taifa na Sera za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) ameashiria kuwasili nchini mapema mwaka ujao wa Kiirani unaoanza Machi 21, ndege za kivita aina ya Sukhoi 35.

Sukhoi 35 ni moja ya ndege za kivita zenye uwezo mkubwa na hodari zaidi za kizazi cha 4++ duniani, ambayo ina rada ya hali ya juu ya safu ya N-035 na ina uwezo wa kugundua shabaha 30 na kupambana na shabaha 8 kwa wakati mmoja. Kasi ya ndege hiyo katika masafa ya kawaida angani ni kakilomita 1,500 kwa saa na katika masafa ya juu zaidi ni kilomita 2,500 kwa saa. Umri wa injini yake yenye nguvu kabla ya kukaguliwa na kukarabatiwa ni masaa 4,000 katika kila kipindi cha huduma.

Ndege hiyo huweza kusheheni silaha na makombora tofauti ya anga kwa anga, anga kwa ardhi na ya kulipua meli kwa wakati mmoja na wala si rahisi kuonekana kwenye rada. Aidha, ina uwezo mkubwa wa kusheheni na kurusha aina mbalimbali za mabomu na makombora ya laser, ya satelaiti na yanayosambaratisha rada.

[https://media]

Akifafanua suala hilo Shahriar Heidari, mjumbe wa Kamisheni ya Usalama wa Kitaifa na Sera za Kigeni ya Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran pia amesema kuwa Iran imeagiza mifumo ya ulinzi, makombora na helikopta kutoka Russia.

Katika miaka iliyopita, kulienea uvumi juu ya ununuzi wa ndege za kivita za Sukhoi kutoka Russiai, na wakati fulani, uvumi huo ulipata nguvu kiasi kwamba Septemba iliyopita, Brigedia Jenerali Hamid Vahedi, kamanda wa Jeshi la Anga la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, ilithibitisha habari ya ununuzi wa ndege hizo kutoka Russia akisisitiza kuwa suala hilo lilikuwa katika ajenda ya kikosi hicho cha anga.

4c10efed4ee03d27ay9_800C450.jpeg
 
Hizo Story za Iran Kuuziwa Ndege huwa zinarudi kila mara kwa kupakwa rangi nazo eee! next moth pia mtazileta upya last time mlisema hadi washajenga Hanger na zimeshahifadhiwa humo.. now mnaleta story upya za kuuziana
 
Hizo Story za Iran Kuuziwa Ndege huwa zinarudi kila mara kwa kupakwa rangi nazo eee! next moth pia mtazileta upya last time mlisema hadi washajenga Hanger na zimeshahifadhiwa humo.. now mnaleta story upya za kuuziana
Iran hataki kuuziwa ndege tu jamaa wako smart sana kichwan wao wamepewa haki ya kuzalisha na watu wapo underground huko wanazalisha maana yake kuna tech transfer iran sio kama saudi .. kuna baadh lazima wazalishe hapo
 
Back
Top Bottom