Updates za Paris Motor Show 2024 (Tarehe 14 - 20 October)

Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
25,843
74,243
Paris Motor Show ni moja ya maonyesho makongwe ya magari (tokea mwaka 1898) yanayofanyika kila baada ya miaka miwili, ambapo makampuni mbalimbali ya magari yanaonesha magari yao mapya, concepts, teknolojia na vitu vingine vinavyohusiana na magari.
IMG_0440.jpeg

Kwa mwaka 2024, zaidi ya makampuni ya magari 40 kutoka duniani yatakuwepo kuonesha magari yao.
IMG_0441.jpeg

Mbali na makampuni, kutakua na magari mengine maarufu yaliyotumika katika movies mbalimbali maarufu kama vile Batmobile (ya Batman), Aston Martin DBS (ya Casino Royalle James Bond), na DeLorean ya Back from the Future.
IMG_0438.jpeg
IMG_0439.jpeg

Tutegemee kuona magari mapya, kuona teknolojia mpya, restyling (updates) na concepts mbalimbali.
IMG_0443.jpeg

Tutajitahidi kutoa updates kadri tuwezavyo hapa lengo kujifunza na kua inspired.

Karibuni.
 
Citroën Ami EV

ampuni ya magari kutoka Ufaransa Citroën wamezindua gari lao jipya Citoën Ami EV.
IMG_0480.jpeg

Ni kadude kadogo, kenye electric motor ya 8hp na ukichaji kanakupeleka kilometa 70 tu, Kwahiyo kwa kuzingatia size yake na power kanafaa kwa mizunguko ya mjini.
IMG_0481.jpeg

Kuanzia 2025 itaanza kua sokoni na utaweza kuipata kwa £8,000 tu.
IMG_0482.jpeg

Kwa hii garama unapata gari zuri zaidi kutoka China BYD lenye range hadi ya kilometa 300+
 
Citroën C5 Aircross
Bado Citroen wakiendelea na presentation wamezindua pia concept car ya C5 Aircross.
IMG_0483.jpeg

Hii inakuja na PHEV na full EV, ingawa hawajaziongelea zaidi specifications zake.
IMG_0485.jpeg

Hii SUV itaenda kujiunga na familia ya C3 na C4 kutoka kwa Citroën.
 
Renault 4 Retro

Kama unaikumbuka Renault 4 ilioachwa kuuzwa 1994, sasa imekuja. Ikiwa in EV mode.
IMG_0486.jpeg

Kwa range ya 300 hadi 400 kilometa kutegemea battery utakalochagua, ambazo ni 40 kWh au 52 kWh.
IMG_0487.jpeg

Betri za Retro 4 unaweza ukazichaji kwa DC fast charging ya 100 kW so inachukua dk 30 kutoka 15 hadi 80%. Faster kuliko simu yako (natania)! Kama haitoshi R4 inaweza geuzwa P2L ikawa energy source umeme ukikatika.
IMG_0488.jpeg

Itaanza kuuzwa mwakani, ingawa issue ya pricing haijaongelewa.
 
Naona magari ya umeme yanashika kasi kuliko kawaida ndani ya miaka 50 ijayo ukiwa na gari ya petrol au disel watu warakuwa wanakushangaa tu kuwa una gar ya mizigo
 
Naona magari ya umeme yanashika kasi kuliko kawaida ndani ya miaka 50 ijayo ukiwa na gari ya petrol au disel watu warakuwa wanakushangaa tu kuwa una gar ya mizigo
Mingi sana 50, mi naamini ndani ya miaka 10 tu ijayo ni mwendo wa EV
 
Alpine Motors (wale wale wa Formula 1) wana jambo lao.
IMG_0489.jpeg

Kutana na SUV Alpine A390, muundo wa ajabu na ina sport mode ambayo rear wing (spoiler) yake inaweza kupanda na kushuka hadi cm 80, na seat zake zinaweza kuchange na kua kama za F1.
IMG_0491.jpeg
IMG_0490.jpeg

Ooh pia wametuletea gari zao za F1 tusizoruhusiwa kuziendesha.
IMG_0492.jpeg
 
LeapMotors wamezindua B10 EV

Kutoka China, LeapMotors wamezindua EV yao SUV B10.
IMG_0502.jpeg

Ingawa hawajasema zaidi kuhusu specifications zake, ila tunaamini itafanana na Model yao ya C10 walioizindua recently.
IMG_0501.jpeg
Bei pia haijaongelewa ila tunaamini itakua below $30,000
 
Alpine Alpenglow Hy6.
Hii ni Hydrogen powered hypercar, ingawa bado ipo kwenye concept.
IMG_0505.jpeg
IMG_0504.jpeg
IMG_0503.jpeg
 
Skoda Elroq EV
Kwa range hadi ya 560 km unaipata kwa bei ya $36,000 tu.
IMG_0506.jpeg
IMG_0507.jpeg
IMG_0508.jpeg
IMG_0509.jpeg

Inakuja na battery options tatu, kuanzia 55 kWh, 63 kWh na 82 kWh.
 
Audi Q6 & Q6 Sportback e-tron
Audi wamezindua Q6 e-tron ambazo ni EV.
IMG_0517.jpeg

Q6 inakuja na peak power ya 456 hp, na top speed ya 210 km/h tu wakati Q6 Sportback inafika 230 km/h na power ya 509 hp.
IMG_0518.jpeg

Zinakuja na dual electric motors, battery la 95 kWh na inaweza kukufikisha kilometa 450 ikiwa full charge.
IMG_0519.jpeg

Ila ni expensive, angalau $100,000 tu.
 
Back
Top Bottom