KERO Uongozi wa Mkoa wa Mbeya unaendelea kudhibiti Kipindupindu lakini Wakazi wa Isyesye hatuna Huduma ya Maji kwa wiki sasa, hii inarudisha nyuma juhudi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

KwetuKwanza

Member
Mar 13, 2023
74
133
Hadi leo Januari 21, 2025, maeneo ya Isyesye hapa Jijini Mbeya haujapata maji kwa wiki moja sasa, tumetoa taarifa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mbeya (MBEYA UWSA) lakini hatuoaji majibu yanayoeleweka.

Hii sio mara ya kwanza, kila inapotokea kunakuwa na ugumu kwa kupata majibu kutoka kwa mamlaka hiyo inayohusika, sijajua tatizo ni nini lakini wanatakiwa kujirekebisha.

Kama kuna changamoto ya mabomba yaliyopasuka basi wangeweza kuwa na mkakati wa kuyashughulikia kuliko kama hivi Wananchi tunalazimika kutumia maji ya kwenye kisima na kuingia ghara ya kununua maji ya kunywa.
photo_2025-01-21_09-25-08.jpg

photo_2025-01-21_09-25-07.jpg
Wakati huu ambapo Wizara ya Afya na Serikali ya Mkoa wanapambana na hali ya maambukizi ya Kipindupindu lakini MBEYAUWSA inakwama kutoa huduma ya maji kwa muda wa wiki nzima, hapo tunategemea nii kitokee?

Kuna nyumba za wageni zimefungwa sababu ya kukosa huduma ya maji.

Isyesye viwanja vipya ni mji wenye nyumba za kisasa, hakuna vyoo vya shimo. Serikali inawezaje kupambana na kipindupindu wakati watu hawana maji?

Majibu ya Mamlaka, soma hapa ~ Mkurugenzi Mamlaka ya Maji Mbeya: Maji tunayozalisha ni 58% ya mahitaji yanayotakiwa kwa siku
 
Solution ya Maji Mbeya ni kuvuta maji kutoka Rungwe tu au kuchimba visima maeneo salama mji upate maji ya kutosha
 
Back
Top Bottom