UPANDISHWAJI MADARAJA UMEGUBIKWA NA UKIUKWAJI MKUBWA WA HAKI ZA WALIMU.

Katali

JF-Expert Member
Nov 2, 2016
859
694
Ninasikitika kuona Chama chetu kinashindwa kusimamia haki za upandishwaji madaraja kwa walimu kwa kufuata haki.

Waliopewa dhamana ya kusimamia upandisha madaraja sijui ni kwa maksudi au bahati mbaya wanapo tenga makundi na kukataa kupandisha daraja kwa kigezo cha kwamba waliohamia kuanzia 2017/18 hawastahiri kupandishwa katika vituo vya kazi walivyo hamia eti warudi walikokuwa awali ili huko ndiyo wawarekebishie au kuwapandisha madaraja!!hii ni hoja ya kibaguzi na inanikosesha kwa mara nyingine kupandishwa daraja baada ya awali kutoa sababu kwamba jina langu halikutokea miongoni mwa walimu niliomaliza nao sasa wenzangu wanapanda mara ya tatu mimi bado nikiwa daraja lilelile la awali.Kiukweli Mungu anawaona na muomba anilipie kwa hili kwa kiwango hiki wanachonifanyia.

Serikali ina adhima njema kabisa sijui hawa watendaji wanatoa wapi masharti yenye kuumiza kwa kiwango hiki ? Sielewi niende wapi pamoja na jitihada zangu mbalimbali lkn leo nimekutana na ukuta.

Ombi mtumishi anapohama isiwe kigezo cha haribu maisha yake kwani kuanzia mchakato wa kuhama,kuhamisha mshahara,na haki mbalimbali za kiutumishi inakuwa shida si vibaya serikali viongozi wa vyama mbalimbali wakatolea macho kadhia hizi ili kulinda ustawi wa watumishi wa umma na kuwafanya watumikie nchi kwa morale na kuleta ufanisi katika kujenga taifa letu.
 
Mtu unajikuta unajuta.
Mimi niliajiriwa mwaka 2012 kwa bahati mbaya 2016 sikupanda daraja.

Mwaka 2017 nikaomba ruhusa ya masomoni nikapewa na kujiunga na chuo kikuu ili kuongeza Shahada ya pili.

Nimeambiwa sitakiwi/sina sifa za kupanda daraja kwasababu nipo masomoni.

Sasa hapo jiulize nina miaka nane kazini ni miaka miwili tu ndio nimetumia kuwa masomoni lakini naambiwa sina sifa za kupanda daraja.
 
Pole sana, nenda Dom utumishi upeleke kero yako, huko watakusaidia .
 
Jiwe alishasema juz mei mosi ni hadi akaribie kuondoka madarakan ndy atageuza jicho lake kuelekea huko unakosema.
 
Mtu unajikuta unajuta.
Mimi niliajiriwa mwaka 2012 kwa bahati mbaya 2016 sikupanda daraja.

Mwaka 2017 nikaomba ruhusa ya masomoni nikapewa na kujiunga na chuo kikuu ili kuongeza Shahada ya pili.

Nimeambiwa sitakiwi/sina sifa za kupanda daraja kwasababu nipo masomoni.

Sasa hapo jiulize nina miaka nane kazini ni miaka miwili tu ndio nimetumia kuwa masomoni lakini naambiwa sina sifa za kupanda daraja.
Ndio utaratibu. Kati ya vigezo vingine vingi..... Ukiwa masomoni umekosa sifa. Ndio taratibu wasiliana na HR wako kwa walaka rasmi
 
Soma vizuri,nilitakiwa kupanda 2015/16 masomoni nipo sasahivi na nilitakiwa kupanda mara ya pili ila sijawahi kupanda hata mara moja.
Ndio utaratibu. Kati ya vigezo vingine vingi..... Ukiwa masomoni umekosa sifa. Ndio taratibu wasiliana na HR wako kwa walaka rasmi
 
Ninasikitika kuona Chama chetu kinashindwa kusimamia haki za upandishwaji madaraja kwa walimu kwa kufuata haki.

Waliopewa dhamana ya kusimamia upandisha madaraja sijui ni kwa maksudi au bahati mbaya wanapo tenga makundi na kukataa kupandisha daraja kwa kigezo cha kwamba waliohamia kuanzia 2017/18 hawastahiri kupandishwa katika vituo vya kazi walivyo hamia eti warudi walikokuwa awali ili huko ndiyo wawarekebishie au kuwapandisha madaraja!!hii ni hoja ya kibaguzi na inanikosesha kwa mara nyingine kupandishwa daraja baada ya awali kutoa sababu kwamba jina langu halikutokea miongoni mwa walimu niliomaliza nao sasa wenzangu wanapanda mara ya tatu mimi bado nikiwa daraja lilelile la awali.Kiukweli Mungu anawaona na muomba anilipie kwa hili kwa kiwango hiki wanachonifanyia.

