BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 496
- 1,196
Ni uchunguzi wa miezi zaidi ya mitatu kwa nyakati tofauti kwenye maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam na mikoa jirani, ambapo safari yangu inakutana na Walinzi wa kampuni binafsi wakitoa kauli zenye kuashiria uwepo wa mazingira ya upigaji, utapeli na usanii.
Nini kinabainika?
Kwa siku za hivi karibuni kumekuwepo na wimbi la kampuni binafsi za ulinzi nchini Tanzania, kampuni hizo kwa mujibu wa taratibu usajiliwa chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani, kwenye Idara ya Jeshi la Polisi.
Kampuni hizo licha ya kuwa na tija kwa namna moja hama nyingine, lakini zimekuwa kati ya maeneo ambayo yamejaa utapeli kwa Wafanyakazi wengi ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu ya kiulinzi.
Katika kuzungumza na walinzi wengi wanadai kukumbana na mazingira yenye viashiria vya upigaji.
Ifahamike kwamba baadhi ya makampuni binafsi ya ulinzi yanasaini mikataba moja kwa moja na taasisi, kampuni au Mtu binafsi anayehitaji huduma ya ulinzi.
Mfano, kumekuwepo na mikataba ambayo wamiliki wa kampuni wanaingia na kampuni kuwalipa walinzi kiasi cha fedha Tsh. 700,000/=, lakini kiasi kinachomfikia mlinzi ni Tsh. 250,000/= hadi 150, 000 kwa Mwezi wengine wanapata hadi Tsh. 120,000 kulingana na wenye kampuni watakavyoamua.
Wamiliki ambao mikataba imekuwa ikiwabana mfano kuwalipa walinzi Tsh. 400,000/= kwa Mwezi, wamekuwa wakitumia mbinu ya kutengeneza makosa kwa mlinzi husika na mpaka ifikie kiwango wanachokusudia kumpa licha ya kuwasilisha nyaraka zinayoonesha mlinzi alipatiwa pesa zote.
Mmoja kati ya waliokutana na suala hili anaeleza "Mimi kwa Mwezi kampuni yangu inanilipa Tsh. 300,000 lakini ni ngumu kupata hizo hela, naishia kupata 130,000/=, wanachofanya wanakuja kwa kushtukiza wakikuta upo lindo umeweka rungu chini wanakukata 30,000 au ukitoa tu kofia kichwani wanakukata mpaka waone imefikia pesa wanayoitaka ambayo ni Tsh.180,000/= au 150,000."
Mlinzi huyo anayetekeleza jukumu lake kwenye ofisi moja iliyopo Mikocheni anadai suala hilo linawakumba walinzi wengi kwenye baadhi ya makampuni, ambapo kufuatia hali hiyo anadai amezoea mshahara wake ni Tsh. 130,000 licha ya nyaraka kuonesha anapata laki tatu.
Mazingira ya umiliki wa kampuni, tenda kwenye Ofisi za Umma
Kutokana na utaratibu wa muongozo uliopo kupata kibali cha kampuni binafsi ya ulinzi, kutoka Jeshi la Polisi imekuwa ikisababisha kampuni nyingi kumilikiwa na Wastaafu kwenye vyombo vya ulinzi na usalama au vigogo waliopo karibu na mfumo wa utawala (Serikali).
Jambo hilo linatajwa kuwa licha ya utaratibu wa wazi kuwepo lakini sio rahisi kwa Mtu mwenye sifa ambazo uainishwa katika muongozo husika kuanzisha kampuni ya ulinzi, baadhi ya vyanzo vinadai ili kufanikisha vibali stahiki uhitajika 'connection' kama kukunjua mkono.
Kutokana na mazingira hayo imekuwa ikihisiwa hicho ndicho chanzo cha makampuni mengi kutowajibika kwenye masuala mbalimbali hasa yanayogusa haki na maslahi ya Wafanyakazi kwa sababu ya ukaribu uliopo baina ya wamiliki na waliopewa dhamana ya kuwajibisha mambo yanapokuwa kinyume.
