Tanzania njema,
Nakubaliana na wewe kwamba Mkandala si mtandao ila ni kweli ni swahiba wa JK!
siwezi kusema kwa hakikika kama DARUSO,RAAWU na UDASA walikuwa wanamuunga MKANDALA mkono moja kwa moja. ila ukweli ni kuwa katika hili kila mmoja na hasa wahadhiri walikuwa wana maoni yao huku wengine wakipinga na wengine wakimsupport.
Kaka Rwebugiri, JK hana swahiba....ana washirika wa kisiasa tu..
Tanzanianjema
kwa mujibu wa kiongozi wa juu wa DARUSO,ZITTO Amekataliwa kuingia mlimani..
utabiri umetimia,katiba inavunjwa waziwazi,angalia jinsi kijana wa sekondari ya pius msekwa anavyofuatwa na INTELIGENSIA!...MWALIMU FUFUKA UONE MADUDU YA ULIOWAKATAA,
hii itakuwa ni AMRI ya ndanda kosovo tu..si amerudi dar?
kuna kampeni itaanza karibuni ya kuwajibu wapinzani,stay tunned..
wanafunzi wameshasambaa maeneo ya theatre..taarifa nilizopewa ,zito alifanikiwa kuingia ndani ila uongozi wa chuo ukawatakalia kuzungumza na wanafunzi,
kweli tutafika?sasa tangu lini VC Akampangia mwanachuo mambo ya kuelezwa?
mie sijui tunakoenda-
Hii inatia mashaka sana tu,
Wakati ule tulikuwa tunasikia akina Mtikila kuwa walitemebelea sana pale Nkrumah Hall, iweje wakati huu wengine wakataliwe. Again, haya ndio tunaita makosa ya kiufundi kwa upande wa serikali................na hii inadhihirisha kuwa Zitto ana hoja inayochoma, na serikali wamekosa mafundi wa kuwajibia HOJA.
Zitto ni kama jipu linalowasumbua CCM, na CCM wanashindwa kuelewa ya kwamba
Dawa ya JIPU (Zitto) liache mpaka liive halafu litumbue halafu paka dawa, Ukilizuia wakati changa litaibuka sehemu nyingine ambayo yaweza kuwa mbaya zaidi....im afraid!!
Kwani ile Rev Square haipo tena siku hizi..............au ile Rev Square ni kwa ajili ya wanafunzi tu?
Habari zilizo nifikia muda huu zinasema Ukumbi pale Chuo ujemaa pomoni na watu wana ngoja kusikia maneno mazito toka kwa Ziito. Uongozi wa Chuo umekaa chonjo unasema hapana Zitto hawezi kuunguruma pale Mlimani maana Serikali haitapenda. Hizi ndiyo habari zinazo jiri na sijui mwisho wake ni upi . Natoka naelekea kunako maeneo nikiwa na nazidi nitawauma sikio. Ila kwa sasa huu ndiyo uhalisia wenyewe.
Wanafunzi ni wengi sana ila Zitto katakiwa kutogusa maeneo hayo ambayo ni makao ya wasomi wetu .
Wakuu heshima mbele, ninajaribu ku-read between the lines sipati the juice bado on this ishu,
kwa hiyo labda ningeomba more facts, kuanzia kibali cha Mbunge kuruhusiwa kuongea hapo chuoni, na sheria zote zinazohusiana na suala zima la kiongozi yoyote kuruhusiwa na uongozi wa shule kuongea hapo shuleni,
It is a high time sasa kwenye JF tukufu tuache songi songi, na tuweke facts kwanza, ili tuzichambue ipasavyo,
However, shukrani kwa wale mnaojitahidi kutuhabarisha na yanyojiri huko shuleni!
lakini katika hali yakushangaza uongozi wa chuo wakakwamisha kufanyika kwa majadala huo eti kisa zitto atakuwa mmoja wa public speakers. hapa alikuwa amealikwa kama mtanzania mwingine na hata kama hakuwa amealikwa alikuwa na uhuru wa kuhudhuria mjadala huu wa wazi pale mlimani
Zitto akatazwa kuongea UDSM
Wanafunzi wameandamana
habari zaidi zinakuja.. stay tunned