Update ya dawa za kulevya zilizokamatwa mbali na msokoto mmoja wa bangi

Mtarban

JF-Expert Member
Jan 14, 2015
3,846
5,057
Leo swali langu ni fupi kihivyo. naomba nielezwe ni kilo ngapi za unga zilizokamatwa tangy inayoitwa operation ya madawa ya kulevya ianze.

pia naomba nitajiwe aliyekamatwa na mzigo Wa dawa hizo, tofauti na msokoto mmoja wa bangi unaosemekana ulikutwa kwa Wema Sepetu

teh teh teh, nchi yenu Tanzania ina mambo ya kufurahisha sana. unaanzisha vita ya kupambana na dawa za kulevya unaishia kuchafua watu na kukamata msokoto mmoja tu Wa bangi!
 
Acha kuvuta vitu haramu ndio utaelewa.
 
Hivi msokoto si kama ule tu wavutaji wanaouweka mdomoni na kuuvuta? Kama ndiyo huo basi hata mimi naweza kuwa shujaa within a minutes? Bilaa kuchafua mtu!bila kuvutana na mtu! Na bila kuwa hata balozi wa nyumba kumi achilia mbali kuwa Rc!!
 
Acha kuvuta vitu haramu ndio utaelewa.
Hamna waliyokamata, otherwise tungeambiwa na sidhani kama kuna mtu atamkuta na mzigo kwa jinsi muda unavyotolewa kujipanga. Ninavyojua hearsay bila evidence ni bure mahakamani.
 
wanatusaulisha machungu ya mfumuko wa bei ya vyakula na na hali tte ya uchumi tulio nao nshawastikia.
Nashangaa mkuu...juzi tu ishu ilikuwa ni Njaa....lakini leo njaa hakuna ila kuna habari zilizopo...zikiisha hizi utasikia ishu nyingine...
 
Timetoka kwenye njaa sasa tuna shibe na kufurahia madawa ya kulevya...heko wadanganyika mbele kwa mbele, naomba na shule zote za dsm zilizoshika mkia mitahani isahishe upya haiwezekani watakuwa wametufelisha
 
Katika episode za Makonda ambazo nisingependa kuona zikiisha haraka, hii ya unga hii, acha iendelee.
binafsi naisapoti sana vita hii lakini huyu jamaa hawezi kuwa na hatakuwa kamanda wa kutuongoza katika mapambano. never. alifeli tangu episode 1 alipokuwa anaongea na media huku ametia mikono mfukoni.

ufilipino vita inaongozwa na Rais. tunaweza kufanya hivyo hapa au japo tukamtumia Waziri, lakini siyo huyu jamaa ambae muda wote anawaza kwa kutumia akili za kijani.
 
Tena msokoto wenyewe wameenda nao polisi kutoaibika. Yaani nchi hii viongozi wake sijui wanaishi sengerema wote
 
Mkuu kuna kataarifa kanazunguka mitandaoni kutoka kenya, kamemtaja waziri wetu kuwa nae anahusika, huoni kuna kila sababu ya Makonda kukomaa kivyake vyake mpaka kieleweke?
 
Mkuu kuna kataarifa kanazunguka mitandaoni kutoka kenya, kamemtaja waziri wetu kuwa nae anahusika, huoni kuna kila sababu ya Makonda kukomaa kivyake vyake mpaka kieleweke?
Waziri yupi tena au bumbuli trans
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…