Serikali ina adhima njema kabisa sijui hawa watendaji wanatoa wapi masharti yenye kuumiza kwa kiwango hiki ? Sielewi niende wapi pamoja na jitihada zangu mbalimbali lkn leo nimekutana na ukuta.

Ombi mtumishi anapohama isiwe kigezo cha haribu maisha yake kwani kuanzia mchakato wa kuhama,kuhamisha mshahara,na haki mbalimbali za kiutumishi inakuwa shida si vibaya serikali viongozi wa vyama mbalimbali wakatolea macho kadhia hizi ili kulinda ustawi wa watumishi wa umma na kuwafanya watumikie nchi kwa morale na kuleta ufanisi katika kujenga taifa letu.
Sasa kama haumo kwenye ikama ya mwajiri mpya utapandaje?? Kibali cha kupandisha madaraja kinakuja na idadi maalum ya watu ambao wametengewa bajeti.

Wakati mwajiri anaandaa bajeti ya kuwapandisha watumishi madaraja wewe ulikuwa hujahamia hapo bado hivyo huwezi kuwemo kwenye waliotengewa pesa za promotion.

Atakupandishaje bila kukutengea pesa za mshahara mpya?? Itabidi usubiri tu mpaka kibali kingine kikitoka cha promo

Rudi kule ulikokuwepo awali ili kama walikuweka kwenye bajeti wajue wanakusaidiaje!
 
Soma vizuri,nilitakiwa kupanda 2015/16 masomoni nipo sasahivi na nilitakiwa kupanda mara ya pili ila sijawahi kupanda hata mara moja.
Upande 15/16 kivipi na umeajiriwa 2012? Madaraja nadhani wanapandisha baada ya kukaa zaidi ya miaka mi 3 katika cheo kimoja tena baada ya kujiridhisha na utendaji kazi wako.watumishi was serikali mmezoea kupandishwa hovyo bila kuzingatia ufanisi wa majukumu yenu makazini. Watoto wanafeli kila siku kwenye shule za serikali mnataka mpabdishwe madaraja kwa kazi gani hasa ya muhimu mliyofanya. Mimi ningekua rais ningezuia kabisa
 
Naunga mkono hoja yako,tumuunge mkono Magufuli na mambo yake yote.

Acha ubishi bhana.
Mi mwenyewe niliajiriwa 2012 nikapanda daraja 2015.
Kuna ujinga huwa unafanyika halmashauri.
 
Huyo jamaa Waterloo nilikuwa namkubali sana hapa Jf ila ameandika uharo.
Hajui tangu 2012 hadi sasa ni mwaka wa nane.

Sasa mtu nipo masomoni miaka miwili na mwezi wa nane narudi kazini.

Sijawahi kupanda daraja hata mara moja wakati wengine wanapanda mara ya pili.
Kwa kifupi ameandika kama hana akili timamu.
Acha ubishi bhana.
Mi mwenyewe niliajiriwa 2012 nikapanda daraja 2015.
Kuna ujinga huwa unafanyika halmashauri.
 
Kinachowasumbus watu na kuwatoa ufahamu ni unafiki na ubinafsi.
Unasoma comment ya mtu hadi unashindwa kushangaa.

Ila kwa sasa nasikia kupanda daraja ni 4 yrs baada ya kuipitia OPRASS.

Wewe ulistahili kupanda daraja kabla ya kwenda masomoni.
Kwa hiyo ulienda masomoni ukiwa na haki ya kupanda daraja. Ungekuwa uliondoka kituoni baada ya miaka miwili ingekuwa sawa.
 
Upande 15/16 kivipi na umeajiriwa 2012? Madaraja nadhani wanapandisha baada ya kukaa zaidi ya miaka mi 3 katika cheo kimoja tena baada ya kujiridhisha na utendaji kazi wako.watumishi was serikali mmezoea kupandishwa hovyo bila kuzingatia ufanisi wa majukumu yenu makazini. Watoto wanafeli kila siku kwenye shule za serikali mnataka mpabdishwe madaraja kwa kazi gani hasa ya muhimu mliyofanya. Mimi ningekua rais ningezuia kabisa
Mkuu unakosea, kufeli kwa wanafunzi hakutokani na walimu tu, pia kuna mambo mengine yanayochangia. Maslahi madogo kwa walimu na kukosekana kwa motisha kwa walimu huondoa morali ya utendaji kazi.
 
*NJIA ZA KUMFANYA WANAFUNZI WALIPENDE NA KULIFAULU SOMO LAKO*

✓Wambie kwamba hakuna mwanafunzi atakaefeli somo lako.

✓Wahakikishie kwamba somo lako ni somo zuri na rahisi sana kufaulu.

