Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,209
- 4,406
KISULISULI.
Mwashinda bure maombi,mkiyapiga magoti
Hamjui Kuna dhambi,kubwa ya kuomba noti
Kutwa mnaweka kambi,mje mmiliki boti
Pepo za kisulisuli,zilivuma zikaganda.
Watu mnaombwa namba,kutoa mwaringa ringa
Ili kupiga msamba,kwanza jifanye mjinga
Sikio litoe pamba,kubali dona na yanga
Pepo za kisulisuli,hazitokupita mbali.
Bado mwachagua sana,nataka awe mrefu
Kifua kilicho tuna,shoga zangu wanisifu
Mwenye nanilii pana, mwenye ya mbwa mapafu
Pepo za kisulisuli,kwa hivyo haziji kamwe.
Mtaogea magadi,na bado mgonge mwamba
Mwajifanya wakaidi,kwa urembo mnatamba
Hamjui kuna radi,inayosomesha namba
Pepo za kisulisuli,zinazikwa na matendo
Unataka wenye pesa,wachache tena adimu
Ni bahati kuwapata,kuwanasa ni vigumu
Ila tulochoka hasa,ni kubwa yetu sehemu
Pepo za kisulisuli,haziletwi kwa mafuta.
Zaituni na upako,hata ipakwe mwilini
Utabaki peke yako,wenzio wavutwa ndani
Ukiisha muda wako,tukutane kanisani
Pepo za kisulisuli,zina masharti magumu.
Ukikitoa mapema,unazidi kuharibu
Sidhani ndo jambo jema,wala siyo taratibu
Tukikula tunatema,kipya tuna kihesabu
Pepo za kisulisuli,zilikwepo Kwa mabibi.
Wao sana walibana,hawakuwa burebure
Wa sasa mwajua chana,mwajaa viherehere
Hamuwezi tulizana,mwaipenda saresare
Pepo za kisulisuli,huko ni kuliwa pesa.
Walishasema mitume,kitu gani cha kufanya
Kuacha upaka shume,na siyo kujichanganya
Mkituacha tuchume,mengi tutawadanganga
Pepo za kisulisuli,kama kivuli na mwanga.
Muda wako ukifika,punde hivi utaisha
Vilo wima vikishuka,ni vigumu kuviwasha
Tena hutotazamika,utakua kama kasha
Pepo za kisulisuli,hazivumi na ujana.
Unaoisha mapema,wapya wanapozaliwa
Jiepushe kuachama,mbona utachaguliwa
Usiwe hovyo kusema,ni wazi utakimbiwa
Pepo za kisulisuli,huandamwa na bahati.
SHAIRI-KISULISULI
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Mwashinda bure maombi,mkiyapiga magoti
Hamjui Kuna dhambi,kubwa ya kuomba noti
Kutwa mnaweka kambi,mje mmiliki boti
Pepo za kisulisuli,zilivuma zikaganda.
Watu mnaombwa namba,kutoa mwaringa ringa
Ili kupiga msamba,kwanza jifanye mjinga
Sikio litoe pamba,kubali dona na yanga
Pepo za kisulisuli,hazitokupita mbali.
Bado mwachagua sana,nataka awe mrefu
Kifua kilicho tuna,shoga zangu wanisifu
Mwenye nanilii pana, mwenye ya mbwa mapafu
Pepo za kisulisuli,kwa hivyo haziji kamwe.
Mtaogea magadi,na bado mgonge mwamba
Mwajifanya wakaidi,kwa urembo mnatamba
Hamjui kuna radi,inayosomesha namba
Pepo za kisulisuli,zinazikwa na matendo
Unataka wenye pesa,wachache tena adimu
Ni bahati kuwapata,kuwanasa ni vigumu
Ila tulochoka hasa,ni kubwa yetu sehemu
Pepo za kisulisuli,haziletwi kwa mafuta.
Zaituni na upako,hata ipakwe mwilini
Utabaki peke yako,wenzio wavutwa ndani
Ukiisha muda wako,tukutane kanisani
Pepo za kisulisuli,zina masharti magumu.
Ukikitoa mapema,unazidi kuharibu
Sidhani ndo jambo jema,wala siyo taratibu
Tukikula tunatema,kipya tuna kihesabu
Pepo za kisulisuli,zilikwepo Kwa mabibi.
Wao sana walibana,hawakuwa burebure
Wa sasa mwajua chana,mwajaa viherehere
Hamuwezi tulizana,mwaipenda saresare
Pepo za kisulisuli,huko ni kuliwa pesa.
Walishasema mitume,kitu gani cha kufanya
Kuacha upaka shume,na siyo kujichanganya
Mkituacha tuchume,mengi tutawadanganga
Pepo za kisulisuli,kama kivuli na mwanga.
Muda wako ukifika,punde hivi utaisha
Vilo wima vikishuka,ni vigumu kuviwasha
Tena hutotazamika,utakua kama kasha
Pepo za kisulisuli,hazivumi na ujana.
Unaoisha mapema,wapya wanapozaliwa
Jiepushe kuachama,mbona utachaguliwa
Usiwe hovyo kusema,ni wazi utakimbiwa
Pepo za kisulisuli,huandamwa na bahati.
SHAIRI-KISULISULI
MTUNZI-Idd Ninga,Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com