DOKEZO Uongozi Pori la Akiba Maswa umeshindwa kusimamia Haki za Msingi za Watumishi wake

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
1. Kumekuwa na utaratibu wa kusitishwa likizo za Watumishi wanapokuwa likizo na Afisa Mhifadhi II Fundi kwa kigezo cha uhaba wa Watumishi, pia kukataa kutoa ruhusa mbalimbali kwa Watumishi wakiwa na changamoto.

2. Kuna Watumishi wapatoa 6 hawafanyi majukumu yoyote ya Doria bila sababu za msingi isipokuwa kwa kigezo cha kuwa na misimamo kwenye yale wanayoamini, kusimamia haki zao za msingi, na kutoa taarifa mbalimbali za maovu zinazohusu Uongozi wa Pori hali inayopunguza nguvu kazi Kiutendaji.

3. Matumizi mabovu ya Pesa za OC na Kujilimbizika Malipo ya pesa kwa wakuu wa idara hali inayoeleka watumishi kutolipwa au kulipwa kwa kiwango kidogo sanaa. Kuwe na uwazi kwenye Jambo hilo Kuhusu Matumizi ya Fedha za OC kwani Pesa hutoka Juu na Kushindwa kufika chini kwa watumishi.

4. Changamoto ni nyingi ila haziongeleki kwenye vikao vya Ndani au Wakuu wa Taasisi kwani kufanya hivyo ni kutangaza Vita na Viongozi Wakuu wa Pori.

20240505_065035.jpg
 
Back
Top Bottom