Uongozi wa Manispaa Moshi watoa ufafanuzi wa madai ya jengo la soko kugharimu bilioni 2, wasema ni bilioni 1.5 awamu ya 2 inaendelea!

Cute Wife

JF-Expert Member
Nov 17, 2023
1,961
5,082
Wakuu,

Mdau humu alihoji bilioni mbili zimetumikaje kwenye soko ambalo limejaa bati tu na vijumba vi fremu vya mchongo? Jamaa wamekuja na ufafanuzi, kuwa bilioni 1.5 ndio zimetumika kwenye ujenzi wa soko hilo na milioni 500 ndio zinamalizia awamu ya 2.

Hii inamaanisha watakuwa washatumia kama 1.8 hivi, ila hata kama tukisema ni bilioni 1.5, kwa macho tu bilioni 500 ndio imejenga hilo soko Wakuu? Hakika mama ametenda na anatosha :PeepoRunCry::PeepoRunCry::PeepoRunCry:

1742396699304.png

=====

Kutokana na uwepo wa taarifa za upotoshaji kuhusu gharama za ujenzi wa soko la Mbuyuni lililopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Uongozi wa Manispaa hiyo leo Mach 19, 2025 imetoa ufafanuzi.

Akitoa taarifa ya ufafanuzi huo, Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Uhuru Mwembe, amesema Manispaa hiyo ilitenga kiasi cha shilingi Bilioni mbili kwaajili ya ujenzi wa soko hilo ambazo zimekusudiwa kutoka kwa awamu mbili.

Na kueleza kuwa hadi sasa soko hilo limekamilika kwa awamu ya kwanza ambapo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 1.5 na Manispaa inatarajiwa kutoa kiasi cha Shilingi milioni 500, kwaajili ya ujenzi wa awamu ya pili ili kukamilisha soko hilo.


 
Back
Top Bottom