Unyonyaji na utapeli wa madhehebu ya dini

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
26,084
62,774
UNYONYAJI NA UTAPELI WA MADHEHEBU YA DINI.

Kwa Mkono wa, Robert Heriel.

Angalizo; Makala hii inaweza isimfae kila mtu, hasa wale watu waliofunga fikra zao. Ikiwa wewe ni mmoja wao watu hao, tafadhali usisome jumbe hii. Lau kama unahitaji ukombozi wa Kifikra, uwanja ni wako.

Kila mmoja ana dhehebu lake, wachache sana wanaweza kujivunia madhehebu yao, katika uchunguzi wangu, hapa nchini, ni asilimia 5% tuu wanaojivunia madhehebu yao. Hii 95% hakuna anayejivunia isipokuwa tunajidanganya kwa upumbavu wetu.

Wahenga walisema, Kimfaacho tu chake, wakaongezea, Nguo ya kuazima haisitiri Mwili. Wengi wetu tumekuwa wahanga wa misemo hii. Asilimia kubwa tunaabudu katika madhehebu tuliyoazimmwa na wageni, naam ndio watu wa magharibi kutoka nchi za barafu na watu wa mashariki ya kati kutoka nchi za joto kali, nchi za ujangwa.

Dini na madhebu tuliyonayo wengi wetu ni kama nguo ya kuazima, kamwe haijawahi kutusitiri na ndio maana kupitia dini hizo tulifanywa watumwa na kuuzwa enzi za biashara ya utumwa, na baadaye dini hizo hizo zikatufanya tutawaliwe na kuwa makoloni.

Dini na madhehebu hayo ambazo ni nguo za kuazima, hazijatusiri na kamwe hazitatusitiri.

Hiyo ni mada ya siku nyingine, Leo nina mada fupi kidogo ambayo itakuwa sehemu ya maelezo niliyoyatanguliza.

Dini haijawahi kuletwa na Mungu na kamwe haitakuja kuletwa na Mungu.

Wakati Mungu akiumba Imani, wanadamu walitengeneza dini.
Wakati Mungu akiumba Akili, wanadamu walitengeneza Elimu.
Wakati Mungu akiumba Uzuri, wanadamu walitengeza Urembo
Wakati Mungu akiumba wakati, wanadamu walitengeza Kalenda

Sasa unaanza kunielewa, sio?
Jambo lolote lililotengenezwa na Binadamu sio lazima ila laweza kuwa Muhimu. Mtu anaweza kuishi bila DINI lakini kamwe hawezi kuishi bila imani. Mtu anaweza ishi bila elimu lakini kamwe mtu hawezi ishi bila akili. Nafikiri, subiri kidogo, sawa naona unaanza kunipata.

Dini kama ilivyo elimu lazima iambatane na jamii husika, kulingana na mazingira na utamaduni wa watu husika.
Dini inapaswa imilikiwa na jamii na sio kikundi cha watu,
Elimu inapaswa imilikiwa na jamii na wala sio kikundi cha watu.

Dini inatungwa kwa akili za watu tuu wala haina mahusiano na Mungu. Chenye mahusiano na Mungu ni Imani.

Dini karibia zote tulizo nazo ni utapeli na Unyonyaji Mtupu. Uongo! Uongo! Ujanja ujanja, ulaghai laghai, na mwishowe kabisa, ni kutisha watu hasa walio Mbumbumbu.

Mtu unapojitambulisha kuwa wewe ni dini au dhehebu fulani lazima ujiulize dini au dhehebu hilo ni lako kweli au ni nguo ya kuazima.
Kama ni dhehebu au dini yako basi huwezi tapeliwa kijinga jinga, kipuuzi puuzi.
Lakini kama Dini au dhehebu ulilopo ni Nguo ya kuazima basi hapo lazima utapeliwa, huna ujanja lazima upigwe tuu!

Dini ili isiwe ni utapeli au unyonyaji lazima iwe ya jamii fulani. Kama wewe ni Dhehebu fulani lazimma ufaidike na dhehebu hilo kwa nyanja zote za maisha.

Unaweza kujiuliza Dini au dhehebu ulilonalo linakusaidia nini kwenye maisha yako?
Dini lazima ikusaidie kiuchumi,kijamii, Kisiasa na Kiutamaduni.
Kama dini haijakusaidia katika maeneo hayo, au haikusaidii katika maeneo hayo jua unatapeliwa, unanyonywa, na kufanywa hamnazo.
Kuna watu wanazungumzia suala la kuzikwa, sijui, kuoa, sijui ubarikio, na mambo kama hayo.
Hayo mambo hayana msaada wowote kwako, Yaani uwe dini fulani kisa utazikwa, hahahah! Embu acha masihara, ati sijui hutabatizwa sijui kubarikiwa, embu tuweni sirius.

Ili ujue dini nyingi kama sio zote ni Unyonyaji na utapeli angali miradi inayofanywa na dini hizo;
Embu tuanze na Miradi ya Elimu kama shule, Vyuo vya kati na vyuo vikuu.

1. UNYONYAJI NA UTAPELI KATIKA SEKTA YA ELIMU
Hapana shaka, Sadaka yako ndio inayojenga shule za dini yako. Kama hujui hilo ni kwamba haufatilii tuu. Kama haijengi shule au chuo kilichopo katika nchi yako basi kinajenga katika nchi zingine. Yaani Sadaka za nchi ya huku zinajenga shule au chuo katika nchi nyingine.
Msingi mkuu wa mapato ya madhehebu ya Kidini ni Sadaka ambapo baadaye hujenga Miradi mingine kama vile Shule, Vyuo, hospitali, zahanati, Bank, Radio na Luninga.
Sadaka za waumini na watu binafsi wenye uwezo ndio hujenga Miradi hiyo.

Sasa lazima tujiulize Miradi hiyo ipo kwa ajili ya manufaa ya Nani?
Je waumini waliotoa sadaka? Au
Kwa ajili ya jamii husika kujumuisha na wasio wa dhehebu hilo? Au kwa ajili ya Viongozi wa madhehebu?

Viongozi wa dini watakuambia, tunaratajia kujenga shule ya dhehebu letu(Tuliite dhehebu hilo MNARA MWEKUNDU), Na chuo cha Mnara mwekundu.
Lengo la shule ya Mnara mwekundu ni kutoa elimu kwa jamii na kuwafikia watu wasio wa dhehebu letu ili wapate kumjua bwana wa majeshi. Pia Watoto wa waumini wa Mnara mwekundu watapata fursa ya kupeleka watoto wao kusoma katika shule hiyo. Hapa hapa ndio patamu.

Tuyaite majengo ya Ibada wanayosalia waumini wa Dhehebu la mnara mwekundu jina la MNARA, Hivyo shughuli zao zitakuwa zinafanyikwa ndani ya jengo la Mnarani(yaani ndani ya jengo lao la ibada Liitwalo Mnara).

Hivyo kila Mnara utawekewa Goli lake ili waumini wake wachange sadaka zitumwe kwenye ngazi za juu kwa ajili ya kujenga shule na chuo. Kumbuka, bila sadaka ya waumini hakuna Shule wala chuo kwa Dhehebbu la Mnara mwekundu.

Viongozi wa dhehebu ya Mnara watahamasisha kwa kila namna mpaka sadaka ya kujenga shule itakamilika. Hatimaye Shule ya SEKONDARI YA MNARA MWEKUNDU itakuwa imekamilika na Chuo chake.

Ajabu ni pale ambapo, gharama za Ada zitakuwa juu bila ya kujali huyu ni muumini aliyejengaa shule hiyo au sio Muumini. Hii itasababisha waumini wengi ambao kipato chao ni cha chini kushindwa kupeleka watoto wao katika shule za dhehebu lao wenyewe licha ya kuto sadaka.
Huo ni utapeli na unyonyaji mkubwa sana unaofanywa na dini zilizopo ambazo ni mfano wa dhehebu la MNARA Mwekundu.

Wewe mwenyewe unaweza kujiuliza, ukoo wenu wote ni dhehebu fulani, kila siku mnatoa sadaka, pengine sadaka zenu zimeshajenga shule na vyuo kibao, lakini shule hizo hazijakusaidia wewe wala ndugu zako kwa chochote kile, Elimu huna licha ya kuwa dini yako inashule na vyuo kibao ambavyo sadaka yako ndio imejenga.

Kwa nini Dini zisiwe kama serikali, Elimu ya serikali ni nafuu kwa sababu inachukua kodi kwa wananchi wake, ni shule za wananchi, ndio maana wanasoma kwa ada nafuu ikiwezekana wanasoma bure(japo sio bure kwani wazazi wanakatwa kodi au kulipa kodi) kwani kodi yao inakatwa.

Sasa elimu za taasisi za kidini unakuta ni gharama mpaka kwa wewe muumini wa dhehebu hilo licha ya kuwa sadaka yako au sadaka ya wazazi wako ndio imejenga shule hizo au vyuo hivyo. Huo kama sio unyonyaji ni nini? Angalau wangepunguza ada iwe nafuu kabisa kama ya serikali kwa waumini wa madhehebu yao, lakini wapi.

Yaani kijana akishafeli darasa la saba kama hana hela ya kwenda shule za binafsi ndio imekula kwake, wakati kuna shule za dhehebu lake zilizojengwa kwa sadaka yake au ya wazazi wake. Naye anasema Mungu anampenda, hahaha! Mungu hapendi watu wajinga na wanaotapeliwa kienyeji hivyo.

Ukisema dini hizi ni miradi ya watu fulani, waumini watakavyokubishia kama wamelogwa, mwambie kama hili ni dhehebu lako au lenu kwa nini huduma za kijamii mnapewa kwa gharama za juu wakati ninyi mnatoa Sadaka?
Kwa nini isiwepo gharama ya kawaida, bei nafuu ambayo kila muumini ataiweza?
Akikuambia habari za mishahara ya walimu na wafanyakazi, muulize kwani ada nafuu ya kawaida haiwezi kuwalipa hao wafanyakazi? Mpaka yawe mamilioni ya pesa?

2. SEKTA YA AFYA
Dhehebu la MNARA MWEKUNDU litaamua kujenga Hospitali au Zahanati ya dhehebu hilo kwa sadaka pia ya waumini.
Lakini utashangaa gharama za matibabu bado zipo juu hata kwa waumini wenyewe.
Mpaka unauliza lengo la kujenga hospitali hii ilikuwa ni nini hasa ikiwa mpaka wamiliki(waumini) wenyewe wanapaswa kutoa pesa nyingi mno.

3. KUTUMIA NGUVU KAZI YA NCHI BURE
Unakuta Dini au dhehebu inatumia vijana wakike na wakiume, wababa na kina Baba Bure kwa shughuli za dhehebu. Mfano waimbaji walipaswa walipwe kwa kazi yao ya uimbaji kwa kila mwezi, lakini watakuambia unamuimbia Mungu, nani kasema hayo, nani kasema Mungu anaimbiwa, Mbona viongozi wa dini wanalipwa? Wao hawamhubirii Mungu sio? Kuimba ni kazi kama Kuhubiri,
Msitake vijana na Mabinti wa watu wapoteze muda wao bure bila kuwapa mishahara yao, mbona ninyi mnapewa?
Unakuta kijana au binti anahangaika na KWAYA ya bure huku akipoteza muda wake. Wapeni waimbaji mishahara kama sehemu ya wahudumu wa dhehebu lenu. Acheni kudharau karama za wenzenu.

Tangazeni kazi ya uimbaji, watu watume maombi, wafanyiwe usaili, kisha wapewe mkataba iwe wa miaka miwili, mitatu au mitano sawa. Wapeni na malipo kabisa. Sio hamuwapi mishahara lakini sheria kibaaaooo! Sheria nyingi bila malipo. Acheni hizo, ninyi wawaimbia bure tuu kwenye mikutano yenu, ibada zenu, alafu malipo yao ni SARE, Sio?

Mimi nilishasema, mke wangu au mwanangu akiwa chini yangu hawezi kufanya mambo ya bure,

Lipeni posho mashemasi, sijui watunza kumbukumbu, watunza pesa, mbona walinzi mnawalipa, pawepo na mkataba kabisa, wenye malipo yanayofahamika. Watu wafanye kazi kwa hela.

Mtu apige kinanda bure, ati apewe posho tuu, mbona mnadharau kazi za watu, wapambaji walipeni, wasafisha jengo la ibada wapeni malipo yao yawe specific na yafahamike.

Hatutaki Mungu wa Bure sisi, Mungu wa Matabaka, yaani wengine walipwe mishahara wengine posho, na wengine wasipewe kabisa na wote ni watumishi wa dhehebu lile lile. Uliona wapi hiyo kama sio kwenye unyonyaji na utapeli.

Kama hamuwezi, acheni vijana wakaimbe nyimbo za kijamii kama Singeli, Bongo Fleva, Gospel, na HipHop. Huko wakafanye kazi ya kuifunza na kuburudisha jamii huku nao wakijipatia kipato. Kwani lengo la kuimba si ndio hilo. Hayo ya kumuimbia Mungu ni maneno ya wizi, na uongo uongo tuu.

Mungu hahitaji kuimbiwa, hajawahi kuimbiwa na hatakuja kuimbiwa. Mungu sio mhitaji.
Sisi ndio tunaimbiana, tunahubiriana, tunaelimishana, yote tunafanya kwa ajili yetu wala sio kwaajili ya Mungu.

Dini ziache kutapeli watu, kunyonya nguvu zao, kunyonya akili zao, kunyonya Muda wao, na kunyonya karama zao huku hazitaki kuwalipa chochote.

Taikon nimemaliza Muumini wa Dhehebu la Mnara mwekundu

Ulikuwa nami;

Robet Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Heheh eti mnara mwekundu! Afu hao waumini wa mnara mwekundu ndo wanaonaga waumini wengine kama wa gwajiboy, mwampo, kobe and like wanapigwa kumbe wao ndo wanapigwa zaidi...shule,vyuo na hospitali zao ni expensive kiasi kwamba hata wao wenyewe kama wanufaika zinawashinda
 
Nilishawahi kwenda kanisa la efata lipo kanda ya ziwa nmeona nilitaje kabisa nisiwe mnafiki maana "mwenyezi MUNGU hataki" nikasikia mchungaji akisema SITAKI WATU WASIO NA PESA HUMU KANISANI moyo uliniuma sana nkatoka njee huyu mchungaji alipandikiza mbegu mbaya sana na ikizingatia kipindi kile kilikuwa npo kijana mdogo sana naehtaji kumjua MUNGU vilivyo
 
Serikali elimu ni nafuu kwa sababu wa akusanya kodi dini elimu ghari kwa sababu hawakusanyi kodi pia sadaka pekee aitoshi toa huduma ya shule au hospitali mfano mzuri nakupa makongo sec, airwing sec, jitegemee sec hizi ni shule zipo chini ya jeshi jeshi ni serikali lkn shule hizi ada zao ni kubwa na ziko juu ukilinganisha na shule za azania, jangwani, kisutu kwaiyo basi dini taasisi zake aziwezi jiendesha kwa sadaka tuu mana sadaka ni ndogo aitoshi pia sadaka ina kazi nyingi sana.
 
Serikali elimu ni nafuu kwa sababu wa akusanya kodi dini elimu ghari kwa sababu hawakusanyi kodi pia sadaka pekee aitoshi toa huduma ya shule au hospitali mfano mzuri nakupa makongo sec,airwing sec,jitegemee sec hizi ni shule zipo chini ya jeshi jeshi ni serikali lkn shule hizi ada zao ni kubwa na ziko juu ukilinganisha na shule za azania,jangwani,kisutu kwaiyo basi dini taasisi zake aziwezi jiendesha kwa sadaka tuu mana sadaka ni ndogo aitoshi pia sadaka ina kazi nyingi sana.

Sadaka na zaka hazitoshi? Hahahah! Unajua kwa nini hazitoshi hizo Sadaka au unajua kwa nini watu hawatoa zaka? Jibu ni kuwa hawaoni faida yake, wewe utoe sadaka ikajenge shule wakati unajua wazi kuwa hautafaidika na chochote kwenye hizo shule, uliona wapi?
Wapunguze gharama za ada kwa waumini wao kwa sababu wao ndio wamiliki na ndio wanaotoa zaka na sadaka.

Sijasema wasome bure, japo uwezekano huo upo
 
Mm church natatajia kwenda huko tar 19-Dec tangu 2008 na yote ni kwa ajili ya kumbatiza mtoto wangu

Mwaka 2006 nlichaguliwa kwenda maua seminary form 5&6 cha ajabu ada ndio ilikuwa hatar 750k per year wakat kikwete anatoa elimu ile ile kwa 70k nkatemana nao

Just imagine 2006 ada ni 750k je sasa hiv itakuwa kiasi gani?
 
Mm church natatajia kwenda huko tar 19-Dec tangu 2008 na yote ni kwa ajili ya kumbatiza mtoto wangu

Mwaka 2006 nlichaguliwa kwenda maua seminary form 5&6 cha ajabu ada ndio ilikuwa hatar 750k per year wakat kikwete anatoa elimu ile ile kwa 70k nkatemana nao

Just imagine 2006 ada ni 750k je sasa hiv itakuwa kiasi gani?

Alafu unaambiwa ni shule ya dhehebu lako? Hahahaha!

Watu waache wizi. unyonyaji na utapeli.

Mara nyingi naamini Serikali ndio Dini. Kwani ndio inaweza kukupa huduma nyingi kwa gharama nafuu
 
Back
Top Bottom