Sintofahamu Sekta ya Elimu
Kwa muda mrefu sasa sekata ya elimu imepita katika changamoto nyingi sana kama vile;
1. Kukosekana kwa mfumo rasmi wa viwango vya ufaulu kwa shule za sekondari. Kwa mfano alama A kwa kidato cha nne sasa inaanzia 75% hadi 100% na kidato cha sita ni 80% hadi 100%.
2. Kukosekana kwa uwiano sawa wa viwango vya ufaulu kwa vyuo vikuu. Viko vyuo ambavyo Pass mark ni asilimia 40 na vingine ni asilimia 50.
3. Kukosekana kwa uwiano wa ukokoyoaji wa GPA katika vyuo vikuu. Kuna vyuo ambavyo mwanafunzi ambavyo mwanafunzi akipata A hupewa pointi 5 hivyo kama somo hilo ni la unit au credit 3 mwanafunzi atapata alama 15 lakini kuna baadhi ya vyuo mwanafunzi akipata A ya 75% alama hizo lazima ziingizwe kwenye kanuni maalumu (formula) na bila shaka inachangia 4.4 na tofauti ya 0.6 (au 1.8 kwa somo lenye credit au unit 3) ukilinganisha na wanafunzi wa vyuo ambavyo ilimradi “A” anapewa alama 5.
4. Kukosekana kwa uwiano wa kozi zinazotolewa na vyuo mbalimbali (different course contents). Kwa mfano, somo la Accounting linaweza kutofautiana kutoka chuo kimoja hadi kingine. Swali ni “Nini hasa majukumu ya TCU?”.
Kwa upande wangu, haya mambo yananipa wasiwasi ya hatima ya elimu ya Tanzania. Yananipa shida kutofautisha Mwanafunzi aliyesoma secondary miaka ya 1990’ na wanafunzi wa miaka 2010. Pia ni vigumu kulinganisha wahitimu wa chuo kimoja na kingine kwa alama zile zile za ufaulu mwanafunzi wa chuo kimoja anawezekana kuwa juu na wa chuo kingine akawa juu.
Madhara yatokanayo na sintofahamu hii.
1. Kukosekana kwa ulinganifu wa ufaulu wa wahitimu wa sekondari kipindi kimoja na kingine kwa mifumo tofauti.
2. Mwanafunzi kunekana kuwa alifanya vizuri ingawa alifanya vibaya ukilinganisha na wanafunzi wa miaka Fulani
3. Baadhi ya wahitimu wa vyuo vikuu kuonekana kuwa wana GPA za chini au juu ukilingana na mfumo uliotumika.
4. Wahitimu wa vyuo vikuu kuwa na ufahamu tofauti kwa masomo yanayofanana kulingana na vyuo walivyosoma.
Nini kifanyike ili kupunguza au kuondoa changamoto hizo?
1. Watanzania ni muhimu tukubaliane kuwa na mfumo mmoja wa viwango vya ufaulu na madaraja ambao utakuwa wa kudumu na hautayumbisho na siasa
2. Tume ya Vyuo vikuu (TCU) ihakikishe kuwa course za aina moja zinazofundishwa na vyuo mbalimbali zifanane (course contents should be equal).
3. TCU ihakikishe pia viwango vya ufaulu kwa vyuo vya Tanzania viwe sawa kwa vyuo vyote vya Tanzania (Hasa kwa vyuo vinavyofanana kozi zinazotolewa).
4. Mfomo wa kukokotoa GPA ufanane kwa vyuo vyote vinavyotoa kozi zinazofanana. Hii itasaidia kuwa na uwiano sana kwa wahitimu pindi wanapoomba kazi, kwani hakuna mwajiri anayefuatilia mfumo uliotumika kukokotoa GPA wao wanachoangalia ni kiwango cha GPA.
Zipo Changamoto nyingi lakini nimeona vyema niongelee hizi.