Umeleta mada nzuri ila umeshindwa kuijazia wigo sahihi ili wachangiaji wakupe jibu mujarabu. Hebu tafakari katika nyigo hizi ya kwako ipo eneo gani
1a- Ni muda gani sahihi wa kupata mwenza baada ya kufiwa na mume/mke?
1b - Ni muda gani sahihi wa kupata mwenza baada ya kuachana/kutalikiana na mke au mume?
2- Ni muda gani sahihi wa kuwa na mwenza baada ya kuachana na mchumba tuliyekuwa tukielekea kwenye ndoa?
3- Ni muda gani sahihi wa kuwa na mwenza baada ya kuachana na by/girlfriend?
4- Ni muda gani wa kuwa na mwenza baada ya kuachana na mlupo/one-night stand?
Kwa nyigo hizo hapo juu nadhani majibu yatakuwa tofauti ukianzia na sababu ya kuachana, muda wa mahusiano yenu kabla ya kuachana na mwisho malengo ya mahusiano yenu kabla ya kuachana.
katika hio window period unakuwa na wasaa mzuri wakuji assess kipi ulikosea ama ulikosa na unataka mtu wa aina gani katika utulivu wa hali ya juu, pia inakujengea ukomavu zaidi katika kuhimili ile mikiki ya kuachana. Naamini ndani ya mwaka moyo wako utakuwa umeshapona na kusahau baada ya maumivu makali ikiwa mlipendana sana ila ilitokea tu all of a sudden mmoja kati yenu kuamua ku breakup.sababu ni zipi?
1yr madonda, majeraha yatakuw yameisha iman mbaya juu ya jinsia ingne itakuw imeshatoweka,,,,,, ila inategemea mtu na mtu ndo maana vidole vya mkonon havilingani.
Umetisha mkuu!!dk35 tu zinatosha..
safi sana kwa kucheka, wewe binafsi inakuchukua muda gani?yaani tumecheka (sio mimi pekee hata nilionao hapa)