Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 572
- 1,348
Kazi ya kutafuta miili ya watu watano wanaohofiwa kufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuzama ndani ya Ziwa Victoria imesitishwa kwa muda, kutokana na hali mbaya ndani ya ziwa, hivyo waokozi kushindwa kuona kutokana na kukosa vifaa.
Watu hao wanahofiwa kufariki dunia jana Septemba 15, 2024 saa moja usiku, wakati wakitoka Kijiji cha Mwiruruma wilayani Bunda walipokwenda kwenye harusi kwa upande wa bibi harusi.
Baada ya sherehe kuisha, ndugu wa bwana harusi walipanda mtumbwi kurudi nyumbani katika Kijiji cha Igundu kwa ajili ya maandalizi ya shughuli ya siku ya pili ambapo pamoja na mambo mengine walipanga kumfuata bibi harusi asubuhi ya leo, lakini mtumbwi huo ulipata ajali takriban kilomita moja na nusu kabla ya kufika kijijini Igundu.
Soma Pia: Mtumbwi wazama Ziwa Viktoria, mmoja afariki sita hwajulikani walipo
Akizungumza katika eneo la tukio leo Jumatatu Septemba 16, 2024, Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agustino Magere amesema kazi ya kuwatafuta watu hao ilianza leo alfajiri, lakini imeshindikana kutokana na wazamiaji kushindwa kuona ndani ya maji.
"Kuna tope jingi tena jeusi, lakini pia tumekutana na ukungu, hivyo tumeshidnwa kuendelea na utafutaji wa miili hiyo, tumesistisha kwa muda tukisuburi vifaa zaidi ambavyo vitafika hapa muda wowote," amesema.