xfactor
JF-Expert Member
- Jan 25, 2014
- 1,511
- 1,289
Naongea haya nikiwa na masikitiko makubwa kwa serikali yangu sikivu ambayo baadhi ya viongozi wake wanalazimisha kwenda na kasi bila kujali utu na haki
Serikali inasema kuwa wakazi wa mabondeni walishapewa viwanja mabwepande lakini wamegoma kuishi kule. Leo pia nimesikia kwenye chombo kimoja cha habari waki ongelea suala hili kwa mlengo wa kwamba wakazi wa mabondeni ni wakaidi hawataki kwenda kwenye Viwanja vyao walivyo pewa.
Mimi Kama muhanga wa tukio hili naomba niwe msemaji wa upande wa pili wa suala hili maana mpaka sasa imeonekana upande wa serikali Ndio umekuwa ukisilizwa na kuaminika kwa wanayosema. Upande wa wahanga hauja sikilizwa kabisa na kujaribu kupima uhalisia.
Hapa nitaongelea mambo machache makubwa ambayo yana potoshwa
1. Wakazi wa mabondeni wamepewa viwanja mabwepande
Hili ni kweli Ila kaya chache sana zisizozidi 50 ndio zimepewa Viwanja huko. Kaya hizi zilipewa Viwanja bila kupewa fedha za ujenzi hivyo sishangai kusikia kuwa walirudi mabondeni. Bonde la mkwajuni pekee lina kadiriwa kuwa na zaidi ya kaya 300 hivyo piga hesabu ni kaya ngapi bado hazina viwanja
2. Wakazi wa mabondeni walipewa taarifa ya ubomoaji
Hili si kweli kabisa. Kilicho tokea ni kwamba manispaa ilipita Mwaka 2013 kuweka alama nyumba zote zinazo takiwa kubolewa, kuna baadhi ambazo hazikuwekewa alama hiyo hasa ambazo zilionekana zipo juu kidogo ya bonde.
Baada ya kuweka alama baadhi ya nyumba zilizowekewa alama walipewa viwanja mabwepande, nyumba hizi nyingi zipo mtaa wa suna magomeni. Manispaa iliwasiliana na serikali za mitaa na kuwataka kuwaambia wale ambao walipewa viwanja wahame na ubomoaji utaanza kwao, kwahiyo wale ambao waliwekewa alama na hawakupewa viwanja waliambiwa wasuburi, hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka huu na binafsi niliandika barua wizara ya ardhi mwaka Jana baada ya manispaa kupita kuweka alama nikajibiwa kuwa nisubiri nitapewa taarifa. Cha kushangaza tulishtukia kuona ubomoaji unaanza Tena kwa nyumba zote zilizo wekewa alama na zile ambazo hazina alama bila taarifa yoyote
3. Mabondeni ni sehemu hatarishi
Ubomoaji huu unafanywa na manispaa ya kinondoni, wizara ya ardhi na Baraza la mazingira(NEMC). NEMC Ndio walio ongeza mpaka wa ubomoaji mpaka kusababisha hadi zile ambazo hazikuwekewa alama zibomolewe bila taarifa. Swali la kujiuliza, pale jangwani kuna ofisi zinazo aminika kuwa ni za DART ambazo pia zitatumika Kama parking ya mabasi ya kwenda kasi, ofisi hizo zipo jangwani ambapo maji huwa yana jaa sasa je ofisi hizi Ndio zina haki ya kuwa kwenye sehemu hatarishi? Lakini pia kingine ni kwamba sheria ya mazingira ilikuja 2004 na haya makazi yapo toka miaka ya 70, kwa mazingira haya wakazi wanatakiwa kufidiwa maana sheria ilianza baada ya makazi kuwepo
Naomba nimalize maana kuna mengi. Wakazi wa mabondeni sio wakaidi na wala hawaja goma kuhama Ndio maana mpaka sasa hawaja andamana wala kuleta fujo. Kwahiyo vyombo vya habari na jamii isipotoshe kuwa ni wakaidi kuwa hawataki kuhama wakati wamepewa viwanja. Haya makazi yameanza kujengwa miaka zaidi ya 20 nyuma wakapelekewa umeme na maji huku serikali ikiwa inawaacha wananchi wajenge, tunalipa kodi ya jengo na tuna hati sasa iweje leo adhabu wapate wanachi lakini watendaji wa serikali walio acha watu wajenge hawa wajibishwi
Tusiwe wepesi kulaumu. Makazi ni haki ya kila mtu na ardhi ni yetu sote