Upo uwezekano wa wanafunzi kufeli mitihani ya wizara ya Afya mwaka huu

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,560
4,481
Baada ya matokeo ya mtihani wa baraza ambayo yameonesha ufaulu hafifu sana wa wahitimu wa kozi za famasia ngazi ya kati,wadau ambao ni wamiliki wa vyuo vya famasi walihoji ni kwa nini hawa wanafunzi wanafaulu mitihani ya wizara na kisha wanafeli mitihani ya baraza!

Baadhi ya viongozi wanaosimamia mafunzo katika wizara ya afya,ambao ni wafamasia,wanajipanga kuunda timu ya watu kutoka vyuo vikuu,ili wahusike kwenye kutunga mitihani ya wahitimu watarajali.
Timu hii ambayo haifundishi kwa kutumia mtaala wa nactvet,na hususan vyuo vya serikali,huwa hawaoni tatizo kufelisha wanafunzi kwa kuwa mishahara yao na posho zinalipwa na serikali.Hivyo huwa wanatinga mitihani ambayo kimsingi hata ukiirudisha uwape wao,huenda wasifaulu kwa kiwango kikubwa au wakafeli kabisa.

Iwapo itatokea wanafunzi wakafeli sana,na mkitaka kujua kuwa mitihani ni migumu,chukueni baadhi ya walimu huko huko vyuo wanaochukuliwa kutunga,wapewe moja ya mitihani iliyotakiwa kufanyika hata miaka ya nyuma.
Niko palee niite German Shepherd iwapo watatoboa.

Nashauri wasimamizi wa haya mafunzo wawe makini hujuma isijeingia ili kuthibitisha kwamba serikali inadahili watu wasio na sifa.
 
Back
Top Bottom