Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 18,915
- 47,696
Nchi yetu imejaa watu wanafiki, ama wanaotafuta sifa za kijinga au wanaoishi kwa hadaa. Wanaotamka 1 lakini wanamaanisha 5.
Hivi karibuni kumeibuka kelele za kinafiki toka kwa baadhi ya wanafiki kuwa mtandao wa X (zamani Twitter) ufungiwe eti unahamasisha ushoga. Ukiwauliza umehamasisha wapi, hawawezi kukuambia.
Pia soma: Waziri Nape akiri kufuatilia mijadala inayoendelea kuhusu mtandao wa X kufungiwa, asema TCRA itatimiza wajibu kuhakikisha watoto wanakuwa salama
Lakini hata kama kweli ingetokea huko kwenye mtandao wa X kukawa na mambo ya hovyo, hivi sisi kweli ni wasafi kiasi cha kuwa na uhalali wa kukemea huo uchafu?
Jamii yetu iimejaa uchafu mwingi, tena wenye madhara makubwa kupindukia, huenda kuzidi hata madhara ya ushoga. Serikali imejaa ufisadi, na taarifa za CAG zinathibitisha.
Viongozi wanawatesa wananchi maskini kununua sukari kwa bei ya mara mbili ya bei iliyokuwepo ili kuwanufaisha watawala, mbunge Mpina amethibitisha hili kwa vielelezo.
Kuna viongozi wa Serikali wana tuhuma za kuwabaka mabinti wao wa kazi, wengine wana tuhuma mpaka za kuwabaka na kuwalawiti wanavyuo. Wote hao tunao humu humu. Na wengine wanaendelea kula na kuiba kwa urefu wa kamba zao.
Watawala wanatapanya rasilimali kidogo kwa maisha ya anasa, kuzunguka na mamia ya wasanii Duniani kwa gharama ya maskini wa Tanzania. Watawala wanachezea pesa kwa kununua na kubadilisha magari ya kifahari, kwa mikopo itakayokuja kuwatesa maskini wa kesho.
Enyi wanafiki, mbona hamjashauri tuifungie Serikali kwa uovu huo wote ambao unatendeka ndani ya nchi na unawatesa mamilioni ya Watanzania wa sasa na wa kesho?
Pia soma: CCM na Serikali tuambieni ukweli, kelele za kutaka X(Twitter) ifungiwe ni maandalizi ya kuzima mitandao kipindi cha uchaguzi
Nashawishika kuamini kuwa wote wanaoshauri mtandao wa X ufungiwe, hawaumizwi na ushoga bali wanaumizwa na Watanzania wanaoikosoa Serikali na viongozi wake kwa maovu mengi kupitia mtandao huo wa X.
Kama kweli kweli wangekuwa wanaumizwa na maovu, kwanza wangeanza na maovu mengi yaliyokithiri, hasa ndani ya Serikali, na wangeomba au kushauri tuifungie hii Serikali inayoyalea maovu haya.