✓Wambie wanafunzi wako wanaofaulu kwa kiwango cha juu somo hili si watu maalum na walioteuliwa, hata wewe unaweza kufaulu ukijituma.

✓Unapoingia darasani kuwa na mwonekano mzuri kwani utafiti unaonesha kwamba wanafunzi hupendelea walimu wanaoonekana smart hivyo huwa makini kuwasikiliza.

✓Usikunje sura muda wote unapokuwa darasani onesha tabasamu kwao nao wacheke (inawapunguzia msongo)
Usiwakaripie wanafunzi/mwanafunzi mbele ya wenzao/mwenzao wakiwa darasani au nje ya darasa zungumza nao kwa upole watambue makosa yao. (ukiwa na hasira jizuie kuzungumza na wanafunzi)

✓Wape motisha kila wanapofaulu somo lako sio lazima inayoonekana (Tangible) bali hata zitakazowafanya wajisikie vyema kama kuwasifu mbele ya wenzao wa madarasa mengine, kuwaandika kwenye mbao za matangazo za shule kama ni wanafunzi waliofanya vizuri (hili la kuwaandika kwenye mbao liwe kwa mitihani ya muhula au ya mwaka)

✓Wambie wanafunzi wako unalipenda sana darasa lao na wao unawapenda. Ishia hapo usiendelee kusema kuliko darasa Fulani inaweza kukujengea chuki na darasaa jengine kwani watapata taarifa hizo.

✓Usiwape adhabu kwa wanaokosea na kukosa alama katika somo lako, hii itapelekea wengi kuzifanya na kutambua makosa yao (waazibu wasiofanya kazi zako)
Usiwalaumu mbele ya wanafunzi wenzao waliokosa badala yake waambie mnaweza kuwapita waliofanya vizuri leo.

✓Waambie wanafunzi wako watafute mambo yanayowafanya wafeli somo lako na wakwambie ili uwasaidie.

✓Cheza gem nje ya uwanja, unapokutana na wanafunzi wako nje da darasa zungumza nao kwa utani ili kuwapunguzia masafa(distance) baina yako na wao, utani uwe ni wa kawaida wasijiulize kitakachofuata baada ya utani wako ni kipi?(baadhi yao watakuogopa).

✓Unapowapa kazi za majaribio hakikisha unafanya masahihisho na kuwaonesha makosa yao (wanafunzi wenye alama za chini sana wafanyie individual correction na kuwaeleza wanavyopaswa kufanya badala ya walivyofanya).

✓Kwa maswali magumu kujibu onesha mfano wa kujibu na uwapatie wanafunzi wako waone yanavyojibiwa.

*UKIFANYA HAYA TARAJIA KUPATA MATOKEO* *CHANYA KWENYE SOMO LAKO*
*ASANTE MWALIMU JITAHIDI UTASHINDA*

*WALIMU HOYEEE*
 
Ninasikitika kuona Chama chetu kinashindwa kusimamia haki za upandishwaji madaraja kwa walimu kwa kufuata haki.

Waliopewa dhamana ya kusimamia upandisha madaraja sijui ni kwa maksudi au bahati mbaya wanapo tenga makundi na kukataa kupandisha daraja kwa kigezo cha kwamba waliohamia kuanzia 2017/18 hawastahiri kupandishwa katika vituo vya kazi walivyo hamia eti warudi walikokuwa awali ili huko ndiyo wawarekebishie au kuwapandisha madaraja!!hii ni hoja ya kibaguzi na inanikosesha kwa mara nyingine kupandishwa daraja baada ya awali kutoa sababu kwamba jina langu halikutokea miongoni mwa walimu niliomaliza nao sasa wenzangu wanapanda mara ya tatu mimi bado nikiwa daraja lilelile la awali.Kiukweli Mungu anawaona na muomba anilipie kwa hili kwa kiwango hiki wanachonifanyia.

Serikali ina adhima njema kabisa sijui hawa watendaji wanatoa wapi masharti yenye kuumiza kwa kiwango hiki ? Sielewi niende wapi pamoja na jitihada zangu mbalimbali lkn leo nimekutana na ukuta.

Ombi mtumishi anapohama isiwe kigezo cha haribu maisha yake kwani kuanzia mchakato wa kuhama,kuhamisha mshahara,na haki mbalimbali za kiutumishi inakuwa shida si vibaya serikali viongozi wa vyama mbalimbali wakatolea macho kadhia hizi ili kulinda ustawi wa watumishi wa umma na kuwafanya watumikie nchi kwa morale na kuleta ufanisi katika kujenga taifa letu.
Wewe ulionewa, ulistahili kupanda daraja 2016,na hadi unaenda masomo bado ulikuwa unayo haki ya kupanda daraja.
 
Back
Top Bottom