'Connection' hii imekuwa ikitumika pia katika kutoa tenda kwenye taasisi za umma bila mchakato wa kiushindani au ikitokea mchakato huo umehusika basi rushwa imekuwa nyuma ya pazia kupata tenda hizo.
Mfano zipo ofisi nyingi za Serikali hata ambazo ni nyeti kuna kampuni zimepewa tenda lakini walinzi wengi uwezo wao ni mdogo na hawana hadhi ya kuhudumu kwenye ofisi nyeti za umma.
Walinzi kadhaa wanadai mishahara sio ya kuridhisha licha ya kampuni husika kuingia mikataba inayowanufaisha zaidi wao binafsi.
Hali hii inaweza kuleta athari kubwa endapo itaendelea, ikiwemo walinzi hao kuhusika kwenye mipango uovu, mfano wizi na unyanganyi, na tayari tuhuma za aina zimekuwepo tayari ambapo baadhi ya walinzi wakiwa kwenye majukumu yao kudaiwa kujihusisha na matukio ya uovu.
'Kuna wimbi la walinzi ambao hawana weledi'
Licha ya suala la maslahi ya walinzi lakini kuna jambo lingine ambalo nimelifuatilia na kubaini sio rafiki, zamani walinzi wengi waliokuwa wanaajiriwa kwenye kampuni hizi walikuwa angalau wana A, B, C za ulinzi lakini kwa sasa makampuni mengi yanawatumia watu wengi ambao hawajapitia hata mafunzo ya Mgambo wala hawana ujuzi wa ulinzi.
Wafanyakazi wengi kutokuwa na mikataba
Nimebaini wafanyakazi wengi hawana mikataba na hili limechangia kufanikisha upigaji pia kutoa vibarua kwa Watu ambao hawana sifa.
Licha ya sekta hii kuwa nyeti kwa kugusa usalama wa raia na mali zao lakini bado wafanyakazi wengi wanafanya kazi katika mazingira magumu ambayo hayatoi matumaini yao ya kesho, ni wachache kati ya wengi ambao wanawekewa pesa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
Kwenye hili uchunguzi zaidi unahitajika
Inasemekana kutokana na kuaminika kwa kiwango fulani kwa Kampuni ya ulinzi ya Suma-JKT ikilinganishwa na kampuni nyingi hasa za ndani, inaelezwa kumekuwepo na Suma-JKT kivuli ndani ya Suma-JKT halisi.
Ni kwamba kuna watu wamekuwa wakipewa tenda kama Suma-JKT licha ya kuwa ni kampuni nyingine, jambo hilo limedaiwa kuwa ni ngumu kubainika kwa sababu hata walinzi upewa sare zinazofanania na Suma-JKT halisi.
Jambo hilo linaacha maswali lakini ni vyema nilifikishe hapa jukwaani ili wahusika walifanyie kazi zaidi maana nimekosa muda wa kulichunguza kwa kwa kina.
Baadhi ya makampuni yakipata tenda wahuka (wahitaji) wakahitaji huduma ya ulinzi wa Suma-JKT dili halikwami badala yake mazingira yanatengezwa kufanikisha mchongo kwa kutumia Suma-JKT kivuli.
Nashauri nini?
Miezi kadhaa iliyopita niliona Tume ya Haki za Binadamu na Utawala bora wametoa taarifa ya kufanya uchunguzi kuhusu madai ya ukiukwaji wa haki za walinzi kwenye kampuni binafsi, lakini mpaka sasa sijasikia ripoti ya uchunguzi wao ikitolewa hadharani au kwenye vyombo vya habari, sijui labda wenzangu mmesikia?
Ni vyema muongozo wa kuanzisha kampuni binafsi ukaboreshwa ili kuepuka mazingira sawa katika kuanzisha kampuni hizo, lakini pia kufanya tathimini ya kampuni zilizopo mpaka sasa kubaini kama zinatimiza mashariti ya taratibu za kumungozo.
Zoezi la tathimini hiyo suala la maslahi kwa wafanyakazi lipewe kipaumbele pamoja na wimbi la kuongezeka kwa kampuni hizo pia uweledi wa walinzi kulingana sifa husika.
================

Lilivyokuwa andiko la Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora